Ewura yafafanua bei ya mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ewura yafafanua bei ya mafuta

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Dec 28, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Ewura yafafanua bei ya mafuta Monday, 27 December 2010 19:57

  Hidaya Omary
  MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei mpya elekezi ya mafuta inayoonyesha kuwa imepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na bei elekezi ya toleo lililopita.

  Taarifa iliyotolewa jana na mamlaka hiyo imeeleza kuwa kushuka kwa bei ya mafuta, kumetokana na kushuka kwa bei ya nishati hiyo katika soko la dunia na kupanda kidogo kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.

  "Bei za aina zote tatu za mafuta za jumla na rejareja hapa nchini zimeshuka ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 8 mwaka 2010," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

  Taarifa ilieleza "Katika toleo hili bei za rejareja zimeshuka kama ifuatavyo: petroli 0.56%, dizeli (5000 ppm) 2.44%, dizeli (500 ppm) 2.21% na mafuta ya taa 3.19%."

  "Mabadiliko haya ya bei za mafuta hapa nchini yametokana na kushuka kwa bei katika soko la dunia na kupanda kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya Marekani, (sarafu ambayo hutumika katika manunuzi ya bidhaa za mafuta kwenye soko la dunia)," imesema taarifa hiyo.

  Taarifa ilifafanua "Bei za jumla kulinganisha matoleo haya mawili zimepanda kama ifuatavyo: Petroli 0.58%, dizeli (5000ppm) 2.53%, dizeli (500 ppm) 2.29% na mafuta ya Taa 3.36%.

  Hata hivyo taarifa hiyo ilisema kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ili mradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo ambayo ni asilimia asilimia 7.5 ya bei elekezi.


  Katika hatua nyingine adhabu zinazotolewa na Ewura kwa wafanyabiashara wanaozidisha bei ya mafuta, zimefanya wengi kuuza mafuta hayo kwa bei elekezi.

  MKuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa Ewura Titus Kaguo, alisema jana kuwa bei halali ya petroli jijini Dar es Salaam Sh 1,666 na kikomo ni 1,791 na bei ya Disel yenye kiwango kikubwa cha salfa ni 1,647 na kikomo ni 1,770 huku bei kikomo kwa diesel yenye salfa chache ni 1,686 na kikomo ni 1813.

  “Pale awali wafanyabiashara walikuwa wakikiuka masharti, lakini baada ya kuona adhabu ni kali kwani wengine waliishia kulipa hadi Sh milioni 80 wameacha kabisa na hakuna kitu kinachoitwa kuongeza bei zaidi ya maelekezo ya mamlaka,” alisema Kaguo.

  Pia alisema pamoja na kuonekana bei zinapanda, kuwepo kwa Ewura kunampa faida mtumiaji kwa asilimia 30 chini zaidi ikilinganishwa kama Ewura isingekuwepo bei zingekuwa za juu zaidi.

  Akizungumzia kupanda kwa bei, alisema hali hiyo inatokana na mabadiliko katika soko la dunia kama itatokea siku bei zikashuka basi, Ewura nayo itashusha kama ilivyofanya mwaka 2009, iliposhusha kutoka 1800 kwa Dar es Salaam hadi 1,100 kwa lita ya mafuta ya petroli na kutengeneza historia ya kushuka kwa bei kwa bei za hapa nchini kwani bidhaa ikipanda haijawahi kushuka,
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Hizi bei badi ni juu sana na kamwe nchi hii haitaweza kusonga mbele na mzigo huu wa gharama ya nishati hii..something must give in...................kwa hiyo EWURA waache kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa......................waangalie Kenya mbona bei kule zimeshuka maradufu?

  Tofauti iko wapi?
   
Loading...