Eti Ukitaka Usioe Nenda Kwa Mdada Mapema Asubuhi

Eti Ukitaka Usioe Nenda Kwa Mdada Mapema Asubuhi

Wakuu

Kuna mahali nimesikia eti ukitaka kupata taswira halisi ya mdada basi we jifanye umejichanganya utokezee kwao mapema sana ile asubuhi.

Eti hapo ndo utaiona "taswira" yake halisi (na sio zile wanazopost kule insta, facebook n.k).

Eti paaaap....unakuta mtu ana sura kama anaskilizia maumivu ya kukata vitunguu.

Eti hata kama ulikuwa na mpango wa kutwaa mazima, unaweza kurudisha mpira kwa kipa.

Wakuu kuna ukweli hapa?
mbona dada zako na mama yako kila asubuhi unawaona na huchoki kuwapenda
 
Akili yako nyembamba haijajua mke ni nani na nini maana yake
 
Back
Top Bottom