Evarist Chahali, hili limenitisha!

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,087
5,079
Katika gazeti la Raia Mwema la jana tarehe 13 mwandishi wa makala na mchambuzi wa siasa za ndani anayishi Uskochi amendika kuhusu tahadhari aliyopewa na vyombo vya Usalama vya huko aliko kuwa kuna tishio la maisha yake. Ameeleza ya kuwa ana uhakika tishio hilo limetokea nyumbani.

Simfahamu huyu bwana wala background ingawa kuna makala moja ambayo aliandika na between the lines nilihisi ni mtu wa Usalama wa Taifa.

JUMAMOSI Februari 2 mwaka huuitabaki katika kumbukumbu zangu kwa muda mrefu, pengine katika uhai wangu wote.

Majira ya saa 3 asubuhinilikurupushwa usingizini na kelele za mlango uliokuwa ukigongwa kwa nguvu. Wakati ninajiandaa kwenda kufungua mlango, nikasikia sauti yenye dharuraikisema, “bwana Chahali, polisi hapa, tafadhali fungua mlango.”

Nilichanganyikiwa kwani tangunifike nchi hii zaidi ya miaka 10 iliyopita sijawahi kufanya kosa lolote aukukwaruzana na vyombo vya dola/sheria.

Baada ya kufungua mlango,askari waliovalia kiraia walijitambulisha na kuonyesha vitambulisho vyao. Piawalinisihi kuwa nisiwe na hofu ya kudhani kwamba nimefanya kosa lolote.

Kwa kifupi, walinieleza kuwawamepewa ujumbe kutoka moja ya taasisi za intelijensia za hapa kuwa kuna tishiola uhakika dhidi ya maisha yangu. Hata hivyo, walieleza kuwa kwa vile waowalipewa tu ujumbe huo na kutakiwa kuuwasilisha kwangu, hawakuwa na maelezo yaziada. Walisisitiza kuwa nichukue tahadhari muhimu na kunipa maelekezo yamawasiliano ya dharura.

Kwa vile nilikurupushwausingizini, awali taarifa hiyo ilionekana kama ndoto iliyokuwa inaendelea hatabaada ya kutoka usingizini. Ilinichukua takriban saa tatu kuzinduka kutokakatika mshituko huo, na kutambua uzito wa taarifa niliyopewa na polisi hao.

Nikaamua kwenda kituo kimojacha polisi kupata ufafanuzi zaidi. Mara baada ya kujitambulisha, mazingira yanamna suala hilo lilivyokuwa likishughulikiwa kituoni hapo lilinipa picha kuwajambo hilo lina uzito. Kwa kifupi, baada ya kitambo nilipewa ufafanuzi ambao haukutofautiana na maelezo niliyopewa awali na polisi walionitembelea katikamakazi yangu.
Kikubwa ni kuwa taarifa hiyoilionyesha kuwa tishio hilo dhidi ya maisha yangu linatokea huko nyumbani.

Swali linaloendelea kunisumbua kichwa ni KWA NINI iwe hivyo.

Wakati si vigumu kwangu kuhisi wahusika wa mpango huo wa kijahili, napata shida kuelewa kwanini wahusika hao watumie fedha za walipakodi kuandaa operesheni ya kutaka kunidhuru ilhali ninaamini kwa asilimia 100 kuwa mimi si tishio kwa usalama wa Taifa letu.

Ndiyo, baadhi ya ninayoandika kwenye makala zangu na tweets zangu huko kwenye mtandao wa kijamii wa twitter yanaweza kuwachukiza baadhi ya watu, lakini kwa hakika kuchukizwa huko si sababu ya kutaka kunidhuru.

Hadi wakati ninaandika makala hii nimekuwa nikiishi kwa tahadhari kubwa. Faraja kubwa kwangu inatokana na sababu tatu za msingi.

Kwanza, kwa vile nilizaliwa na kukulia katika familia inayomtanguliza Mungu katika kila jambo, nina imani kubwa kuwa mamlaka pekeekuhusu uhai wangu (yaani kuwa hai au kufa) ni Mungu pekee. Hakuna mwanadamu anayeweza kupora jukumu hilo la Mungu na kufanikiwa kufupisha uhai wa yeyote.

Pili, nina imani kubwa na taasisi za usalama za hapa Uingereza. Kimsingi, wenzetu hawa wanathamini sana usalama na uhai wa binadamu pasi kujali mhusika ni mzaliwa wa hapa au ni ‘mgeni’ kama mimi. Ushauri na sapoti ninayoendelea kupata inanipa matumaini makubwa kuwa nipo kwenye ‘mikono salama.’

Lakini tatu ni ukweli kwamba takriban miaka mitano sasa nimekuwa nikiishi na uelewa kwamba kuna baadhi ya watu huko nyumbani wanaoniona kama kimelea cha maradhi hatari ambacho kikiachwa bila kudhibitiwa kitazua balaa.

Kwa sababu hiyo, tangu wakatihuo nimekuwa nikiishi kwa tahadhari japo si kubwa kama hii ninayolazimika kuichukua sasa. Lakini ili uweze kuchukua tahadhari ni lazima uwe na mbinu naujuzi wa kuchukua tahadhari husika. Kwa bahati nzuri, watu hao wanafahamu fika kuwa nina ujuzi wa kutosha na kuelewa na kumudu fika mbinu za kuishi kwatahadhari.

Hata hivyo, kumudu mbinu nisuala moja na kuishi kwa kutumia mbinu hizo ni kitu kingine. Si jambo lakupendeza hata kidogo kuishi ukiwa na uelewa kuwa siku moja, mahala fulani unaweza kukumbana na madhara fulani. Lakini kadri unavyolazimika kuishi kwanamna hiyo inakuwa kama sehemu muhimu ya maisha yako, na ndivyo ilivyo kwangu.

Pamoja na kuchukulia kwauzito taarifa hizo za tishio dhidi ya uhai wangu, nimechukua hatua nyinginekadhaa ikiwa ni pamoja na kuwafahamisha watu ninaohisi kuwa ndio wahusika wampango huo dhalimu kwamba ni ukosefu wa busara wa hali ya juu kupoteza fedha zawalipa kodi kutaka kunidhuru.

Ingekuwa vema raslimalizinazotumika kufanikisha mpango huo zikaelekezwa kwenye uchunguzi wa mabilioniya fedha za Watanzania yaliyofichwa kwenye mabenki nchini Uswisi huku nchi yetuikikabiliwa na deni kubwa la ndani na nje la zaidi ya shilingi trilioni 30!

Lichaya kuwa na mwangaza kuhusu mahala linakoanzia tishio hilo kutoka huko nyumbani, sina hakika kama ni mkakati wa kitaasisi au ndiyo yaleyale niliyowahi kuandika katika makala yangu moja huko nyuma juu ya kuwapo kwa rogue elements katika taasisi zetu nyeti.

La muhimu kwangu kwa sasa nikuhakikisha kuwa majahili hao hawafanikiwi katika azma yao. Pia sioni haja ya kuvifahamisha rasmi vyombo vya dola huko nyumbani. Itoshe tu kusema hapa kwamba mipango kama hii katika zama hizi haina tena tija.

Hakika suala hili limenikera sana lakini ninajitahidi kuzingatia busara za mwandishi wa Laws of Power, Robert Greene, ambapo kanuni ya 21 inausia kuwa “Play a Sucker to Catch a Sucker –Seem Dumber than your Mark” (yaani, kwa tafsiri isiyo rasmi,jifanye mjinga kumnasa mjinga).

Kanuni hii inasema, ninanukuu, “Noone likes feeling stupider than the next persons. The trick, is to make your victims feel smart – and not just smart, but smarter than you are. Oncec onvinced of this, they will never suspect that you may have ulterior motives”(hakuna mtu anayependa kuonekana mpumbavu zaidi ya mtu mwingine. Ujanja nikumfanya mlengwa wako ajione mwerevu, na si mwerevu tu bali mwerevu zaidi yako.Pindi akaamini hivyo, hatohisi kuwa una nia kubwa zaidi yake).

Nimalizie makala hii kwa kusisitiza kuwa vitisho kama hivi kamwe havitonizuwia kusimamia ukweli na kuuhubiri pasi kumhofia mtu au taasisi.

Ninatambua yaliyowakumbabaadhi ya waandishi wa habari wa nyumbani.

Kwangu hizo ni chachu za kuendeleza walichoanzisha.

Kadhalika, ni vema walioandaa mpango huo dhalimu wakatambua kuwa licha ya kitendo hichokuwa na uwezekano wa kuharibu ‘mahusiano ya kiusalama’ kati ya nchi yetu naUingereza (kwa kuwatwisha mzigo usio wa lazima kuhakikisha mimi kama mkazi wanchi hii sidhuriwi), lakini pia kinakwaza kiapo changu cha utii kwa nchi yangu (nilipokuwa mtumishi wa umma) ‘kuyaacha mambo fulani yaendelee kubaki yasiyopaswa kuongelewa hadharani.

’Laws of Power ya 19 inasisitiza, “Never offend a wrong person” (kamwe usimkorofishe mtu asiyestahili).

"If you're not ready to die for it,take the word 'freedom' out of your vocabulary" ~ Malcom X
 
Interesting! Mkuu unaweza kuweka hapa bandiko lake lolote ili tuone kama ni tishio?

Akina Mzee Mwanakijiji wanaliza watu kila siku na wanafahamika si wangeshakuwa historia kama Stan Katabalo!
 
Last edited by a moderator:
Simfahamu huyu bwana wala background ingawa kuna makala moja ambayo aliandika na between the lines nilihisi ni mtu wa Usalama wa Taifa.
Chahali ni TISS, sema aliasi. Ingawa kuna usemi usemao "Ukishakula nyama ya mtu........"

Ni kawaida watu wa idara hizi duniani kote kufuatiliana, sishangai na wala haitokei kwake tu. Labda kama anatafuta public sympath
 
Interesting! Mkuu unaweza kuweka hapa bandiko lake lolote ili tuone kama ni tishio?

Akina Mzee Mwanakijiji wanaliza watu kila siku na wanafahamika si wangeshakuwa historia kama Stan Katabalo!
Ukurasa wa 20 wa Raia Mwema ya jana.Najaribu kuangalia elecronic version ingawa mara nyingi Raia Mwema wanachelewa kuweka gazeti lao mtandaoni.Naamini JF kuna wajuzi wanaweza kutuwekea.
 
ATTENTION SEEKER AT WORK.

Kitu cha ajabu hata mleta mada hamfahamu huyu jamaa. achilia mbali watanzania wengine wa kawaida.

Humu duniani ogopa sana hii kitu inayoitwa spinning. Huyu jamaa sitashangaa kama anatengeneza mazingira ya kutaka kuuza makala zake 'mahili' za kisiasa.

Haitakuwa ajabu kama hatawaokota wengi ambao ni matajiri wa fikra finyu.

Kama walioko ground zero wanatembeza siasa ambazo mpaka serikali inakuna kichwa na bado wako huru kutembea mitaani na kunywa kahawa kwenye vijiwe. Yeye huyu jamaa amefanya nini mpaka serikali ipoteze pesa kwa ajiri ya gharama za Convert operation.

Kwa mawazo kama hayai, basi hitimisho ni kila mtanzania maisa yake yako hatarini.
 
Chahali ni TISS, sema aliasi. Ingawa kuna usemi usemao "Ukishakula nyama ya mtu........"

Ni kawaida watu wa idara hizi duniani kote kufuatiliana, sishangai na wala haitokei kwake tu. Labda kama anatafuta public sympath
Suala kubwa ni kuwa kwa nini atishiwe maisha,tena mbali na nyumbani? Je ana organize mpango wa kupindua serikali? Je makala zake ndani ya Raia Mwema? Naamini haya ndo maswali ya msingi ambayo tunatakiwa tutafakari.
Kuna suala la Ulimboka ambao limeitia doa idara yetu takatifu na hili likiwa ni kweli ina maana kuna kasoro fulani mahali fulani.
 
"if u are not ready to die for it,take the word 'freedom' out of your vocabulary-Malcolm X"
Kama kweli una nia ya kuendeleza mapambano basi GO ON but kama ni pandikizi ni bora tu urudi kwenu kama walivyofanya wakina stupid Shonza.
 
Suala kubwa ni kuwa kwa nini atishiwe maisha,tena mbali na nyumbani? Je ana organize mpango wa kupindua serikali? Je makala zake ndani ya Raia Mwema? Naamini haya ndo maswali ya msingi ambayo tunatakiwa tutafakari.
Mkuu, kama uliwahi kuwa mmoja wa watu hawa, tena umewahi kushiriki covert mission yoyote na ukaachia ngazi basi ujue lazima utawindwa. Si ajabu, haishangazi hata kidogo. Chahali anajua sababu ya kufuatiliwa, anajua wazi hata akiandika gazetini wakiwa wamedhamiria kuikamilisha kazi yao kwake watamfikia tu. Najua, kuandika ni ku-pre-empty lakini inaweza isifanye kazi kama mkakati upo. Si yeye pekee alokimbia, wapo wengi. Yeye anatambulika kwa jina, wengine ni undercover mara zote.

Sitaki kuamini kuwa Chahali ana mkakati wa kuipindua serikali, hapana; makala zake chokonozi kwa Idara yawezekana ndiyo yanayomgharimu. Hata ukiwa CIA ukaasi, ukianza kuandika makala za kuiponda ujue hatma yako iko hatarini.
Kuna suala la Ulimboka ambao limeitia doa idara yetu takatifu na hili likiwa ni kweli ina maana kuna kasoro fulani mahali fulani.
Hakuna idara takatifu; labda ingetokea Ikulu ikawa takatifu. Alofanya mission ya Ulimboka si mtu wa TISS, ni wahuni wanaoingizwa huko bila kufata ethics na hawana utaalam wowote wa covert missions. Angekuwa mtu maalum wa kazi, basi Ulimboka angekuwa historia kwa sasa.
 
Interesting! Mkuu unaweza kuweka hapa bandiko lake lolote ili tuone kama ni tishio?

Akina Mzee Mwanakijiji wanaliza watu kila siku na wanafahamika si wangeshakuwa historia kama Stan Katabalo!
Mbona unaji contradict,Mwanakiji analiza watu kil siku na hapo hapo unataja Katabalo ambae kifo chake kina utata au Mwanakijiji ni mwenzao?
 
Nimejaribu ku attach
Mkuu nimeisoma hiyo makala, nilichogundua ni kwamba huyu Bwana anajua maadui zake wanamuwinda ni kina nani na wanafanya hivyo kwa sababu gani. Inalelekea kuna mambo mengi anayajua ambayo wanaomtafuta kumtoa roho wana wasiwasi akiyaweka hadharani watabaki watupu.

Lakini amenifurahisha aliposema;
"Kwa bahati nzuri, watu hao wanafahamu fika kuwa nina ujuzi wa kutosha na kuelewa na kumudu fika mbinu za kuishi kwa tahadhari".

Ninashawishika kuamini kwamba huyu Bwana ni ex-system kama mchangiaji mmoja alivyosema.

Tiba

Kwa sentensi hiyo kwenye red huhitaji kujiuliza Chahali ni nani. Ndiyo, anajua nani anayemfuatilia, anajua technics gani wanatumia na anajua endapo atashindwa kuwamudu wanaomfuatilia huenda akadhurika yeye. Nampendea kitu kimoja, ni pro change!
 
Suala kubwa ni kuwa kwa nini atishiwe maisha,tena mbali na nyumbani? Je ana organize mpango wa kupindua serikali? Je makala zake ndani ya Raia Mwema? Naamini haya ndo maswali ya msingi ambayo tunatakiwa tutafakari.
Kuna suala la Ulimboka ambao limeitia doa idara yetu takatifu na hili likiwa ni kweli ina maana kuna kasoro fulani mahali fulani.

the same reason why the Kremlin poisoned their ex-KGB Litvinenko who lived in exile(LONDON)
images
 
The thing is hataki kusema na kurudisha hesabu za wenyewe,yeye anavuta mshiko wa kazi maalumu halafu hatekelezi ndio maana wenzake hawamuelewi,hebu tumuulize riports zao zote amerudisha?,labda wenyewe wanadoubt huenda akazitoa gazetini au zikafika pahala sipo,mind kuwa muhaini sio lazima ubebe bunduki!!
 
Huyu bwana huwa ananiacha hoi kwa jinsi anavyojifikiria kuwa yeye ni maarufu, hizo makala zenyewe anazoandika huwa hazina lolote la maana, kama ni mambo yake na TISS uko aache kutafuta sympathy kupitia makala, au inawezekana aliishiwa cha kuandika.
 
utawajua tu....
 
The thing is hataki kusema na kurudisha hesabu za wenyewe,yeye anavuta mshiko wa kazi maalumu halafu hatekelezi ndio maana wenzake hawamuelewi,hebu tumuulize riports zao zote amerudisha?,labda wenyewe wanadoubt huenda akazitoa gazetini au zikafika pahala sipo,mind kuwa muhaini sio lazima ubebe bunduki!!
Ujumbe umefiks
 
Back
Top Bottom