Ewura yashusha tena bei ya mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ewura yashusha tena bei ya mafuta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 29, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 28 August 2011 20:38[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Raymond Kaminyoge

  MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imeshusha bei ya mafuta kuanzia leo.Kwa hatua hiyo, bei ya ukomo ya petroli kwa Mkoa wa Dar es Salaam sasa itakuwa Sh2,070, huku dizeli ikiwa Sh1,999 na mafuta ya taa Sh1,980. Bei ya ukomo wa bidhaa hiyo itatofautiana kulingana na umbali wa maeneo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu alisema hiyo ni kutokana na kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia.Alisema ikilinganishwa na bei ya zamani, petroli imeshuka kwa Sh44.55 sawa na asilimia 2.11 huku dizeli ikishuka kwa Sh31.99 sawa na asilimia 1.57 na mafuta ya taa yakishuka kwa Sh25.62 sawa na asilimia 1.28.Mnamo Agosti 2, Ewura, ilishusha bei ya mafuta.

  Petroli ilishuka kwa Sh202.37 kwa lita ambayo ilikuwa ni sawa na asimilia 9.17, dizeli kwa Sh173.49 sawa na asilimia 8.32 na mafuta ya taa kwa 181.37, sawa na asilimia 8.70 hali iliyosababisha vurugu na uhaba wa bidhaa hiyo.

  Lakini, siku 11 baada ya kushusha bei hiyo, Ewura ilipandisha tena bei ya mafuta kutokana na kile ilichodai kuwa ni kupanda bei katika soko la dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania na kusababisha Bodi ya mamlaka hiyo kubanwa na Baraza la Mawaziri.

  Jana, Masebu akitangaza nafuu hiyo ya bei ya mafuta, alisisitiza: " Tutaendelea kukokotoa bei za bidhaa za mafuta kila baada ya wiki mbili, hiyo itatokana na mabadiliko ya bei ya bidhaa za mafuta katika soko la dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na Dola ya Marekani."

  Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei ya mafuta zitaendelea kupangwa na soko... " Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta."

  Alisema kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta kwa bei ya ushindani ili mradi ziko chini ya bei ya kikomo.

  "Wafanyabiashara na wateja wakubaliane na bei zitakazopangwa na Ewura kwa kuwa bidhaa za mafuta zinabadilika mara kwa mara," alisema.

  Masebu alisema vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei ya bidhaa hiyo katika mabango yanayoonekana bayana na kuwataka wateja kununua mafuta katika vituo vinavyouza kwa bei ya chini ili kuhamasisha ushindani.

  "Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo kitakachokiuka agizo hilo," alisema Masebu.

  Alisema wanunuzi wanashauriwa kudai stakabadhi ya malipo inayoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei yake kwa lita.

  "Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo yenye kiwango cha ubora usiofaa," alisema Masebu.

  Bei kikomo kwa kanda Kwa mujibu wa jedwali la Ewura, bei ya petroli kwa Mkoa wa Arusha sasa ni Sh2,154, huku dizeli ikiwa Sh2,083 na mafuta ya taa Sh2,064.Mkoa wa Dodoma petroli itauzwa kwa Sh2,128, dizeli Sh2,058 na mafuta ya taa Sh2,038.Katika mkoa wa Mwanza petroli sasa ni Sh2,219 huku dizeli Sh2,149 na mafuta ya taa Sh2,130.Jedwali hilo la bei linaonyesha kwamba, bei kwa mkoa wa Mbeya petroli itauzwa kwa Sh2,176 huku dizeli ikiuzwa kwa Sh2,106 na mafuta ya taa kwa Sh2,087.Mkoa wa Kigoma petroli itauzwa kwa Sh2,301, dizeli Sh2,230 na mafuta ya taa Sh2,211.

  Tetesi za vitishoMkurugenzi huyo alisema kuna tetesi za baadhi ya wamiliki wa vituo vya mafuta wanaotii maagizo ya Serikali kutishiwa na washindani wao.
  Alisema wamiliki hao wamekuwa wakiwatishia wenzao wanaopinga maagizo ya Serikali kwa kutaka waungane nao ili wawe na nguvu katika madai yao.

  "Siwezi kuingia kwa undani kama nilivyosema hizi ni tetesi ambazo tunazifanyia kazi, ikibainika watakuwa wanatenda kosa na watachukuliwa hatua za kisheria," alisema Masebu.

  Vituo vya mafuta vyafungiwa Mamlaka hiyo imevifunga vituo vitatu vya mafuta katika Mikoa ya Dar es Salaam, Iringa, Mwanza kutokana na kuvunja sheria.

  Ofisa Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo alisema kwa Dar es Salaam Kituo cha mafuta cha Kobil kilichopo Kigamboni kimefungiwa kutokana na kuuza mafuta yaliyochakachuliwa.Alisema kituo hicho ambacho kilifungiwa Agosti 26, mwaka huu, kimepewa siku saba kujieleza kwa nini kisichukuliwe hatua za zaidi za kisheria kwa kosa hilo.

  Kaguo alisema kituo kingine kilichofungiwa ni Hass Magu kilichopo Magu, Mwanza ambacho baada ya kufungiwa na Ewura kiliendelea kuuza mafuta.Kingine kilichofungiwa ni Mafinga Petrol Station ambacho uongozi wake uliwakataza wakaguzi wa Ewura kufanya kazi yao.

  "Kwa hiyo ninataka kuwaeleza wananchi kwamba Ewura tupo kila mahali, tutawachukulia hatua wale wote wanaokiuka sheria," alisema Kaguo.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Kazi kwelikweli
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Meaningless!
  Kama serikali haiwezi kusubsdise kweny eneo hili kila siku itakuwa ni kutangaziwa bei mpya za kupanda na kushuka kama homa za vipindi!
  I thought the Governmet would intervene in the name of stabilization!...wajue kuwa tunahesabu na kunukuu huu usumbufu wa kutwa kucha!
   
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,486
  Trophy Points: 280
  Kaazi kweli kweli.......:bump:
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Shiling imeshapanda?
  Last tyme walisema mafuta yanapanda bei kwakuwa shiling ya Kitanzania imeshuka dhidi ya dolla. Swali ni kwamba shiling imepanda? Wiz mtupu
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  ukisikia pwaaaa
   
 7. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #7
  Aug 29, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  kichefuchefu tena leo
   
 8. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,676
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Ndiyo mafuta yanavyouzwa!! mafuta si chumvi.
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Hakuna punguzo lolote ni mwizi mtupu.
   
 10. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,506
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kweli nimesikia kichefuchefu siku mbaya leo
   
 11. V

  Vonix JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,987
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Mchezo mchafu hayo mafuta yanayoshushwa bei ni yapi?????stock mpya ipi???alafu baada ya wiki moja watayapandisha wakidai shilingi imeshuka bei, mafuta yaleyale kwenye tank unayashusha na kuyapandisha bei ndio taabu ya kuajiri form six na form four kwenye ofisi nyeti kama hizo.kwa tank lenye uwezo wa kuhifadhi 10,000,000lts tutegemee baada ya wiki mbili liwe limeisha??????jipangeni upya hapo hamna kitu.
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Hivi kwanini EWURA isifutwe? Nadhani Jairo alikuwa kwenye mkakati huo!
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Aug 29, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  kwa hiyo masebu katangaza bei ya mafuta kwa dar peke yake? kwanini asitangaze na mikoa mingine, anaposema bei itategemeana na umbali anamaanisha nini nyambaf yake.
   
 14. p

  pimbika Member

  #14
  Aug 29, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si chochote wala lolote huu ni utapia mlo............wakipandisha itakuwa 3000 halafu watashusha iwe 2800
   
 15. p

  plawala JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngeleja alikuwa na mpango huo,ingawa hata kama ikifutwa litakuja balaa jingine
   
 16. s

  samko Member

  #16
  Aug 29, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huku kwetu kandaya ziwa ytashuka?
   
 17. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,163
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  Sion walipo shusha!
   
 18. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kinachonichekesha ni kuwa kuna a significant number of stations hawauzi mafuta, wanasema yamekwisha, specifically petrol!!! Serikali ni legelege tu, hata ikitoa amri "wauza mafuta" wanakaidi......

  There is a lot of dirty games on this I suspect!!!
   
 19. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Hizo bei zinashuka Dar peke yake mie kuna kituo kimoja cha Oryx bulyanhulu kila siku nanunua mafuta ya petrol kwa 2300 yashuke yapande bei haibadiliki hivi Ewura mko wapi au mkifika mnapozwa kitu kidogo kwani serikali iko Dar pekee
   
Loading...