GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 57,157
- 110,635
- Mcha mungu sana ( narudia tena ) mcha mungu mno uwe mkristo au muislam kwangu haina tatizo
- Unayejitambua
- Usiwe mzuri sana wala mbaya sana
- Elimu kuanzia diploma, degree, masters na phd na umri wake uwe wa kuanzia miaka 27 hadi 36 tu tafadhali
- Mvumilivu wa kimaisha hata kama utanikuta mimi sina uwezo
- Uwe tayari kunisaidia kimawazo na kifikra ili tuweze kufika mbali kimaisha
- Hakikisha kuwa wewe siyo tasa na hujawahi hata mara moja kutoa mimba
- Utakaye nipenda siyo mimi tu bali wazazi, ndugu na marafiki zangu
- Uwe ni mtu wa kujichanganya na kupenda watu
- Usiwe na dharau, majivuno au sifa bila kusahau usiwe ni mtu wa kunipa stress kwani utanichanganya
- Uwe unajua kufanya mapenzi ya kiuhakika na kama hujui basi uwe tayari kufundishwa na ufundishike kweli
- Utakayeweza kunitoa hapa nilipo kimaisha na kifikra na kunifanya nikaribie mafanikio ya akina dangote
- Uwe ni mpenda michezo japo kama hupendi napo siyo tatizo kwani najua nitakushawishi tu na utapenda
- Utakayeweza kunifanya nijione mfalme mbele ya wanaume wenzangu kwa jinsi utakavyonipenda
- Ambaye utaniheshimu na siyo kuniogopa kwakuwa mimi ni mwanaume ( namaanisha uwe very confident )
Ewe mdada au mwanamke humu jf ambaye unataka kweli kuwa na mwenza wako ili mfanye maisha na ufikie malengo nae kimaisha nakukaribisha na kama hutojali tunaweza tukawasiliana kwa pm au ukanitumia tu namba yako ya simu na nitajitutumua kukutafuta ili tuzungumze zaidi na nitafurahi siku moja nikija kutoa shukran zangu za dhati kwa waanzilishi wa jf na members wote humu kwa kuniwezesha kuwa na mwenza wangu.
Wasifu wangu japo kiufupi;
Mimi ni kijana wa kawaida tu mtanzania kabila la mjita kutoka mkoani mara, umri wangu ni miaka 36 nimejiajiri tu mwenyewe kwa vishughuli vyangu vya hapa na pale ( huku nikiwa siyo manji, dewji, dangote wala bill gates ) na nina elimu ya wastani ya shahada ya kwanza japo mwenyezi mungu akijaalia mwaka huu huu mwezi november nategemea kuhitimu rasmi na shahada yangu ya uzamili na ninaishi hapa hapa dar es salaam wilaya ya kinondoni jimbo la kawe ( nimepanga tu na sijajenga ).
Angalizo;
Naomba jambo hili lichukuliwe kwa umakini na umuhimu mkubwa sana kwani sijaweka hapa huu uzi labda nipoteze muda bali kiukweli sasa umefikia muda wa mimi kuwa na mwenza wangu wa kimaisha hivyo nisingependa kuwepo na mzaha au sanifu ktk hili suala. na ni imani yangu jf itanipatia mke wangu mtarajiwa kutokea humu humu.
Mungu awabariki nyote na awapeni maisha mema na mazuri