EU Walaani Tamko la Vyombo vya Usalama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

EU Walaani Tamko la Vyombo vya Usalama!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Buchanan, Oct 13, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hussein Issa na Salome Kuga

  TAMKO la mnadhimu mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo bado linakosolewa baada ya waangalizi wa uchaguzi mkuu kutoka Jumuiya ya Umoja wa UIaya (EU) kulaani kitendo hicho, wakieleza kuwa kimevuka mipaka ya shughuli za chombo hicho.

  Akitoa tamko hilo Oktoba mosi, Shimbo aliwaambia waandishi wa habari kuwa vyama vya siasa havina budi kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu yatakayotangazwa baada ya upigaji kura na kwamba vyombo vya usalama vimejiandaa kikamilifu kupambana na yeyote atakayejaribu kuyakataa.

  Hata hivyo, serikali imekuwa ikimtetea Shimbo kwa kusema kuwa alitoa tamko hilo kama kiongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ma si kama kiongozi wa jeshi na kwamba kitendo alichofanya ni sahihi.
  Badala yake, tamko hilo lilipingwa na vyama vya siasa, taasisi za kijamii na wasomi ambao walitafsiri kuwa ni vitisho dhidi ya wapigakura na kwamba lililenga kulinda ushindi usio wa haki.

  Jana, mwangalizi mkuu kutoka tume ya Ulaya inayoshuhudia uchaguzi mkuu nchini, David Martin alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa kazi ya kuonya dhidi ya vurugu wakati wa kampeni inatakiwa ifanywe na Tume ya Uchaguzi (Nec).


  "Kauli hiyo ilitolewa kimakosa kwa kuwa zipo tume za uchaguzi... inakuwaje tena JWTZ kuhusika kutoa kauli kali kama hizi tena katika kipindi hiki cha uchaguzi," alihoji Martin.

  Martin alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kazi yao ya kuangalia mwenendo wa uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika Oktoba 31 na ndipo alipoulizwa swali kuhusu tamko hilo la Shimbo.

  Martin alisema kuwa ujumbe wake umekuja kutathmini kwa kina mchakato mzima wa uchaguzi na kuangalia kiasi gani uchaguzi unaheshimu kanuni za kimatiafa zinazotawala chaguzi za kidemokrasia na sheria za nchi.

  Kwa mujibu wa Martin ujumbe huo unaohusisha Kamisheni ya Ulaya, Baraza na Bunge la Ulaya ni tume huru inayofanya kazi zake bila kukipendelea chama chochote cha siasa.

  "Tuko hapa kwa ajili ya kuendesha shughuli zetu kwa uhuru bila kuegemea au kupendelea upande wowote," alisema.

  Martin alieleza kuwa jukumu la msingi lililowaleta nchini ni kuangalia mchakato mzima wa uchaguzi na kwamba baadaye watatoa ripoti maalumu ya kitaalamu ambayo alisema itakayosaidia ukuaji wa demokrasia nchini.

  Alieleza kuwa siku ya uchaguzi kutakuwa na kikundi cha wataalamu sita wakishirikiana na waangalizi 22 wa muda mrefu, na wengine 42 wa muda mfupi ambao kwa pamoja watakuwa wakifuatilia zoezi la upigaji kura Bara na Visiwani.


  "Kazi ya watalaamu hao ni kuangalia tu na hawatatenda chochote ambacho kitaweza kuingilia au kushawishi uchaguzi kwa kuwa si jukumu la tume hii," alisema Martin na kuongeza:

  "Lakini nategemea kuwa ripoti yetu ya mwisho ambayo tutaiwasilisha kwa viongozi wa Tanzania miezi miwili au mitatu baada ya uchaguzi, itawasaidia kwenye maamuzi ya mustakabali wa demokrasia ya nchi yenu," alisema.

  Wakati akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari Agosti mosi, Shimbo alikuwa ameambatana na naibu kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi, Peter Kivuyo na mkuu wa Operesheni Maalum (DCP), Venance Tossi.

  Siku hiyo, Shimbo alisema
  : "Tuko tayari kupambana na yeyote yule; kuna matamshi makubwa yanatolewa kuwa damu itamwagika; hakuna damu itakayomwagika na wala hatutaruhusu jambo hilo kutokea na asitokee mtu akajaribu kufanya hivyo; uchaguzi umeanza vizuri na uishe vizuri."

  Kwa mujibu wa Luteni Jenerali Shimbo, vyama vya siasa, wagombea na wapambe wao wanapaswa kufanya kampeni kwa ustaarabu na kwa kufuata sheria na kanuni za uchaguzi zilizopo.

  Pamoja na kueleza kuwa kuna wanasiasa ambao wanatoa matamko ya uchochezi, hadi sasa Jeshi la Polisi halijamkamata mtu yeyote na kumuhusisha na tuhuma za uchochezi, jambo ambalo kisheria ni kosa.

  Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa amekuwa akipa changamoto Jeshi la Polisi kukamata wanasiasa ambao wanatoa kauli zinazoonekana zinalenga kumwaga damu badala ya kutoa vitisho.

  Kauli ya Martin imekuja siku chache baada ya Mtandao wa Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu (FemAct) kutoa tamko la kulaani kitendo hicho.

  Mbali na kulaani tamko hilo FemAct, ambayo imeundwa na mashirika 50 yasiyokuwa ya kiserikali, ilisema inaamini kauli hiyo ya Shimbo haikutolewa bure bali kwa msukumo wa chama fulani cha siasa.


  Source: MWANANCHI
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Oct 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Labda wenye ngozi nyeupe wakiongea akina Shimbo, Kinana, JK, et al, wataelewa sasa maana sisi walala hoi hatujaeleweka!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa atapandishwa kwenye ndege na kusindikizwa airport..
   
 4. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Juzi nilimsikia rais Museveni akisema kuwa uganda imekwisha acha kutegemea wafadhili kwa ajili ya bajeti ya maendeleo na akatoa mifano ya miradi ya kuzakisha umeme n.k ambayo inatekelezwa kwa fedha za waganda wenyewe.

  Sasa sisi rais wetu kweny kampeni ansifia jinsi tanzania itakavyopata misaada kutoka kwa nchi zingine kama vile marekani n.k na hataki kabisa hoja zinzohusu nchi kujitegemea kwa kutumia raslimali zake yenyewe.

  Mfano hai ni ahadi ya kujenga nyumba za waalimu kwa shilingi bilioni 260 kwa hisani ya watu wa marekani ilhali epa peke tyake ziloifujwa nusu ya kiasi hicho bilioni 133 zenye uwezo wa kujenga shule za sekondari 1330 kwa kila moja kugharimu milioni 100.

  Kwa hali hiyo jk hawezi kamwe kuwatimua wazungu hao
  .
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  TAMKO la mnadhimu mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo bado linakosolewa baada ya waangalizi wa uchaguzi mkuu kutoka Jumuiya ya Umoja wa UIaya (EU) kulaani kitendo hicho, wakieleza kuwa kimevuka mipaka ya shughuli za chombo hicho.

  Jana, mwangalizi mkuu kutoka tume ya Ulaya inayoshuhudia uchaguzi mkuu nchini, David Martin alisema jijini Dar es Salaam kuwa kazi ya kuonya dhidi ya vurugu wakati wa kampeni inatakiwa ifanywe na Tume ya Uchaguzi (Nec).

  "Kauli hiyo ilitolewa kimakosa kwa kuwa zipo tume za uchaguzi... inakuwaje tena JWTZ kuhusika kutoa kauli kali kama hizi tena katika kipindi hiki cha uchaguzi," alihoji Martin.
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,887
  Trophy Points: 280
  Wenye akili wameliona hilo. Ila Kinana na Makamba walimpongeza sana Shimbo
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona ata wadhungu wameliona ilo basi angalau CCM watatoa matongotongo machoni mwao
   
 8. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Walituona sisi walala hoi hatujua majukumu yao ya kiutendaji na mipaka yao ya kiutendaji sasa hao EU walinza na kutaka kujua utendaji wa JW ni upi katika nchi hii na wakagungua wao ni kulinda mipaka na kuhakikisha nchi haivamiwi na wabaya wetu

   
 9. D

  Dick JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ametimiza wajibu wake, big up!
   
 10. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  amiri jeshi mkuu ni kikwete na ndie aliemweka shimbo madarakani, hivyo hapo wadau mi naona yeye ni mbizi wa kafara tu..
  hatuwezijua inawezekana ni amri ya amiri jeshi mkuu hivyo shimbo akawa mdogo kama piriton
   
 11. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  masikini kikwete anavyopenda safari za nje .... mbona sasa hivi yanagonga pants na kurudi....lol
   
 12. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuu nimeipenda comment yako ingawa umeandika kama mtu aliyeng'oka meno ya kung'atia miwa.
   
 13. R

  Rugemeleza Verified User

  #13
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kila mtu mwenye akili timamu alielewa kuwa kauli ya Shimbo ilikuwa ni ya hatari kama sio kinyume cha sheria. Ajabu CCM Makamba, Kinana na Membe wakaisifia. Hao ndio viongozi bora wa CCM na ndio wametufikisha hapa. Ajabu yake wanakuwa na ushujaa wa kifisadi kutetea uozo.
   
Loading...