Eti wachaga kuna ukweli ktk hili kuhusu nyinyi?

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Eti kwamba zamani ndugu wa kichaga walipogombana walikuwa wakiapizana
na kuvunja undugu ndo maana si ajabu kukuta majina koo nyingi za kichaga
yanapishana kidogo tu lakini unakuta wahusika hawajuani kabisa. Ila ukichunguza
pengine kisayansi kwa kutumia DNA uwezekano wa kugundua kuwa
wahusika ni ndugu wa damu ni mkubwa.

Hebu angalia majina haya!

Shao vs Shayo; Munishi vs Munisi, Lyaruu vs Lyatuu; Ngoma vs Nguma; Shuma vs Shirima; Mushi vs Moshi, Ngowi vs Ngoli, Kwai vs Swai. Mengine ongezeeni jamani!

Ila msikasirike jamani, nimelileta jukwaani kwa lengo la kuwekana sawa tu
mambo ya historia haya!
 
Ukipata bahati ya kujua ya wachaga mwili utasisimka. Mradi wachache tumdgundua, ni silaha tosha!
 
yap its true kuna jamaa jina lao la ukoo ni Kawiche aliambiwa na babu yake kwamba koo za kawiche na kaviche ni moja walitengana kwasababu ya ugomvi wa shamba
 
hamchokaji kuwajadili hawa viumbe
Tambueni haya mambo yalisababishwa na geografia
Hizo ni koo tu na hakuna ukweli wowote mbona hata lugha inatofautiana
Marangu na Rombo ni majirani saana lakini ukienda ROMBO kuna lugha tofauti zaidi ya NNE
Kirua Vunjo na Oldmoshi na majirani saana Wanaongea Vichagga tofauti kabisa, hali kadhalika, kibosho na Uru, Machame na Hai

na ukifuatilia saana utajikuta kilichosababisha hii kitu ni distance kati ya eneo na eneo na si vinginevyo
 
Kuna majina na kama Temu na Shayo ambako wanawake wlikuwa wanatambuliwa kama Matemu na Mashayo na baadaye yakaanza kujitegemea yenyewe
 
Ukipata bahati ya kujua ya wachaga mwili utasisimka. Mradi wachache tumdgundua, ni silaha tosha!

Yapi hayo mkuu maana wengine tunakaribia kupeleka posa huko! Ila kuna cousin wake wa kiume ndo wako karibu mpaka nakereka!
 
Back
Top Bottom