EWURA yatangaza Bei mpya za mafuta, Petroli na Diesel bei zaporomoka

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei elekezi za mafuta zitakazoanza kutumia kuanzia keshi Mei 2, 2018.

Katika taarifa ya EWURA, bei za rejareja za mafuta ya petroli zimepungua kwa TZS 88 kwa lita moja, dizeli imepungua kwa TZS 61 kwa lita moja, huku mafuta ya taa yakipanda kwa TZS 2 kwa lita moja.

Aidha kwa upande wa bei za jumla, bei za mafuta yote zimepungua ambapo petroli imepungua kwa TZS 100.91 kwa lita moja, dizeli TZS 73.71 kwa lita na mafuta ya taa TZS 10.49 kwa lita moja.
 
Attachments

  • Cap-Prices-wef-02-May-2018-ENGLISH.pdf
    986.3 KB · Views: 235
Wapandishe tu, na mshahara wasiongeze, waendelee kusema uchumi mzuri, uzuri hawajuwi bei za nyanya, vitunguu, sukari, mafuta ya kula, mchele wala unga, na ndio maana wanapata hata akili ya kupandisha kila kitu!
Waendelee kuponda maisha huku sisi tukibeba mzigo wa raha zao, wajilinde hata na na mamizinga majumbani kwao tusije kuwavamia kwa kisingizio kwamba tuna njaaa..
Waendelee kuishi kama mbinguni..
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei elekezi za mafuta zitakazoanza kutumia kuanzia keshi Mei 2, 2018.

Katika taarifa ya EWURA, bei za rejareja za mafuta ya petroli zimepungua kwa TZS 88 kwa lita moja, dizeli imepungua kwa TZS 61 kwa lita moja, huku mafuta ya taa yakipanda kwa TZS 2 kwa lita moja.

Aidha kwa upande wa bei za jumla, bei za mafuta yote zimepungua ambapo petroli imepungua kwa TZS 100.91 kwa lita moja, dizeli TZS 73.71 kwa lita na mafuta ya taa TZS 10.49 kwa lita moja.
Shukran mkuu, lkn apo kwenye mafuta ya taa sjaelewa aise.
Yaani kwa Bei za reja reja mafuta ya taa yamepanda kwa Tsh 2, na kwa Bei ya jumla mafuta ya Taa yamepungua bei kwa tsh 10.49 , Hii point nifikirishi sana ,kuna nn hapo ?
Yaani bidhaa inayotumiwa na Watanzani wengi tulio na kipato cha chini ambao ni Masikini wapiga kura wa MAGUFULI ishuke kwa mfanya biashara zen masikini aneitafuta kwa ugumu tsh ipande ?
EWURA hapa mm huwa siwaelewi kabisa, hata kama hii bidhaa ni adimu kwa nn mfanya biashara apunguziwe na final consumer apandishiwe, cc tulio masikini hatuwezi kununua kwa Bei hiyo ya jumla maana inataka uchukue mzigo Mkubwa,uwezo wetu ni kuchukua kidogo kidogo na kutumia .
EWURA this is not fair, Leo hii eti niende dukani kununua mafuta ya Taa niambiwe na muuzaji kuwa YAMEPANDA BEI, wakati kumbe mmepunguza Bei , idiot and shame on you EWURA.
 
Mbona naona kama imepanda huu uzi unapotosha jana nimeweka mafuta kwa 2,171 nikiwa Kia~Kilimanjaro hapo kwenye bandiko naona inatakiwa kuwa 2,175...Sasa imepanda au imeshuka?
 
Mafuta yote Yamepanda Bei...
 
jamaa wanajiandaa kupandisha bei bila shaka...mara itakapo panda itakuwa kwa sh 200
Soma uhalisia kwenye hiyo Chat, mafuta yamepanda Bei, hawa watu hawa wanacheza na akili za watu.
Makumbafu sana
 
Mbona naona kama imepanda huu uzi unapotosha jana nimeweka mafuta kwa 2,171 nikiwa Kia~Kilimanjaro hapo kwenye bandiko naona inatakiwa kuwa 2,175...Sasa imepanda au imeshuka?
Soma hiyo PDF mkuu, ww unazungumzia Jana wakati imetangazwa itaanza kutumika trh 2 may, we jamaa vipi, soma vizuri post ya MTU, una haraka gani
 
Mkuu, nimeisoma vizuri hiyo PDF nasema jana nimejaza mafuta kituo kilichopo KIA wilaya ya Hai na bei ilikuwa ni Tsh.2,171 per Litter, kwenye hiyo bei mpya inasoma Tsh 2,175 kwa lita, hapo mafuta yamepanda au yameshuka?
 
We Fanya hivi, kesho c ndo zinaanza kutumika kajaze wese then tupeane mrejesho hapahapa ,tuone kama ni kweli au laah.
Huwezi jua ,yawezekana labda taarifa imetoshwa na wazee wa Lumumba ili kuficha ukweli.
Ukweli utajulikana
 
Back
Top Bottom