Eti niolewe na mfuga kuku. Loh!!!

Eti niolewe na mfuga kuku. Loh!!!

Siku zote ananitoa out, tunaenda viwanja vikali vikali nikajua nimepata bae ambaye ni ofisa. Hee!! Kumbe mfuga kuku!!

Mara kadhaa amekuwa akijieleza kuwa hatokuwa na nafasi siku hii na hii kumbe anaenda kwenye mabanda yake ya kuku.

Tangu anitokee ni miezi 2 na kitu imepita, tulishafika hatua ya kukubaliana kuoana. Lkn muda wote huo nilikuwa sijaenda kwake.

Leo ktk kuupokea mwaka mpya ndiyo nimeenda mpk kwake nikakuta shughuli yake ya kumuingizia kipato ni kufuga kuku

Come on!! Nimekasirika sana. Yaani mm niwe na mume ambaye asubuhi namuandalia chai ili akafagie mabanda ya kuku? Nitaificha wapi sura yangu mbele ya mashosti zangu tuliomaliza nao chuo wakija kunitembelea? Never on earth!

Nataka mume namuandaa anaenda airport kuhudhuria kongamano mikoani ama nchi za watu. Siyo anahangaika na kinyesi cha kuku!

Ameniharibia sikukuu yangu huyu! Ananionaje kwanza mm? Nafaa kuwa mke wa mfuga kuku mm?? Huyo mwalimu tu asitie maguu hapa.
Aghiiiiiiii!!! Sitaki.
Ngoje uwe mhenga hata hata mfanya usafi wa chooni humpati. Heshima mjini ni pesa .Degree kitu gani bana wakati pesa huna unashindwa hata huyo mfuga kuku?
 
Pale mwanaume anapoamua kuwa mwanamke, kazi kwelikweli!
 
Wewe hutafuti mume, utakuwa unatafuta wanaume wa kuwalia pesa tu...mume si kazi nzuri kama unavyodhan ww..ukiangalia hivyo, bac utaambukizwa ukimwi na kufa bure
 
Mfuga kuku ana pesa kuliko hata wafanyakazi wengi tu,sema wewe umekariri! ebu fikria anapata trai nne za mayai,trai moja elfu 15,sasa elfu 15x4=60000tsh per day,kwa mwezi ana milioni na laki nane! hapo dharau inatoka wapi?
 
Hata sijajua bado jirani. Sababu kila kukicha anabadilika kama kinyonga.
d7c5bf11724f982ab5712756f3e40c1c.jpg

Kuna vituko saana jf...
 
BILA SHAKA ULIANDIKA THREAD UKIBANA PUA.

Roho nzuri hyo,UJE KUANGUKIA KWA MSTAAFU WA VITA VYA 2 VYA DUNIA
 
Lakini papuchi si alisha kukula. Aina shida endelea kuikaliza nyumbani utakuja olewa na mziba masufuriA
 
Mwanamke ka ww, mnaishia pabaya sana naona in unadharilisha elimu yako!!! Wew unataka kuolewa kwa showoff! Ungekuwa na Busara huyo ndo mwansume ambae ndoa yenu ingedum, kwa ww kuendelea kumtia moyo ili ikiwezkana baadae abadili kaz baada ya mtaji kukua
 
Hahahaaaaaaa hao wa hivyo hutokaa huwapate...Behind any successful man there is a woman...so nyuma ya hao kuna wanawake wenzako ambao wamevumilia na kuwafariji mpk kufikia huko....mpende na kumfariji uliyenae ili one day umsindikize airport kama exporter mkubwa sana wa chicken and chicken products.....
 
Siku zote ananitoa out, tunaenda viwanja vikali vikali nikajua nimepata bae ambaye ni ofisa. Hee!! Kumbe mfuga kuku!!

Mara kadhaa amekuwa akijieleza kuwa hatokuwa na nafasi siku hii na hii kumbe anaenda kwenye mabanda yake ya kuku.

Tangu anitokee ni miezi 2 na kitu imepita, tulishafika hatua ya kukubaliana kuoana. Lkn muda wote huo nilikuwa sijaenda kwake.

Leo ktk kuupokea mwaka mpya ndiyo nimeenda mpk kwake nikakuta shughuli yake ya kumuingizia kipato ni kufuga kuku

Come on!! Nimekasirika sana. Yaani mm niwe na mume ambaye asubuhi namuandalia chai ili akafagie mabanda ya kuku? Nitaificha wapi sura yangu mbele ya mashosti zangu tuliomaliza nao chuo wakija kunitembelea? Never on earth!

Nataka mume namuandaa anaenda airport kuhudhuria kongamano mikoani ama nchi za watu. Siyo anahangaika na kinyesi cha kuku!

Ameniharibia sikukuu yangu huyu! Ananionaje kwanza mm? Nafaa kuwa mke wa mfuga kuku mm?? Huyo mwalimu tu asitie maguu hapa.
Aghiiiiiiii!!! Sitaki.
Haha wenzako wanatafuta hata hao wafuga kuku na hawapati,kisaa kya mau
 
Back
Top Bottom