Ex wangu aliniacha mwenyewe, sasa ananiblock mitandaoni.

Ex wangu aliniacha mwenyewe, sasa ananiblock mitandaoni.

Mkuu, nishamove on muda mrefu ila nimeshangaa tu kwa nini aniblock na kwa nini afanye hvyo sasa wakati tuna miezi karbu 11 toka tumeachana.
Hapo hupaswi kushangaa tena kwa hiyo miezi 11 ulitakiwa umblock mapema sana, hata mimi nikiachana na mwanamke cha kwanza namblock kila mahali especially kwenye hizi social media ili nimsahau kwa haraka sana.Nilichogundua ni kwamba inaonekana wewe bado unampenda huyo msichana ingawa yeye hakuhitaji tena sababu kama ungekua umeshakubali ku move on basi sidhani kama ungekua na haja ya kulalamika juu ya hili.Nakushauri achana na huyo binti asikuumize kichwa, kama kuna mtu anamdanganya basi kuna siku lazima atarudi kwa machozi mark my words brother.Inawezekana kapata kijamaa ndo kinamzuzua kwasasa ila kijamaa kikishamchoka atarudi kukulilia mrudiane sasabu sisi wanaume baba yetu ni mmoja, kabla hatujamvua nguo mwanamke huwa tunamuonesha mapenzi ya dhati kabisa lakini ukishatembea nae mara mbili tatu basi unamuona wa kawaida sana na hana jipya.Kubali matokeo na kama hujawahi kumkosea basi naamini atarudi kukupigia magoti.
 
Pole sana. Nikiangalia uandishi wako inaelekea bado unampenda sana huyu binti. Sasa na wewe kwa kuwa alishakuacha na wewe achana naye jumla. Tumia fursa hii ya kukublock ili imalize kabisa shauku au hali yako ya kutaka kumuona kupitia picha zake.
 
sasa unalia lia nini kisa amekupa block...mtoto wakiume usijitetee sana huachagia u sijui mnaongea baada ya kuachana...we mwanaume hata siku moja hamtamkii mwanamke hamtaki au anamuacha anatulia anapiga mishe zake,,wadada ndio watublock na kututamkia ila acha kulia lia ukiblokiwa
 
Sasa hapo kinakuuma kipi mtu hakulishi,hakuvishi ya nini kuumia ebu acha utoto fanya vitu vya maana.
 
Kafanya jambo zuri kukublock,kilichokuwa kikiwaunganisha ninyi ni mahusiano ya kimapenzi na si kingine mkuu.
Kama mapenzi yamekwisha,unadhani mtawasiliana nini tena?shukuru kakusaidia,na ukubali kuendelea na maisha pasipo yeye mkuu.
 
Jifunze kubalance shobo.
Huyu mwanamke sijui anateseka au ana shida gani.

Aliniacha mwenyewe mwaka jana, nikajaribu kumbembeleza akakataa akasema nikubali tuwe marafiki tu vinginevyo nimsahau.

Kwa bahati nzuri au mbaya huyu binti aliwahi kunitambulisha kwa baba yake, baba yake tulikua tukiwasiliana mara moja moja, siku moja akanipigia tukaongea, akaniuliza tunaendeleaje, nimamwambia vizuri ila sio sana, akanisisitiza nimwambie kama kuna shida, nikamwambia tuko poa, baadae akampigia binti yake, wakaongea wanayoyajua, baadae binti yake akanipigia akasema nisiwasiliane na baba yake, nikakubaliana nae bila kinyongo.

Baada ya hapo sikuwahi kumpigia sim wala meseji, hata yeye hajawahi kunipigia wala kunitafta, ila alikua rafiki yangu facebook, instagram, twitter na kwingine.

Amekua akipakia picha zake insta story, naangalia bila shida, jana nikaona kapakia picha asubuhi, baadae sikuiona, nikamtafta sikuona hata jina lake, nikamtafta facebook, twitter na huko kwingine sikuona jina lake, nikajua kaniblock kila mahala.

Nashindwa kuelewa, sina ugomvi na yeye, aliniacha mwenyewe, ni miezi mingi sasa, sasa sijui amewaza au anateseka nini hadi kuniblock.

Katika maisha yangu huyu ndie mwanamke alieniacha(ofcourse sina tabia ya kuacha mwanamke labda aniache yeye) ambae ameniblock social media zote na ambae siwasiliani nae, wengine wote tunawasiliana kama kawaida hata kama wana watu wao na wengine wameolewa na wengine wakipata shida wanatuma invoice, kama naweza naiclear.

Kwa wale mnaowaelewa wanawake vizuri, Kwa huyu shida iko wapi wakuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mlishaachana, kublokiwa kila mahali kunakushtua nini sasa...

Aliyempata ndiyo kamwambia akublock kila mahali na aachane na wewe kabisa... akiachika ataku-unblock...

Cc: mahondaw
 
MIMI HILO LIMENIKUTA...

ALINIACHA MWENYEWE...AKAENDA KWA WAKE WA SIKU ZOTE ALIYENICHEAT NAE...MIMI NIKASEMA HAMNA NOMA...JAPO NILITESEKA SANA...NIKAONA NIMPOTEZEE...JAPO YEYE ALILIA ETI TUENDELEE KUWA FRIENDS...NIKASEMA SIWEZI KUMWACHA KWA MTINDO HUO...HUKU AKAWA ANAMPOST POST BWANA AKE...
NIKAMPOTEZEA KABISA...MAANA NI SAWA NA KUTEMBELEA MUWA KAMA MKONGOJO...

BAADAE NIKAPATA BINT MZURI ALIYETULIA ALINIPENDA KWELI NA NIKAMPENDA KWELI...NA NAMUAMINI ASILIMIA 99.0...ALLAH AKANITUNUKU MTOTO MZURIIIIIII KUTOKA KWA MALKIA HUYO...

NIKAMTAFUTA SASA NIPO TAYARI TUENDELEE KUWA MARAFIKI...KUACHANA SIO UADUI...ILI TUBALANCE SASA...

NIKASHANGAA MTU KACHANGE...ANANICHUKIA TENA...HAPOKEI SIMU WALA HANIPIGII KAMA ZAMANI...HANITUMII TEXTS TENA...

MBAYA ZAIDI ALINIBLOCK WHATSAPP...

NIKACHEKA TU...MKUKI KWA NGURUWE...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mwanamke sijui anateseka au ana shida gani.

Aliniacha mwenyewe mwaka jana, nikajaribu kumbembeleza akakataa akasema nikubali tuwe marafiki tu vinginevyo nimsahau.

Kwa bahati nzuri au mbaya huyu binti aliwahi kunitambulisha kwa baba yake, baba yake tulikua tukiwasiliana mara moja moja, siku moja akanipigia tukaongea, akaniuliza tunaendeleaje, nimamwambia vizuri ila sio sana, akanisisitiza nimwambie kama kuna shida, nikamwambia tuko poa, baadae akampigia binti yake, wakaongea wanayoyajua, baadae binti yake akanipigia akasema nisiwasiliane na baba yake, nikakubaliana nae bila kinyongo.

Baada ya hapo sikuwahi kumpigia sim wala meseji, hata yeye hajawahi kunipigia wala kunitafta, ila alikua rafiki yangu facebook, instagram, twitter na kwingine.

Amekua akipakia picha zake insta story, naangalia bila shida, jana nikaona kapakia picha asubuhi, baadae sikuiona, nikamtafta sikuona hata jina lake, nikamtafta facebook, twitter na huko kwingine sikuona jina lake, nikajua kaniblock kila mahala.

Nashindwa kuelewa, sina ugomvi na yeye, aliniacha mwenyewe, ni miezi mingi sasa, sasa sijui amewaza au anateseka nini hadi kuniblock.

Katika maisha yangu huyu ndie mwanamke alieniacha(ofcourse sina tabia ya kuacha mwanamke labda aniache yeye) ambae ameniblock social media zote na ambae siwasiliani nae, wengine wote tunawasiliana kama kawaida hata kama wana watu wao na wengine wameolewa na wengine wakipata shida wanatuma invoice, kama naweza naiclear.

Kwa wale mnaowaelewa wanawake vizuri, Kwa huyu shida iko wapi wakuu?
Mimi tu ndo ntaekuambia ukweli achana na ushauri wowote.

Kaka ukiachwa achika sasa unafuatilia mambo yake ya nini ? Huyu dada hakupendi hata tone akikuona ni kama kaona kinyesi kibichi .

Fikiria baba yake alimuuliza mna tatizo ,akamjibu baba sasa Mimi mile kinyago ka kingwendu nakipeleka wapi,dingi akajibu dah afadhali ungeniharibia sura za wajukuu .

Bro na ww mblock.
 
Jibu rahisi sana, amepata mume mwingine kwahiyo anahitaji awe peke yake zaidi. Usimsumbue, kwani unateseka? Ingelikuwa anakutafuta namna fulani ndio ungelileta huo uzi wako. Kifupi mantiki ya uzi wako haiendani na title. Amekublock kila mahali maana yake fanya yako, usimsumbue. Na ndio namna pekee ya kumsahau mpenzi wako wa zamani upo hapo
 
Back
Top Bottom