Eti!"wamebobea kwenye Uchumi",Inaumiza,Inashangaza na kusikitisha!!!!!.

article

Senior Member
Sep 10, 2016
177
334
Uchumi unaweza ukatolewa tafsiri na maana lukuki kwa mujibu wa wabobezi katika masuala ya kiuchumi nchini na ng'ambo.
Sio lengo langu kutoa maana ya neno hili lakini ili niweze eleweka kwa nilichokusudia kuwakilisha kwenye hili jukwaa la wenye fikra pevu ni vizuri nikatoa ufafanuzi uchumi ni nini,na maneno mengine machache kwenye ufafanuzi yana maana gani kwa muono wangu.
Uchumi ni nguvu ya kuendesha maisha ya Mwanadamu inayotokana muunganiko wa mali zinazoonekana na mali zisizoonekana. Nguvu ni nishati inayowezesha kitu mfu au hai fulani kiweze kufanya kazi iliyokusudiwa.Mwanadamu ni kiumbe hai mwenye hisia na uelewa mkubwa wa masuala mbalimbali kwenye maisha yake akiwa hai na baada ya kufa. Na hii ni sifa kuu inayomtofautisha na viumbe wengine walio hai kwenye dunia.Mali ni maliasili ambayo inamilikiwa na mtu au kikundi cha watu kihalali inayotegemea kuwa au kuleta faida ya kiuchumi kwa mtu au kikundi cha watu husika baadae.
Wabobezi katika masuala ya Uchumi mara nyingi uchukuliwa kwamba ni wale ambao wamesesomea masuala kiuchumi na kufikia hatua za juu za kimasomo kwenye fani hii lakini kwangu mbobezi wa uchumi ni yule mwenye majibu ya changamoto,mipango,sera na mbinu sahihi na tatuzi za kiuchumi na mwenye msimamo usiyoyumba inabokuja suala la utekelezaji wa mbinu ,mipango na sera zake za kiuchumi bila ya kujali kiwango chake cha elimu ya darasani na fani yake ya utaalamu unaopatikana kupitia darasani.
Mara nyingi wachumi wamekuwa wakitoa tafsiri na ushauri wa masuala mbalimbali ya kiuchumi kwa umma na idara au taasisi mbalimbali pale wanapoitajika ila matunda ya kazi zao imekuwa ni vigumu kupimika kutokana matokeo hasi yenye utata kwenye nchi husika wanazoshauri.
Ushauri wao umekuwa wa mchango mdogo kwa jinsi ninaovyoona kwenye kuimarisha uchumi ,kutatua changamoto za kiuchumi na kutoa muelekeo wa uchumi hasa nchini,Mara nyingi ushauri wao umekua chanzo cha mabadiriko hasi ya kiuchumi na hili halijapewa nafasi ya kujadiliwa kiupana na kiundani kwenye sehemu za mijadala huru kama hapa Jamii forum,mijadala mingi imejikita kuwajadili na kuwakosoa viongozi wa kisiasa na wasio wa kisiasa wanaofanya maamuzi mengi ya kiuchumu kwa kutegemea ushauri wao potofu na usio na muono wa mbele.
Kwa mfano wanaoitwa wabobezi wa uchumi inchini wengi wamekaririshwa na kuaminishwa eti ili nchi iendelee inatakiwa nchi iwekeze sana kwenye miundo mbinu hivyo nchi imekuwa ikikopa sana ili kuwekeza kwenye miundo mbinu na deni la Taifa linalotokana kwa kiasi kikubwa na mikopo kwa ajili ya miundo mbinu hivi karibuni huko Bungeni Dodoma lilizua mjadala mzito uliosambaa mpaka kwenye mitandao ya kijamii kutokana kuonyesha kuongeza mwaka mpaka mwaka huku wachumi wakishindwa kuonyesha jinsi gani deni hili kubwa litalipika, wakijikita zaidi kwenye faida zinazoonekana za deni na kuachilia mbali hasara kubwa iliyojificha kwenye Deni hili.Kabla ya kukopa tunafahamu kwamba lazima ufanye tasmini na ujue jinsi gani ,kiasi gani na kwa mda gani utalipa Mkopo kwa zamana iliyokubalika bila ya kusahau tasmini ya hatari (Risks) za mkopo na wewe utapata kiasi gani kutokana na mkopo ndani ya mda wa mkopo na nje ya mda wa mkopo huo, nina hofu kama wachumi wetu huwa wanalifanyiaga tasmini hii kikamilifu ,kiusahihi na kizalendo na kwa kutanguliza maslai ya taifa letu mbele!!! .Nadhani Mikopo hii imetuongezea umaskini na kuzitajirisha nchi zinazotupa misaada ili zitujengee miundo mbinu ambayo tunaweza kuijenga sisi wenyewe bila ya msaada wa watoa mkopo bila kujijua huku wachumi wakisema kukopa kwa ajili ya miundo mbinu ni muhimu sana kwa mandeleo ya nchi bila ya kujua kuwa maendeleo haya siyo endelevu!
Tukope kwa ajili ya uzalishaji mali na si vinginevyo huu ni mtazamo endelevu wangu ninaotegemea kuwa utapingwa vikali kama vile Mtizamo na maono ya yule aliyepingwa na aliyesulubiwa kwa mawazo na mtizamo wake yenye utofauti wa hali ya juu na baadae kuchukuwa ufalme wa filosophia na kuteka karibia dunia nzima kwa uwezo wake wa zaidi ya Mwanadamu wa kawaida.
Miundo mbinu ya nchi isijengwe kwa fedha , wataalamu wa kukopa au kampuni za kigeni na pia Nchi hiache kusomesha wataalamu wa sanaa kwa kuwa si wazalishaji na pia iwastaafishe watumishi karibia wote kwenye fani ya sanaa wabakie na wana sheria tu kwa manufaa ya umma na Nchi ijikite kusomesha kwenye science na teknologia,fedha na biashara Nchi ifute elimu bure kwa sekondari na itoe elimu bure kwenye vyuo vya ufundi na vyuo vikuu kwa nyanja za elimu nilizozitaja.
Nafahamu mtaniuliza "sasa hizo mali zikizalishwa zitasafirishwaje kwenda sokoni?" Jibu la swali "Watumwa walifikaje Amerika kutoka Afrika?" linaweza kusaidia kupanua uelewa.Mzigo wenye soko ukiwepo, usafiri hauwezi kukosa ili mzigo huo ufike sokoni ,nafahamu hamjafundishwa huu mtizamo chimbifu kwenye vyuo vyenu huko mnapokwendwa kupata huo mnaouita utaalamu wa uchumi.

Mara nyingi ushauri wa nini kifanyike kutoka kwa wachumi wa nchi yangu unaegemea sana miongozo iliyopita ya wataalamu kutoka ng'ambo katika kufikia hitimisho la masuala nyeti kiuchumi nchini. Jambo hili linatia hofu sana kama ushauri wao utafanyiwa kazi kiutekelezaji hasa katika kipindi hiki cha utawala ambapo mwongozo wa ujumla unahitaji kubadirisha uchumi wa nchi yetu kwa asilimia kubwa kwenye nyanja mbalimbali.
Jambo jipya la kiuchumi kufanyika linakuwa linategemea kiasi kidogo mchango wa miongozo iliyopita hivyo wachumi wetu hawana budi kuandaa mifumo na sera mpya za kiuchumi ili kuja kukabiliana na changamoto za mabadiriko makubwa ya kiuchumi ambayo inchi imepanga kuyafikia kabla ya 2025.
Wachumi wetu ni nadra kuja na fikra mpya na utelezezaji mpya wa mipango na sera mara nyingi wanaegemea mifumo mingi ya kizamani,azimishi na tegemezi ambayo inachelewesha na kukwamisha maendeleo endelevu.Pia wengine ufunga safari ng'ambo eti kujifunza wenzetu wanafanyaje? Hawajiulizi hao wenzetu nao walijifunza kwa nani?Hivi nchi kama vile "China","U.K","U.S.A", Urusi na nyinginezo zilizo juu kiuchumi mlishawai kujiuliza zenyewe zilijifunza kwa nani au nani alikuwa " foreign consultant" wao mpaka kufikia hatua hiyo ya maendelo waliyofikia!!!!???. Eti tunaitaji ushauri kutoka ng'ambo!!!!,inasikitisha kusikia mambo kama haya kutoka kwa watu wanaoitwa wasomi lakini kusikitika na kusononeka haitoshi ndio maana nimeleta uzi huu na kuingia rasmi na kikamilifu kwenye kigoda hiki kutoa mitazamo yangu mbadala.Hivi ipo sahihi kuomba ushauri wa kulinda mali zetu nje?? .Hivi ni sahihi kumpa jambazi akuhifadhie ufunguo wako wa hazina ?.Tafiti za wang'ambo zinaweza fanyika kwetu bila malipo au kwa malipo kiduchu ila sisi kwao tunajipukuta mifuko yote!!! hivi kiuchumi hii inakubalika??
Mara nyingi wachumi utumia historia ya nyuma kiuchumi kutabiri yajayo au kulinganisha matokeo ,jambo ambalo linaleta maswali mengi yenye majibu tegemezi kutokana na uchumi kutokuwa mgando.
Wamekuwa wakipotosha ukweli kuhusiana na umaskini na utajiri kwa kutoa tafsiri potoshi waliyofundishwa na kuikubali bila ya kufanyia uchambuzi kama ipo sahihi au hapana.Kwa mfano wameigawa Tanzania miongoni mwa nchi maskini zaidi ulimwenguni kwa kigezo cha kipato cha kifedha cha mtu kwa mwaka bila ya kujali uhalali wa kipato hicho na kipato hicho kinamnufahishaje mhusika.Tanzania siyo inchi maskini jaribuni kufikiria zaidi ya hapo mlipofikia ni nchi pekee africa ya kwanza kuzisaidia inchi nyingine ,yenye mali zote zenye samani kubwa kwa ajili ya maendeleo katika nyanja zote na ya kwanza Africa na dunia kwa ujumla kwenye maendeleo ya kweli .Nachekesha eh!!??.
Wachumi huwa wanashauri kuhusu masuala ya kiuchumu ili kwa bahati mbaya ufahamu wao ni mdogo sana kwenye masuala ya mali ambayo ndio msingi wa Uchumi popote duniani na hii inaniongezea hofu kuendelea kuwategemea wachumi wetu kwa kuwa pia maanuzi yao hayazingatii Msingi wa uchumi wetu ulioandaliwa kwa sayansi ya juu ya uchumi na Baba wa Taifa ambaye mimi namuita Baba wa Uchumi Africa ijapokuwa hawa wanaojiita wabobezi wamemshindwa kumpa sifa inayostaihili kwenye fani ya uchumi kwa kuwa wanaminishwa kuwa sera na mbinu za kiuchumi alizoasisi zilishidwa wakati sera zake nyingi ndizo zimefikisha uchumi wa inchi yetu hapa ulipo ila hawataki kulitambua hili suala la kujivumia.
Wachumi wamekuwa wakipotosha ukweli na kuzifanya nchi tajiri kujiona maskini na maskini kujiona tajiri na kuzalau nyingine kwa sababu tengenevu na baguzi kutumika kama kigezo cha kuita nchi tajiri au masikini.
Tafsiri ya umaskini kwa nchi kwa wachumi hawa ina mapungufu makubwa na haifai kwa matumizi ya kiuchumi kwa kuwa inaangalia zaidi mali zinazoweza kuthaminishwa kwa vipimio vya kifedha vilivyopo.Kuna mali nyingine ambazo samani yake ni kubwa sana lakini ni vigumu kwa vigezo vya kuthaminisha vinavyotumika kutoa thamani ya kifedha kwa mali hizi, kwa mfano Amani na utulivu mali zisizoonekana zilizo ardhini ,mawazo jengevu na jina la nchi na ukubwa wa eneo la nchi zalishi na isiyo zalishi. Anaweza akaja anayejiita mbobezi kwenye uchumi akacheka sana na Kusema eti! Amani na utulivu ,jina la nchi,mawazo jengevu ni mali na utajiri ?Namshauri akafanye utafiti kwenye maeneo haya.
Wachumi wetu ni watu wa kunakili kupitia wengine, wamekosa ubunifu na maarifa mapya wamekuwa ni wepesi wa kukosoa kupitia nakala za miongozo ya wengine.Hawaamini katika mawazo mapya wakati wakati wote mawazo mapya ndio yanayoleta maendeleo endelevu na ya kudumu na wao wanalifahamu hilo.Utawasikia wakisema eti "wenzetu hawafanyi hivi".Hakuna Nakala za mbinu za maendeleo endelevu ni vizuri wachumi wetu wakafahamu ilo ili waweze kuja na mbinu mpya za kuleta maendeleo zilizojikita katika mazingira ya kiuchumi ya nchi yetu na kuacha kupoteza fedha kwenye "consultancy".na kusoma historia za uchumi wa nchi za ng'ambo ambayo haina matunda kwetu.
Nchi ya pili kiuchumi dunia kwa sasa imedhibitisha ilo hivyo sasa ni wakati wa muafaka kwa wachumi wetu kuachana na nakala za majibu ya changamoto na mbinu za kiuchumi na kuja na majibu , mbinu na sera mpya na sahihi ya changamoto za kiuchumi nchini ili kuboresha uchumi wetu utao mhakisi mtazania wa kawaida na kuufanya wa kuingwa africa na dunia kwa ujumla kabla ya Fikiria kuomba ushauri wa kulinda mali zetu kama vile wanyama pori kwa asiye na wanyama pori na huku tukiwapuuza wazawa eti hawana elimu husika wakati wao wameishi na wanyama hawa kwa miaka isiyo hesabika na kupoteza fedha nyingi kwa ijili ya ushauri!.Hii kazi inawezwa kufanywa na mmasai bila ya kumpa ushauri wowote unaoitwa wa kitaalamu wala mafunzo ya darasani kwa kwa gharama ndogo na kwa ufanisi wa hali ya juu lakini angalia washauri wanavyoshauri ,"Drones zinafaa"
Nawakilisha,
Article.
 
Napenda sana kusoma, ila naomba uangalie namna ya ku put into summary. Inaonekana una mawazo mazuri sana na ya msingi baada ya kusoma paragraph mbili za bandiko lako.
 
Back
Top Bottom