Eti unalazimisha kupendwa……..Thubutuu…………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti unalazimisha kupendwa……..Thubutuu…………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jul 5, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  hair-salon 400x267.jpg

  Kama unatamani kufanikiwa katika uhusiano wa kijamii, ni muhimu ukakubali ukweli kwamba si kila mtu atakupenda, si kila mtu atavutiwa na ujio wako na hasa kwa mara ya kwanza. Kila mtu anacho kifurushi cha sifa za vitu anavyopenda na asivyopenda ambavyo alivitengeneza siku nyingi.Usidhani una haja ya kujilaumu kama uliyeshindwa iwapo inaonekana mtu fulani hakupendi au havutiwi nawe.

  Kama kuna mtu anayekuchukia, sababu ya kukuchukia huko huenda ikawa na uhusiano mdogo na wewe ama huenda isiwe inahusiana kabisa na wewe. Huenda mtu huyo anakuchukia kutokana na kudhani unamuogopa ama kumkwepa, kuona haya ama kuonekana kutokuwa tayari kukaa naye na kuzungumza naye ama kutokuwa katika kiwango kimoja na yeye. Kwa kifupi huenda wewe na mtu huyo, ni watu tofauti msioweza kwenda pamoja hivi sasa.

  Usijisikie vibaya na kuanza kujiweka kando na kuwa mpweke kwa kudhani kwamba dosari zako ni kubwa kuliko sifa zako. Kwa kweli, huenda baadhi ya hizo dosari zikawa na mvuto mkubwa kwa watu wengine. Unaweza kuwa umenenepeana sana, lakini ukawa na tabasamu la kuvutia na furaha katika maisha yako. Wapo watu ambao mwili wako huo mkubwa unaweza kuwavutia ama wanaweza wasiuone ama kuonekana kero kwao. Unaweza kuwa na hali mbovumbovu au afya nyondenyonde, lakini ukawa na uwezo mkubwa katika kusakata dansi na mkweli kwa marafiki zako. Ukweli ni kwamba wapo watu wanaotafuta watu wakweli ama watakaowapatia furaha, wema au waungwana na hivyo wewe kuwa na sifa za kujenga nao urafiki.

  [FONT=&amp]Ikiwa una shaka kwamba wewe si mzuri wa kutosha wa sura na umbo kuweza kuwavutia marafiki wapya, hasa kwa wanawake. Lazima uelewe kwamba si kila mtu anatafuta uzuri wa sura kwa marafiki zake. Jifunze kupumzisha akili yako. Badala ya kujifunga kwenye mapungufu yako, weka mkazo kwenye sifa zako bora mbele ya watu. Boresha zaidi sifa nzuri ulizo nazo kwani hizo ndizo wale wanaozipenda zitawavuta kuwa karibu na wewe na si vinginevyo.[/FONT]
   
 2. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Nyce & constructive thread.
   
 3. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Well said,katika maisha huwezi kupendwa na wote! Lazma kuna watakaokupenda na watakaokuchukia tena bila hata sababu..what is needed ni kuishi maisha yako jinsi ambavyo unaona ni sahihi cause huwezi kumfurahisha kila mtu
   
 4. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  kweli tupu...
   
 5. f

  fidelis zul zorander JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 679
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  nice advice..na ni vyema watu wangejua kuwa sio muonkano mzuri tu ndo uakuletea mahusiano bali na tabia pia..
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,836
  Trophy Points: 280
  Nimejifunza
   
 7. salito

  salito JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  asante mkuu..
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ndio maana wanasema binadamu wote ni wazuri, kwa sababu kibaya kwako ni kizuri kwa mwingine.
   
 9. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Mimi sikubaliani! LOL
   
 10. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Hakika umenena!
   
 11. mito

  mito JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,642
  Likes Received: 2,030
  Trophy Points: 280
  Mkuu naona leo umeamua kumwaga mambo ya western tupu! haya bana......
   
 12. M

  Mathias BM Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Congratulation! you are the best!!
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe Mtambuzi
   
 14. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Very encouraging....hasa sisi wanawake, we should learn the sign, unalazimisha upendwe na matendo yanaonyesha vinginevyo
   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  ukivuka mtazamo wa kuishi kwa ajili ya wengine na kuanza kuishi kwa ajili yako, vitu kama hivi huwa havisumbui.
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hii inasaidia sana kwetu tunaohudumia jamii,,,,,maana kila mtu anakua na mtazamo wake kwako,,,,hili si kwa mwanamke tu hata kwetu MALEZ
   
 17. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Vipi kwani? Eiyer kalikoroga? Kakutamkia hakupendi? Maana Eiyer nae full madeko sa ingine.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Naomba kutofautiana na wewe dingi (kwanza Jana umelala wapi wewe?)
  Hiyo paragraph ya mwisho, I for one huwa sitafuti uzuri wa sura kwa marafiki wala mpenzi. It is the heart and compatibility that matters. So I have the ugliest friends (by the way I look more beautiful nikiwa nao, so ni double advantage hehehehe)

  Jioni tutaiongea kesi yako, naona maza anakushindwa sass. Nirushie vocha kabisa kutengeneza mazingara
   
 19. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Yaani graph ya mapenzi inazidi kudrop kila siku, sijui anataka kuoa waziri ila kamchomolea nje kwa kuwa yeye ni LY tu! LOL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Yeah ni kweli
   
Loading...