EWURA yaomba wananchi kutoa maoni ya IPTL

Mmhh Muuogopeni Mungu nyinyi wtu 2022 wnatka kuongezewa leo wasubiri kwa uishe bac
 
Taarifa nilizonazo kutoka kwa mbunge Fulani mwenye mabasi yaendayo Dodoma na mwenye jimbo mojawapo la Dodoma amesema NGalamgosi amekuwa hata rushwa hapokei hivyo wakaamua kumzunguka kupitia viongozi wakubwa. Kwa hiyo Serikali ilikuwa inatafuta njia yakumundoa ila hawakuwa na chochote chakufanya. Bahati nzuri hili la EWURA kutanganza kutaka maoni ya Juu ya leseni ya IPTL kimewauzi serikali kwani kumbe serikali ilitaka hilijambo lisitangazwe ila bali EWURA itoe lesseni kimyakimya. Kwa ufupi ni hivi serikali inataka IPTL iendelee kuzalisha umeme sasa kitendo cha Ngalamgosi kutangaza watu watoe maoni maana yake mission ya serikali ingegoma. Kutokana na hilio basi IPTL watapewa leseni kimyakimya.
Nadhani umeandika ukiwa cho..oni, msg yako in harufu mbaya sana
 
Jamani, inamaana huo mkataba wa miaka 20 na IPTL ulisainiwa 2002?! Mimi nilidhani ni mwaka 1995 hivyo uliisha 2015 na sio 2022??! Which is which?, na je, huo mkataba unawalazimisha EWURA kuwapa leseni?
 
Inamaana serikali hii ya JPM inania mbovu kiasi hiki na wananchi wake?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Maswali Mkuu kuhusu sakata hili ni mengi, lakini kama ujuavyo nchi yetu pendwa na Siri kali.

Jamani, inamaana huo mkataba wa miaka 20 na IPTL ulisainiwa 2002?! Mimi nilidhani ni mwaka 1995 hivyo uliisha 2015 na sio 2022??! Which is which?, na je, huo mkataba unawalazimisha EWURA kuwapa leseni?
 
Wakuu Mag3 na Nguruvi3 nafasi ikiruhusu pitieni mtaa huu.
Mkuu hili jambo linashangaza
Wakati wanatia saini mikataba ya awali wananchi hawakushirikishwa. Jitihada za kupitia Bunge zilizimwa
Leo wanataka wananchi watoe maoni. Hili lina utata sana, nani anahakiki maoni hayo ya wananchi?

Kesho watakuja na hoja asilimia 99 wamesema mkataba uongezwe kwasababu wao ndio wenye takwimu
Hilo litajenga uhalali wa IPTL kuendelea na 'kazi'

Kwanini mkataba au hoja hizo zisipelekwe Bungeni na kupitia wabunge kuwe na mjadala wa wazi?
Hili litasiadia mbele ya safari kwasababu hoja zote zitakuwa mubashara, tutajua nani amesema nini na kwanini

Nadhani kuna mchezo unataka kuchezwa, suala la kushirikisha wananchi kwa siri sidhani kama lina nia njema
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Ewura, Edwin Kidifu amesema mchakato unaofanyika sasa ni wa kisheria na maoni ya wadau ndiyo yataamua IPTL ipewe leseni au laa! Kidifu anasema IPTL imeomba kuongezewa muda wa leseni yake kwa sababu mkataba wake wa miaka 20 na Serikali wa utekelezaji wa mradi wa umeme unakwisha mwaka 2022.

Wana JF,

Tafadhali, rejea maelezo ya kaimu mkurugenzi wa huduma za sheria wa EWURA hapo juu.
Napata matatizo ya kuelewa inakuwaje mkataba unaoisha 2022 unaombewa kuongezewa leo hii 2017? Haingii akilini miaka mitano kabla ya muda kuisha IPTL inaomba kuongeza muda. Swali jingine la kujiuliza ni muda unaoombwa. Je ni muda wa kiasi gani unaoombwa? Kimsingi mikataba ya namna hii yenye utata ni vyema yote isitishwe mpaka irekebishwe na mamlaka husika. Kuendelea kuiongezea muda mikataba ya aina hii ni kuendelea kuwaumiza watanzania bila sababu ya msingi.
 
Mkuu mikataba wa hawa matapeli na TANESCO unaendelea hadi 2022 lakini leseni yao ya kufanya biashara nchini ndiyo inamaliza muda wake July 2017.
Kisheria kama hawana learning nyingine ya kuwaongezea muda wa kufanya biashara nchini hawastahili kujihusisha na hiyo biashara yao ya ufuaji wa umeme.

Wana JF,

Tafadhali, rejea maelezo ya kaimu mkurugenzi wa huduma za sheria wa EWURA hapo juu.
Napata matatizo ya kuelewa inakuwaje mkataba unaoisha 2022 unaombewa kuongezewa leo hii 2017? Haingii akilini miaka mitano kabla ya muda kuisha IPTL inaomba kuongeza muda. Swali jingine la kujiuliza ni muda unaoombwa. Je ni muda wa kiasi gani unaoombwa? Kimsingi mikataba ya namna hii yenye utata ni vyema yote isitishwe mpaka irekebishwe na mamlaka husika. Kuendelea kuiongezea muda mikataba ya aina hii ni kuendelea kuwaumiza watanzania bila sababu ya msingi.
 
Naunga mkono hoja Mkuu. Hili la kudai wanakusanya maoni ya Watanzania kwa siri ilikuwa ni changa la macho ili wafanye tena uhuni wao kwamba Watanzania kwa asilimia kubwa wametaka IPTL waongezewe muda wa leseni yao hadi 2022.

Mkuu hili jambo linashangaza
Wakati wanatia saini mikataba ya awali wananchi hawakushirikishwa. Jitihada za kupitia Bunge zilizimwa
Leo wanataka wananchi watoe maoni. Hili lina utata sana, nani anahakiki maoni hayo ya wananchi?

Kesho watakuja na hoja asilimia 99 wamesema mkataba uongezwe kwasababu wao ndio wenye takwimu
Hilo litajenga uhalali wa IPTL kuendelea na 'kazi'

Kwanini mkataba au hoja hizo zisipelekwe Bungeni na kupitia wabunge kuwe na mjadala wa wazi?
Hili litasiadia mbele ya safari kwasababu hoja zote zitakuwa mubashara, tutajua nani amesema nini na kwanini

Nadhani kuna mchezo unataka kuchezwa, suala la kushirikisha wananchi kwa siri sidhani kama lina nia njema
 
Tangu lini EWURA na Mashirika mengine ya UMMA yakaomba maoni/ushauri kutoka kwa wananchi, huu kama si usanii ni kitu gani - kusimamishwa Mkurugenzi Mkuu ndiyo mnakumbuka kwamba kumbe Tanzania inaweza kuwa na Wananchi wenye ushauri/maoni ambayo yanaweza kuwa msaada mkubwa kwenu!! Taifa letu tulivyo wa ajabu wakati mwingine, a very responsible person Serikalini anakuja na hoja kwamba linapo kuja saula la mikataba baina ya wawekezaji na Serikali/Shirika la UMMA ni SIRI, I hope uongozi wa awamu ya tano awawezi ku-entertain upuuzi huu - Taifa linapigika kijinga kutokana na Watanzania wenzetu kukosa UZALENDO wa kweli, wanao fanya mambo haya wanajulikana lakini hawachukuliwi hatua yoyote wanaendelea na matanuzi bila woga wana mali zakushangaza they're totally untouchable. Binafsi napendekeza baada ya kumaliza zoezi la waajiriwa hewa na vyeti feiki basi Serikali ijikite kuwachunguza watu hawa i.e uchunguzi unao endelea kwa waajiriwa wa TMAA umulike mashirika ya Hifadhi za jamii, TRA, Tanesco, EWURA, TBS, Sugar Board of Tanzania, Bandari na TDFA.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu kama sikosei hili tangazo la kuwataka Watanzania watoee maoni yao lilitangazwa kabla ya huyo DG kutumbuliwa.

Tangu lini EWURA na Mashirika mengine ya UMMA yakaomba maoni/ushauri kutoka kwa wananchi, huu kama si usanii ni kitu gani - kusimamishwa Mkurugenzi Mkuu ndiyo mnakumbuka kwamba kumbe Tanzania inaweza kuwa na Wananchi wenye ushauri/maoni ambayo yanaweza kuwa msaada mkubwa kwenu?
 
Boss BAK Maoni ya Wananchi au yangu ni:

1. Kwanza waturudishie pesa yetu waliyotuibia, ilifikia baadhi yao kutudharau kwa kuita ni Pesa ya Mboga, wengine walisema ni waliamua tu kusaidia. Na wengine walibeba kwenye Lumbesa na Malboro.

2. Wasiongezewe muda.

3. Wafungashe Virago warudi kwao.

4. Tanesco apate mshindani.

My Take: Huyu Mdudu IPTL ni Kansa.

Friday, June 9, 2017
Ewura yaomba wananchi kutoa maoni ya IPTL

EWURAAAAAA.jpg

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo

Kwa ufupi
Akitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo leo Ijumaa jijini hapa, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo amesema kuna baadhi ya watu wanapotosha umma kwamba tayari IPTL wameshapewa leseni ya kuiuzia umeme Tanesco.

By Peter Elias, Mwananchi pelias@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kujitokeza kutoa maoni kuhusu dhamira ya Kampuni ya kufua umeme ya IPTL kuomba kuongezewa muda wa leseni yake ya kuiuzia Tanesco umeme.

Akitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo leo Ijumaa jijini hapa, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo amesema kuna baadhi ya watu wanapotosha umma kwamba tayari IPTL wameshapewa leseni ya kuiuzia umeme Tanesco.

"Ewura tunapokea maoni ya wananchi kwa maandishi, kwa hiyo itakuwa ni jambo la kizalendo kwa wananchi kujitokeza na kutoa maoni ama kupinga IPTL au kuunga mkono ili itusaidie nasi kufanya uamuzi," amesema.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Ewura, Edwin Kidifu amesema mchakato unaofanyika sasa ni wa kisheria na maoni ya wadau ndiyo yataamua IPTL ipewe leseni au laa!

Kidifu anasema IPTL imeomba kuongezewa muda wa leseni yake kwa sababu mkataba wake wa miaka 20 na Serikali wa utekelezaji wa mradi wa umeme unakwisha mwaka 2022.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu kama sikosei hili tangazo la kuwataka Watanzania watoee maoni yao lilitangazwa kabla ya huyo DG kutumbuliwa.

Mkuu hawa watu walisha jua in advance what was coming - usidanganyike na time lag ya jamaa huyu kutoa tamko na time ya kusimamishwa kwa Mkurugenzi Mkuu, Watanzania wajanja sana!! We jaribu kufatilia kwa karibu matukio fulani fulani, mfano akitimuliwa kazi unceremonously Mkurugenzi/Mkuuu wa Mkoa au Wilaya kutokana na uzembe basi kesho yake utasikia walio salimika wanatoa maagizo kwa kutumia Media kwamba na mimi ntakuwa mkali sitakubali watu washindwe kuwajibika vilivyo, mtu unabaki unashangaa kwani mwenzao hasingewajibishwa ,je, wao wangeweza kweli kutaka wasikike kwenye vyombo vya habari - sisemi ni wote lakini kuna baadhi yao wanatumia mbinu hizo kulinda ajira, wanao jiamini wala hawaangahiki na publicity STUNTS.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tangu lini EWURA na Mashirika mengine ya UMMA yakaomba maoni/ushauri kutoka kwa wananchi, huu kama si usanii ni kitu gani - kusimamishwa Mkurugenzi Mkuu ndiyo mnakumbuka kwamba kumbe Tanzania inaweza kuwa na Wananchi wenye ushauri/maoni ambayo yanaweza kuwa msaada mkubwa kwenu!! Taifa letu tulivyo wa ajabu wakati mwingine, a very responsible person Serikalini anakuja na hoja kwamba linapo kuja saula la mikataba baina ya wawekezaji na Serikali/Shirika la UMMA ni SIRI, I hope uongozi wa awamu ya tano awawezi ku-entertain upuuzi huu - Taifa linapigika kijinga kutokana na Watanzania wenzetu kukosa UZALENDO wa kweli, wanao fanya mambo haya wanajulikana lakini hawachukuliwi hatua yoyote wanaendelea na matanuzi bila woga wana mali zakushangaza they're totally untouchable. Binafsi napendekeza baada ya kumaliza zoezi la waajiriwa hewa na vyeti feiki basi Serikali ijikite kuwachunguza watu hawa i.e uchunguzi unao endelea kwa waajiriwa wa TMAA umulike mashirika ya Hifadhi za jamii, TRA, Tanesco, EWURA, TBS, Sugar Board of Tanzania, Bandari na TDFA.
Hapa kuna jambo, lini hawa wasiotaka mikataba ionekane wawe weeema kiasi cha kutaka maoni

Hoja yao ni kutaka kujenga 'uhalali' kwa kutumia maoni ya wananchi ambayo wao ndio wanaendesha na kuratibu zoezi
Nani miongoni mwetu anaweza kusema wananchi walishauri kadhaa ikiwa hatujui

Mkuu sidhani EWURA Wwametoka wenyewe, nadhani kuna maelekezo mahususi katika hili
 
Back
Top Bottom