Eti wachaga kuna ukweli ktk hili kuhusu nyinyi?

Sio ugomvi,ni matokeo ya kundi fulani la mahali fulani kuhamia eneo lingine halafu muda unapopita kunatokea mabadiliko ya lugha yanayopelekea majina kubadilika pia.Mfano wachaga wapo wa aina kama 4 hivi,ukisikiliza wanavyozungumza ni tofauti lakini karibu nusu ya maneno ni yaleyale tofauti ni matumizi tu.Pia mfano Kenya kuna Kimath na uchagani kuna Kimath pia.Kenya kuna Mariga uchagani kuna Maringa,je na wakenya nao walikua wanaapizana?Sidhani!
 
Eti kwamba zamani ndugu wa kichaga walipogombana walikuwa wakiapizana
na kuvunja undugu ndo maana si ajabu kukuta majina koo nyingi za kichaga
yanapishana kidogo tu lakini unakuta wahusika hawajuani kabisa. Ila ukichunguza
pengine kisayansi kwa kutumia DNA uwezekano wa kugundua kuwa
wahusika ni ndugu wa damu ni mkubwa.

Hebu angalia majina haya!

Shao vs Shayo; Munishi vs Munisi, Lyaruu vs Lyatuu; Ngoma vs Nguma; Shuma vs Shirima; Mushi vs Moshi, Ngowi vs Ngoli, Kwai vs Swai. Mengine ongezeeni jamani!

Ila msikasirike jamani, nimelileta jukwaani kwa lengo la kuwekana sawa tu
mambo ya historia haya!

wengine Mboro, Mboryo, Mboruo. Hapo sasa
 
Back
Top Bottom