Eti umeoa! Umeoa nini wewe? Bora usingeoa tu

Marco Polo

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
11,742
18,477
Unamkuta kijana kila Mara tukikutana maskani anajisifia eti oohh! Mimi nimeo na nina watoto kadhaa huku akiponda wale ambao hawajaoa.

Kituko ni kwamba mtu huyo huyo ukimwangalia mke wake na watoto wake utawaonea huruma bora watoto lakini mke kachakaa mwili mavazi hanunuliwi yaani kiufupi jamaa hatoi matunzo kwa familia yake.

Imefika wakati mpaka mke wakati mwingine anatuomba sisi msaada wa fedha ya kutumia ndani kwake mpaka namuonea huruma binti wa watu.Sasa najiuliza kijana kama huyu alikimbilia nini kuoa wakati anatesa viumbe wa watu.

Ushauri; Vijana msimbilie ndoa kama hamjajipanga, ndoa ni sanaa na sayansi pana sana wengi wenu mnafikiri kwamba ndoa ni kujigi jigi tu.Badilikeni bwana la sivyo mtajikuta mna share mke na wenzako.
 
Mkuu huo ni mtazamo wako tu lkn kwa upande mwngne ndoa ni heshima na Mungu hawez kuwamnyima ruzik ya kula familia ile kuna watoto pale na nimalaika hata uwe masikin vip ukiwa na mke na watoto huwez kukosa pesa ya kuwalisha km ni mchakarikaj na suala la mavaz kupendeza kunawir ni it's just a matter of time tu mnashirkiana na mke wako kutafuta pesa na kwahal na mal bila kutofautiana yaan wote muwe na lengo moja itafika kipind mtatoka kimaisha no matter hw long mmeztafuta ila one day mtazpata tu zipo family nyng zmeanzia chin sana hata wengne wameanzia kukaa kwa kwao huku anamke inafka mda anakwake na mke wake yuleyule.
Kinachoumiza vijana ni kujiingiza kwenye makund ya vijana ambao hawajaoa na kuwa Na michepuko njee ya ndoa huku akitoa huduma thabt kwa michepuku, ulev na kuendekeza staree hapo lazma mke atateseka na kukondeana kwa mawazo hata km huna pesa ila ukakaa na mkeo na kuonyesha unamjal na kumpenda atarizika na kunawir tu...
Hivyo mleta uzi naomba uwashaur vijana kuoa mapema wasiwe waoga watoto wa njee ya ndoa wanaongezeka kila siku watu wanapesa zao na kuoa hawatak ni umalaya tu unatetea angalia marehem Kanumba amekufa hata mtoto hana angeoa mapema angekuwa na familia wakina Kiba,,Dullsaks watoto kibao njee kuoa hawatak ni kuendekeza umalaya tu...
Nakushaur kuoa mkuu acha Uzinifu
 
Tatizo mnasingiziaga kujipanga huku mnaendelea kuchakaza watoto wa watu na hivi huwa mnajipanga kitu gani hasa mi nasikiaga tu kujipanga kajipanga
 
Tatizo mnasingiziaga kujipanga huku mnaendelea kuchakaza watoto wa watu na hivi huwa mnajipanga kitu gani hasa mi nasikiaga tu kujipanga kajipanga
Hivi hao wanaochakaza wao wameumbwa kwa material gani mpaka wawe wanachakaza tu????
 
Back
Top Bottom