Ewe dada na mwanamke humu JF, Je! Una sifa kuu hizi zifuatazo uwe mwenza wangu wa kimaisha?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,127
  1. Mcha mungu sana ( narudia tena ) mcha mungu mno uwe mkristo au muislam kwangu haina tatizo
  2. Unayejitambua
  3. Usiwe mzuri sana wala mbaya sana
  4. Elimu kuanzia diploma, degree, masters na phd na umri wake uwe wa kuanzia miaka 27 hadi 36 tu tafadhali
  5. Mvumilivu wa kimaisha hata kama utanikuta mimi sina uwezo
  6. Uwe tayari kunisaidia kimawazo na kifikra ili tuweze kufika mbali kimaisha
  7. Hakikisha kuwa wewe siyo tasa na hujawahi hata mara moja kutoa mimba
  8. Utakaye nipenda siyo mimi tu bali wazazi, ndugu na marafiki zangu
  9. Uwe ni mtu wa kujichanganya na kupenda watu
  10. Usiwe na dharau, majivuno au sifa bila kusahau usiwe ni mtu wa kunipa stress kwani utanichanganya
  11. Uwe unajua kufanya mapenzi ya kiuhakika na kama hujui basi uwe tayari kufundishwa na ufundishike kweli
  12. Utakayeweza kunitoa hapa nilipo kimaisha na kifikra na kunifanya nikaribie mafanikio ya akina dangote
  13. Uwe ni mpenda michezo japo kama hupendi napo siyo tatizo kwani najua nitakushawishi tu na utapenda
  14. Utakayeweza kunifanya nijione mfalme mbele ya wanaume wenzangu kwa jinsi utakavyonipenda
  15. Ambaye utaniheshimu na siyo kuniogopa kwakuwa mimi ni mwanaume ( namaanisha uwe very confident )

Ewe mdada au mwanamke humu jf ambaye unataka kweli kuwa na mwenza wako ili mfanye maisha na ufikie malengo nae kimaisha nakukaribisha na kama hutojali tunaweza tukawasiliana kwa pm au ukanitumia tu namba yako ya simu na nitajitutumua kukutafuta ili tuzungumze zaidi na nitafurahi siku moja nikija kutoa shukran zangu za dhati kwa waanzilishi wa jf na members wote humu kwa kuniwezesha kuwa na mwenza wangu.


Wasifu wangu japo kiufupi;

Mimi ni kijana wa kawaida tu mtanzania kabila la mjita kutoka mkoani mara, umri wangu ni miaka 36 nimejiajiri tu mwenyewe kwa vishughuli vyangu vya hapa na pale ( huku nikiwa siyo manji, dewji, dangote wala bill gates ) na nina elimu ya wastani ya shahada ya kwanza japo mwenyezi mungu akijaalia mwaka huu huu mwezi november nategemea kuhitimu rasmi na shahada yangu ya uzamili na ninaishi hapa hapa dar es salaam wilaya ya kinondoni jimbo la kawe ( nimepanga tu na sijajenga ).

Angalizo;

Naomba jambo hili lichukuliwe kwa umakini na umuhimu mkubwa sana kwani sijaweka hapa huu uzi labda nipoteze muda bali kiukweli sasa umefikia muda wa mimi kuwa na mwenza wangu wa kimaisha hivyo nisingependa kuwepo na mzaha au sanifu ktk hili suala. na ni imani yangu jf itanipatia mke wangu mtarajiwa kutokea humu humu.

Mungu awabariki nyote na awapeni maisha mema na mazuri
 
Mkuu kwa uelewa wangu mdogo kuhusu hawa dada zetu na kwa umri unaoutaka number 10 Inapata upinzani wa kishindo kwenye number 7.
nasikitika kuona ndugu yangu unajaribu kumtafuta malaika kuzimu..goodluck
 
Bora usingetaja kabila, ila avatar yako inatoa elimu picha.... All the best bro, siweki kuweka utani maana umetoa tahadhari na kwa kuzingatia historia......nasign off.
 
Ndo mana cku hizi ndoa hazidumu,upendo umekuwa no 8 eti ktk sifa zinazohitajka hii haitakuwa ndoa ni mkataba wa maisha,we mwenyewe mbinafsi kama sio tasa,na hajatoa mimba atakuwa single mama
 
Duh hali siku hizi imekuwa hivi kama maombi ya kazi vile

Kama siyo hairuhusu watu wangeoana wao kwa wao kama ilivyo serekalin kama huna ndugu hupati kazi! huyu mleta uzi lazma angemuoa ndugu yake
 
Ndugu yangu kwa kwa dhati kabisa nikushauri kwamba kama Mwenyezi Mungu amekuumbia mwenzi wako wa maisha usali na kumwomba akuoneshe yeye mwenyewe kwa njia yake atakayoipenda.Hii mitandao ni mizuri kwa mambo mengi lakini sikushari utumie mtandao kumtafuta binadamu mwenzio aliyeumbwa kwa ajili yako.

Pia nikuulize hivi wewe binafsi unachangia vipi kuhakikisha kuwa mabinti/kinadada kuwa na sifa hizo unazozitaka wewe?
Kama wewe mwenyewe upo miongoni mwa watu wanaochangia kuwaribu kinadada tokea wakiwa bado wadogo wasiwe na
sifa nzuri za kuwa wake wema wa baadae usitegemea kumpata mdada mwenye sifa nyingi unazotaka.
Pia unataka awe mcha Mungu wa dini yoyoye hatakama haifanani na yako.Unajua kuwa amani ya familia kwa asilimia kubwa inachangiwa na watu wa imani moja?Mkishatofautiana imani ni mwanzo wa vurugu ktk familia.Hivyo jali kipengele cha imani na umtafute mwenza wa imani yako.
 
Angalia tena wewe mwenyewe kuanzia namba 1 hadi 15, na uondoe sifa zote ambazo hazitakiwi kuwepo hapo, lasivyo muumbe wa kwako wewe mwenyewe, pia kama unamaanisha basi tambua kwa mtindo huo mwenzi kwako itabaki kuwa ndoto. La mwisho ni hilo kabila ndugu yangu?? usiogope sana ila ndio hivyo tena!!!, umemwaga sifa weeeee zen mwisho unatutajia hilo kabila.

Kabila + Avatar + baadhi ya sifa hapo juu = 0, labda uende huko Musoma.

Nb: Punguza vigezo hivyo, mf; unaweza mpata mtu mkahakikisha wote vizazi vipo vizuri na bado mkakosa mtoto, mtoto ni zawadi, wapo watu hadi leo miaka 30 ndani ya ndoa no mtoto, vipimo vinaonesha wapo safi kabisa.

Zaidi ni wewe mwenyewe kaka kila lakheri.
 
Laaah Mkuu sijui nikupe bint mmoja. Lakini Nina uhakika gani kama baada ya mwaka atakuwa bado anaviungo vyake vyote kamili? Maana sikawii kupigiwa simu na majirani nikachukue binti yangu akiwa hana masikio, na viungo vingine na wewe umetorokea kusiko julikana bora usingetaja mkoa uliotoka
 
Ila umejitahidi kuandika vizuri na kujielezea anyway ngoja wadada waje ukamate angalau ht kichwa kimoja.
 
Laaah Mkuu sijui nikupe bint mmoja. Lakini Nina uhakika gani kama baada ya mwaka atakuwa bado anaviungo vyake vyote kamili? Maana sikawii kupigiwa simu na majirani nikachukue binti yangu akiwa hana masikio, na viungo vingine na wewe umetorokea kusiko julikana bora usingetaja mkoa uliotoka

sijazoea uwongo hivyo siwezi kuficha kabila langu au uhalisia wa maisha yangu na kama kweli yupo atakayenipenda basi hawezi kuogopa kabila au mkoa ninaotoka. ukweli wangu hapo ndiyo uhalisia wangu.
 
Bora usingetaja kabila, ila avatar yako inatoa elimu picha.... All the best bro, siweki kuweka utani maana umetoa tahadhari na kwa kuzingatia historia......nasign off.

mwenye upendo wa kweli hawezi kutumia avatar yangu na kabila langu kuwa ndiyo kigezo cha yeye kunikataa na kuniogopa. mwenye nia ya kweli nami naamini atajitokeza tu na bwana atatenda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom