EU yatoa msaada bilioni 960/-

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
UMOJA wa Ulaya (EU) kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya (EDF), umeipatia Tanzania Euro milioni 385 sawa na Sh bilioni 960 kwa ajili ya kutekeleza miradi minne ya maendeleo. Kiasi hicho ambacho kiliidhinishwa jana asubuhi Makao Makuu ya EU, Brussels Ubelgiji, kimeelezwa ni kikubwa kuwahi kutolewa na umoja huo kwa Tanzania.

Miradi minne ambayo itanufaika na fedha hizo ni pamoja na Mkataba wa Malengo ya Milenia (MDG) kupitia Mfuko Mkuu wa Bajeti ya Serikali (GBS) ambao utapata Sh bilioni 546 na mradi wa kujenga na kukarabati barabara. Mradi wa tatu utahusisha sekta ya nishati hasa katika suala la upatikanaji wa nishati mbadala kwa maeneo ya vijijini (Sh bilioni 14) na wa mwisho unahusu kuisaidia Wizara ya Fedha na Uchumi kwa ajili ya kuboresha uwezo wake wa kuandaa mikakati ya kupambana na umasikini.

Zaidi ya miradi hiyo minne, Tanzania pia imepewa Sh bilioni 26 kupitia bajeti kwa ajili ya kufidia athari zilizopatikana mwaka jana kutokana na bei kubwa ya mafuta ya petroli na mahitaji ya ziada ya chakula yaliyojitokeza. Balozi wa EU nchini, Timothy Clarke akizungumzia msaada huo, alisema EU haijawahi kuamua kwa mara moja kutoa kiasi kikubwa kama hicho cha fedha kwa Tanzania tangu miaka ya 1970 ambapo umoja huo ulianza kutoa misaada.

Clarke alisema msaada huo unatoa garantii na uhakika wa kutolewa fedha hizo kwa kipindi cha miaka sita ijayo. Tanzania ni kati ya nchi saba ambazo zimefaidika na msaada huo. “Hiki ni kipimo cha imani yetu kwa Tanzania kwamba itaendelea kwa nguvu zaidi kupambana na changamoto za kiuchumi zilizopo mbele yake na kuweka utawala bora, uwajibikaji, uwazi na kupambana na rushwa kuwa ajenda yake kubwa,” alisema Clarke.
HabariLeo | EU yatoa msaada bilioni 960/-
 
hela nyingi ya misaada lkn maendeleo sifuri.Tunashukuru lakini kwa msada,
 
Pesa hizo zinakwenda wapi? au kama wakubwa ndio wanaokula?Tujiulize sisi wabongo kuna maendeleo gani mpaka sasa? Miji inakosa Umeme maji Safi tunatumia Visima badala ya mabomba ya maji?Rushwa imezidi hakuna Maendeleo yoyote yale Watu wote wanakimbilia mijini na kuacha Vijijini,Ardhi nzuri tunayo Maji ya kutosha tunayo lakini bado mijini tunakosa Umeme na Maji Ya kunywa Je hayo ndio Maendeleo? Tutafika kule tunakokwenda?Mito,Maziwa,tunayo lakini tunashindwa ni jinsi gani namna ya kutumia hiyo Mito na Maziwa?Uchumi tunao lakini tunaukalia Je tutakuwa mpaka lini Masikini wa kuomba omba Misaada kutoka nje?itafika wakati hao wanaotupa Msaada Watachoka kutupa hiyo Misaada na Wataacha kutupa hiyo Misaada tutakuwa Omba Omba Mpaka lini? Watanzania Wenzangu?Tujiulize hilo? kila wakati. Tuache kuogopana kuambiana ukweli na vitendo ndivyo vinavyotakia sio kunyamaza kimya tu.
 
Mwandishi wa habai hii kachapia. Mpaka leo Euro moja haijafika hata T.shs 2000, ni kama 1840 kwa maana hiyo Euro milioni 385 ni sawa na bilioni 708.4 tu.

Back to the point, inabidi hawa jamaa wa EU kama wako seriuos na misaada yao wasimamie wenyewe hiyo miradi ya barabara na umeme vinginevyo hizi pesa atakula Rostam Azizi na washirika wake na hakuna cha maana kitakachofanyika..
 
Back
Top Bottom