Ewura, hivi gesi ya kupikia haina bei elekezi?

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,676
6,933
Nauliza hili kwenu mamlaka ya Ewura mnisaidie kwasababu huku Mtongani na kuelekea Ununio bei ya gesi ya mihan mtungi wa kati ni shilingi elfu hamsini sawa na bei ya oryx!

Maeneo ya Mkwajuni Kinondoni mtungi wa gas ya mihan ule wa kati unauzwa shilingi elfu arobaini na tano tu. Inakuwaje huku Mtongani tena mkoa huu huu bei iwe juu hivyo?

Ewura tupieni jicho pande hizi kwani tunaumizwa pasi na sababu. Ikibidi makampuni yanauza gas hizi yafungue maduka yao huku badala ya hawa mliowaachia wanawaharibia biashara.
 
  • Thanks
Reactions: 454
Kitu kinapanda bei kulingana na demand(uhitajio mkubwa) hujiulizi Kwanini bei ya Soda Bar na mtaani ni tofauti?
 
Kitu kinapanda bei kulingana na demand(uhitajio mkubwa) hujiulizi Kwanini bei ya Soda Bar na mtaani ni tofauti?
Elewa somo basi. Ewura ni regulator wa mafuta na gas na kwa eneo la mkoa mmoja hakuwezi kuwa na bei mbili tofauti za lita ya mafuta. Huko kwenye soda hakunihusu kwani mie situmii. Au ewura wapo pande za soda siku hizi?
 
Back
Top Bottom