Wivu huoni lakini roho inauma. Ulimwachia nini?
Umegeuka hadithi ya Sungura na Zabibu, alipoona hawezi kuzipata akasema 'sizitaki zile mbovu'
Pole sana yeye amemchagua mwenyewe bila ya kulazimishwa.
Yani tangu tulipoachana 2005 sijawahi kum-miss wala nini, yani hata ikitokea tumeonana ni hi hi hakuna zaidi. Lakini saa hizi ninapofikiria kuwa yuko kwenye honeymoon na yule mrugaruga niliyemwona juzi, no, hapana, haikubaliki aise!
Onyesha heshima kwa mume wa huyo dada!
Yani tangu tulipoachana 2005 sijawahi kum-miss wala nini, yani hata ikitokea tumeonana ni hi hi hakuna zaidi. Lakini saa hizi ninapofikiria kuwa yuko kwenye honeymoon na yule mrugaruga niliyemwona juzi, no, hapana, haikubaliki aise!
Samahani mkuu, nimeeleza tu hisia zangu kwa nilichoona alhamisi 9 Dec 2010
We vipi mzima kweli
Yeye anajua anachokipata ndo maana kamchagua
na alikupiga chini maana wewe ndo ulikuwa huna sifa za kuwa naye
alah....
dah.....naweza nikakuelewa vizuri tu...pole sana.....ambao hawajawahi kukutwa na hali hii hawawezi kukuelewa.......jitahidi uwe busy usahau hayo mambo........ni hilo tu kutoka kwangu
Habari ndungu huwa sitembelei anga hizi lakini naona hapa imebidi....... Kama ameolewa hatakuwaje demu wako tena..... jamaa hamfai???? kumbuka..... True love is not finding a perfect man, but loving an imperfect man perfectly...
Tuliachanaga miaka mingi sana kwa hiyo nilijua sina hisia yoyote naye tena. Alivyonijulisha anaolewa anaomba mchango wa send-off nikamchangia kama kawaida na send-off nimeshiriki sherehe juzi 9 December. Sasa sijui ni kwanini nilipomwona yule mchumba wake alhamisi ile, nikaanza kuhisi kwenye nafsi yangu kwamba yule jamaa hamfai, yaani kwa ninavyomfahamu yule dada ile siyo type yake kabisa! Dada kakosea kuchagua bana, no! Siwezi kueleza hii hali, naamini siyo wivu but no, siyo yule kabisa bana!