Ex wangu aliniacha mwenyewe, sasa ananiblock mitandaoni.

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
1,853
2,000
Huyu mwanamke sijui anateseka au ana shida gani.

Aliniacha mwenyewe mwaka jana, nikajaribu kumbembeleza akakataa akasema nikubali tuwe marafiki tu vinginevyo nimsahau.

Kwa bahati nzuri au mbaya huyu binti aliwahi kunitambulisha kwa baba yake, baba yake tulikua tukiwasiliana mara moja moja, siku moja akanipigia tukaongea, akaniuliza tunaendeleaje, nimamwambia vizuri ila sio sana, akanisisitiza nimwambie kama kuna shida, nikamwambia tuko poa, baadae akampigia binti yake, wakaongea wanayoyajua, baadae binti yake akanipigia akasema nisiwasiliane na baba yake, nikakubaliana nae bila kinyongo.

Baada ya hapo sikuwahi kumpigia sim wala meseji, hata yeye hajawahi kunipigia wala kunitafta, ila alikua rafiki yangu facebook, instagram, twitter na kwingine.

Amekua akipakia picha zake insta story, naangalia bila shida, jana nikaona kapakia picha asubuhi, baadae sikuiona, nikamtafta sikuona hata jina lake, nikamtafta facebook, twitter na huko kwingine sikuona jina lake, nikajua kaniblock kila mahala.

Nashindwa kuelewa, sina ugomvi na yeye, aliniacha mwenyewe, ni miezi mingi sasa, sasa sijui amewaza au anateseka nini hadi kuniblock.

Katika maisha yangu huyu ndie mwanamke alieniacha(ofcourse sina tabia ya kuacha mwanamke labda aniache yeye) ambae ameniblock social media zote na ambae siwasiliani nae, wengine wote tunawasiliana kama kawaida hata kama wana watu wao na wengine wameolewa na wengine wakipata shida wanatuma invoice, kama naweza naiclear.

Kwa wale mnaowaelewa wanawake vizuri, Kwa huyu shida iko wapi wakuu?
 

Chimunguru

JF-Expert Member
May 3, 2009
10,590
2,000
Bado unampenda, kwani akikublock Facebook mtaani hamuonani? Mkikutana barabarani atakublock vile vile? Huwajui wanawake wewe achana na huyo opportunist.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom