Ex wife wa tiger wood mzima kweli????

A fool is a fool! They never learn! Hujaona mjini hapa mtu anapata kazi nzuri ananunua V8 na kupanga mansion ufukwe wa kigamboni, anafanya party ya kuhamia nyumba ya kupanga? Analipia clowns wa fun city na mwalimu wa kufundisha watu kuogelea. Vipo mjini humu wifi! Na waliofilisika anawajua, sie twaenda kula mishkaki na kutambaa!

Hahahaha. . . .kweli watu ni noma. Sema tatizo watu huwa hawafikirii kwamba hata nae yanaweza yakamkuta ya kumkuta. Tena utakuta wanasema kabisa "fulani mjinga kweli, alichezea pesa sasa hana kitu" kumbe nao ni muda tu haujafika.
 
Chezeiya machalii wa mererani eh? How many times do they fall back and forth?

Hahahaha wale ni funiko wifi. Nakumbuka nyumbani walikua wanakuja wiki kijiji kizima kinakunywa kwa bill yao, kelele za pikipiki mpaka kunakucha, wanaopendwa wanakula nyama mpaka wanakinahi alafu wanaenda Arusha kula raha. Baada ya mwezi unasikia fulani karudi machimboni, akija nyumbani ananyweaaaa mpaka abahatike tena. Alafu hua hawajifunzi, wanarudia yale yale.
 
Asee huyu uncle kama angepata tena pesa angerudia mchezo wake wa zamani manake watu walimcheka na wanamcheka mpaka leo, so lazima angetaka kuwaringishia na kurudisha heshima iliyopotea. Watu wangekoma manake pasingetosha.
Dah, hapo patam kweli.
 
Hahahaha. . . .kweli watu ni noma. Sema tatizo watu huwa hawafikirii kwamba hata nae yanaweza yakamkuta ya kumkuta. Tena utakuta wanasema kabisa "fulani mjinga kweli, alichezea pesa sasa hana kitu" kumbe nao ni muda tu haujafika.

hiyo ndo sana
mjini hapa watu wanabadili maagari kutwa huku kujenga wanaona ujinga
akifilisika ndo baasi.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom