Evarist Chahali: Kinana amenidhulumu shilingi milioni 12.5

Evarist Chahali: Kinana amenidhulumu shilingi milioni 12.5

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Jana nilipata ujumbe kutoka kwa mheshimiwa mmoja akinieleza masikitiko yake kuwa licha ya jitihada zake kubwa kunisaidia kupata malipo kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, yaliyotokana na ushiriki wangu kwenye kampeni za chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, suala hilo ilibidi liishe kienyeji yaani bila malipo hayo kufanyika.

Sijawahi kuficha kuwa licha ya sababu nyingine za ushairiki wangu kwenye kampeni za CCM, pia nilifanya kazi ya usadi kwa makubaliano ya malipo. Na si kwamba sikulipwa hata senti tano. Hapana. Muungwana mmoja alitimiza ahadi yake, na nikalipwa kila nilichostahili.

Kazi iliyostahili malipo kutoka kwa Kinana tuliifanya mie na mhusika flani yupo hapa Uingereza, na makubaliano yalikuwa shilingi milioni 12.5 kwa kila mmoja wetu. Kazi tuliyofanya ilipitia kwa dada Mwele Malecela kwa maelekezo ya Kinana mwenyewe.

Awali sikuamini kabisa kuwa mtu anayeonekana “mwema” kama Kinana, na ambaye “hana shida kifedha” angeweza kupuuzia kutupatia haki yetu. Lakini jitihada mbalimbali zangu binafsi, dada Mwele na huyo mhusika mwingine wa hapa, na pamoja na kuwashirikisha watu mbalimbali ikiwa pamoja na huyo mheshimiwa aliyenitumia ujumbe jana, Bwana Kinana “akachikichia” stahili yetu.

Dhuluma sio kitu kizuri. Na ninaamini ipo siku Bwana Kinana atatambua kuhusu hilo the hard way. Kuna uwezekanao mkubwa ameshasahau kuhusu alichotutenda, lakini waswahili husema “mla kunde husahau ila mtupa maganda hasahau.”

Na hili la Kinana “kuchikichia” stahili yetu ni maumivu ya awali kabla ya “kugeukwa” na mtu ambaye baadhi yetu tulitukanwa kila aina ya tusi tulipokuwa tunamnadi, mgombea wa CCM John Magufuli, ambaye sasa anatamani kuona baadhi yetu tukidhuriwa, kisa tunamkosoa.

Lakini yote tunamwachia Mungu. Duniani tunapita tu, na ipo siku tutawajibika kwa Mola kwa matendo yetu wakati wa uhai wetu.

Chanzo: : Kinana amenidhulumu shilingi milioni 12.5
 
Waingereza wana msemo unaosema, ‘’ There ain't no such thing as a free lunch’’

Hii ina maana kuwa usione watu wanatoka mpaka mapovu kwenye majukwaa ya siasa au mitandao ya jamii ukadhani wanafanya kazi hiyo kwa ujira wa uzalendo! Hakuna kitu kama hicho! Njaa haina uzalendo!

Hata hawa wanaomshambulia Rais Magufuli bila kuona hata mazuri aliyoyafanya/anayofanya usidhani wanafanya hivyo bila ujira na kuna wengine waliahidiwa ujira/kazi na CCM baadaye wakatelekezwa!

Andiko hili linatufikrisha kuwa kuna mengine mengi ambayo yaliahidiwa kwa baadhi ya watu lakini hayakutekelezwa!

Shilingi Milioni 12.5 sio pesa kidogo kwenye maisha ya ‘’kubeba box’’ kwenye nchi za watu! Ndio maana kwa sasa Chahali amegeuka na anawatupia CCM na serikali yake makombora mpaka ya matusi ya nguoni!

Wait a minute, Kwani Kinana ameondoka na cheo cha Katibu Mkuu wa CCM? Kwani mkataba ulikuwa wa Mzee Kinana as person au Mzee Kinana as CCM secretary-General?

Inashangaza sana mtu anayejinasibu anafanya kazi ya Usadi(consultation) lakini hajui hata maana au umuhimu wa binding contract!

Huyu ni ex-Tanzania Intelligence and Security Services! Gosh!
 
Huyu atakuwa yule mwana udaku shigongo, waiter asante umeongeza hii bucket nifurahie namna ambavyo wana ccm wanavyoisoma namba
IMG_0413.JPG

Mkisema bia serengeti lite, hapa samaki samaki bei ni ile ile bia 5000, kila nikiona lalamiko la ccm nnaongeza bucket ingine bado nipo
 
Hii inazirihisha kuwa mkuu hakupenda kinana aachie ngazi, sasa ni kichafuana kwa kwenda mbele.

Sasa kinana hela atatoa wapi kama jiwe amekataa kulipa watu, wasanii wenyewe mmewapiga pamoja kuwa mlinzuguka nao kwenye kampeni za mgombea wenu wa urais kipindi hicho.
 
Waingereza wana msemo unaosema, ‘’ There ain't no such thing as a free lunch’’

Hii ina maana kuwa usione watu wanatoka mpaka mapovu kwenye majukwaa ya siasa au mitandao ya jamii ukadhani wanafanya kazi hiyo kwa ujira wa uzalendo! Hakuna kitu kama hicho! Njaa haina uzalendo!

Hata hawa wanaomshambulia Rais Magufuli bila kuona hata mazuri aliyoyafanya/anayofanya usidhani wanafanya hivyo bila ujira na kuna wengine waliahidiwa ujira/kazi na CCM baadaye wakatelekezwa!

Andiko hili linatufikrisha kuwa kuna mengine mengi ambayo yaliahidiwa kwa baadhi ya watu lakini hayakutekelezwa!

Shilingi Milioni 12.5 sio pesa kidogo kwenye maisha ya ‘’kubeba box’’ kwenye nchi za watu!

Mzee Kinana timiza ahadi yako!
Ccm wote matapeli
 
Huyo Mwele Malecela namdharau sana, tokea Le Mutuz atoe tuhuma humu za Mwele kumtumia Mange dhidi ya Le Mutuz na nikathibitisha kuwa ni kweli yuko karibu na Mange.

Yule mzee Malecela ana tabu mno na mtoto kama huyu + Le Mutuz
 
Mkuu;
Naomba ufunguke zaidi kuhusu tuhuma alizotoa Le Mutuz!
 
Walilipwa kuwaletea watanzania matatizo.

Walijitoa akili kwa malipo kidogo,leo ndio wanajidai kufungua midomo yao baada ya kugundua walidanganywa.

Nawaangalia sana,watu wana bei zao,hata 2020 mtashangaa mno.
 
Back
Top Bottom