Ewe Mdudu Smartphone kwa nini Hivi.?

Ewe Mdudu Smartphone kwa nini Hivi.?

Mwananchi wa chini

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
227
Reaction score
599
Hivi ndivyo ambavyo mdudu simu na technolojia imetukamata na hatuwezikuona chochote chamaana, sio marafiki sio watoto sio mke au mume sio muda wako mwenyewe. Masaa yote, dakika zote na sekunde zotw ni simu mkononi. Tukomboke
 

Attachments

  • tec.jpg
    tec.jpg
    42.7 KB · Views: 39
Teknolojia imekuwa na faida na hasara zake pia. Simu zimehusika sana katika kuvunjika Ndoa. Kufumaniwa kwingi chanzo chake ni simu. Wazee wetu hawakuwa na simu wakawa wanadumu sana kwenye mahusiano yao. Hivyo ni vizuri hizi simu tuzitumie kwa akili, maana mambo yetu mengi ya sirini yamekuwa wazi kupitia hizi simu.
 
ukweli ni kwamba sie tuliozaliwa miaka ya 80 na 90, na 2000 ndio wa kwanza kuishi ulimwengu huu wa masmartphone hapa duniani, tukionacho ni ulimbukeni tu ila utaisha, tukiwa watu wazima wa makamu na majukumu yakitujaa na kuchoshwa na simu na kuona kuwa ni utoto tutapuuzia na tutaishi kawaida, subirini waliozaliwa miaka ya 2010 na 2020 wakianza kuwa wakaka na wadada na kujipostiposti sisi tutakaa pembeni kuwakosoa kwasababu tutakuwa tayari tumevuka hilo rika
 
Mkuu ya kwangu inanayo itumia mara nyingi si tumii ya bando huwa freebasics ili muda wote niwe active hata swala LA charge yangu inakaa kiukweli japo ya kawaida
Yaani tupo wote katika hili ..simu yangu ikikosa bundle ama charge huwaga nina kuwa kichaa kwa muda mfupi "..
 
Hizi ndoa kuwa ngumu na watu kuziogopa yote ni matokeo ya simu. Zaman nani alikuwa anajua matatizo ya ndoa?! Kila mtu alikuwa nayo moyoni tu. Cyo asa hivi
 
Hizi ndoa kuwa ngumu na watu kuziogopa yote ni matokeo ya simu. Zaman nani alikuwa anajua matatizo ya ndoa?! Kila mtu alikuwa nayo moyoni tu. Cyo asa hivi
Hivi madam ile tabia yako ya kuangalia porn kwenye simu ulishaacha?[emoji4][emoji4][emoji4]
 
Yaani siku hizi hata ukipanda daladala hata wazee hawaongei tena wako busy na simu zao za tochi.
 
Back
Top Bottom