Ewe mwanachuo jipange

Ewe mwanachuo jipange

Mawazo mazuri sana,, hongera kwa hilo. Ingawa haya ni kama maneno ya kiongozi wa dini kuwaasa waumini waache maovu ilihali waliopo ndani ya nyumba hiyo ya dini ni wale waliozunguukwa na wigo wa maadili........
Namaanisha kuwa wahusika unaowashari wengi hawako huku! Wapo fb na insta.
Ni kweli usemayo,yatamsaidia aliyepo humu kama ataona inafaa kufungua uzi huu.
 
Mimi sina demu lakini BOOM huwa halikai yaan, hata sielewagi kwa kweli...
Hata mimi nilikua kama wewe ila nikakaa chini nikadadavua mambo nikagundua mimi ndo tatizo. Tatizo langu nililigundua ni kushindwa kuweka bajeti yangu katika usawa na uhalisia, toka nikiwa mwaka wa kwanza nilikua na bajeti nzuri sana mfano:
Total income: 2M
total expenditure: 1.1M
saving: 800k
Income after expenses: 100k

NB: bajeti nzuri kulingana na maisha yalivyo kwangu binafsi

Kusema ukweli sikuiweka katika uhalisia bajeti yangu ya mwaka mzima wa masomo nilipoteza vingi japo sijilaumu maana sijapotea (naungana na mtoa mada). Naingia mwaka wa mwisho nikiwa na hali mpya, nguvu mpya na kasi ya ajabu kuelekea uhalisia wa bajeti yangu na nimepata njia mbadala kuweza kutatua tatizo langu la kutumia “saving". Njia mbili ninazo;

1. Kuwekeza kila pesa ninayotunza moja kwa moja kila baada ya kupokea fedha ya kujikimu. A.K.A boom
NB: hapa itakua savings ya awamu mbili ya fedha ya kujikimu.

2. Kufungua akaunti nyingine ili niweke pesa za “savings" ili nikimaliza chuo niwekeze mazima.

Kutoka moyoni nakuunga mkono kama sio hoja mtoa mada ni wakati wetu sisi tuliovyuoni kujiandaa kimwili na kiakili kupambana na mazingira na uhalisia.

" We must have a backbone not a wishbone"
 
Asante sana aiseee,umenipa kitu fulani hapa.
 
Waambie mkuu maisha huku sivyo kama wazaniavyo usipokua makini utamaliza chuo na pc tu ambayo itabidi uiuze pindi ukimliza chuo ili upate hela ya kuzungukia maofisi mbalimbali kutafuta ajira

Hahahaha mkuu umenikumbusha mbali, mi hapa nilimalza nikajikuta nina flash tu miaka hyo hata pc sina hahaha
 
Wazungu walituletea msemo 'if you fail to plan,you plan to fail' mwenzenu nilishindwa kuplan, japo ninajipa tumaini kuwa it is never too late,nina tumaini nitarekebisha kwa namna moja au nyingine.

Mimi ni mwanachuo,na mambo yakienda vema basi mwakani nitakuwa nahitimisha,japo nina hofu na nitapambana vipi na hali ya huko niendako sababu ni kama nimechelewa kujipanga.

Mambo yamebadilika,upepo hausomeki huko baada ya chuo,ajira hamna kama zamani,pesa hazikamatiki.Ila nina amini kabisa una uwezo wa kujipanga kabsa kukabiliana na ugumu uliopo mbele kama tu utajipanga mapema.

Wanafunzi wengi wa chuo, 'BOOM HALIKAMATI BOOM' Hili ni kosa kubwa ambalo nimelifanya,boom la miezi miwili nilitumia kwa mda wa mwezi mmoja au mmoja na nusu. Serikali inatoa 8500 kwa siku,inamaanisha kuna siku nilitumia zaidi ya 8500. Japo kuna wengine waliitumia hii pesa kuongezea kwenye ada nawapa hongera kwa hilo.

1. Kama hauna ma kando kando 8500 ni pesa nyingi sana kwa siku kwa mtu mmoja.Tumia kidogo kadri uwezavyo,inayobaki itunze. Weka hata 2000 kwa siku kwenye kibubu chako,hii pesa utaitumia kama mtaji wa kuwekeza uwapo chuoni au baada ya chuo. Ajira hazieleweki.

2. Epuka kuiga uwapo chuoni. Sometime niliiga,nile kama fulani,nivae kama fulani ninywe kama fulani. Hii imenifanya nitumie pesa hovyo ndugu zangu. Nakushauri kuwa kama mjinga,kuwa kawaida tu,kuwa wewe,ni sumu kuiga.

3. Sikuwa mtu wa mademu,ila niliona wenzangu,mademu 3 mpaka 5 ni kawaida. Huyu kamtoa out kule,huyu kampeleka huku,huyu kamlisha kile n.k yote kudhihirisha yeye ni kidume. Hii ilikuwa sana pale boom linapotoka. Epuka hii,kuwa mwangalifu kwenye matumizi uwapo kwenye mahusiano. Pesa nyingi washikaji waliitumia hapa.

4. Hakuna mtu kwenye historia aliwahi kuikamata fashion. Kila siku kuna fashion mpya iwe mavazi,technologia n.k Nilipenda kuwa na smartphone kali,ikitoka iphone 6 nilitaka kuwa nayo,sijui nguo gan nilipenda kuwa nayo. Achana na hii mambo,kila kitu kina mda wake. Nilitumia pesa kwa ajili ya kujiweka wa kiwakati zaidi.

5. Jaribu kufikiria ni kitu gani unaweza fanya,ukawa comfortable kufanya ukiachana na profession unayoisomea,hii itakusaidia na itakupa urahisi wa kuwekeza pale unaposubiria ajira au zisipotoka kabisa. Hata mimi mpaka sasa nipo nachanganua nitafanya nini nimalizapo chuo maana waliopo huko bila ajira ni wengi, nawaza mimi itakuwaje.?

6. Kuwa mwepesi wa kuchagua marafiki,chagua wale wanaoendana na ndoto zako,watakaokusindikiza katika kuitafuta kesho yako.

Utakayo save uwapo chuoni mpaka unamaliza chuo inaweza isiwe kubwa sana lakini tukumbuke hata milioni ilianza na shilingi moja. Kidogo hicho hicho kinaweza kuwa msaada huko uendako. Hata biashara kubwa zilianza kwa kuwa ndogo hapo mwanzo.

Nimejaribu kushare experience yangu chuoni,i hope nitarejea kwenye mstari maana naelekea kumaliza na sikujipanga toka mwanzo.

Shukrani.
Kuna wenzako hata huo mkopo hawana.
 
Kazi iliyo baki mtahani ni moja tu .kubet kwahiyo waambie wajipange maana uku kanji ana masiala kabisa ata mia tano anachukua ukiingia kwenye mabanda ya kupetia usishangae unakutana na dada yako pamoja na mjomba
 
Back
Top Bottom