Eti, nani analeta Madawa ya kulevya Zanzibar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti, nani analeta Madawa ya kulevya Zanzibar?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bikra, May 17, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  May 17, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mnamo miaka 1985's MADAWA YAMEANZA kuingia visiwani bila ya kujulikana mletaji kuna dhana tu ,kuwa wafanyabiashara maarufu waliotumia fursa yao kwa vile milango yote wameidhibiti na wakuu wa nchi wako mikononi mwao kifedha.

  Kwa hiyo, hapo nataka kukwambia kuwa serikali kwa mlango wa nyuma ilisaidia kutendeka maovu.

  Wafanyabiashara hao hao ,baada ya kutajirika wao wamegeuka kufanya biashara nyengine kuona kumekuwa na high traffic na kimataifa ,Zanzibar imekodolewa macho kuwa ni kituo kikuu cha kupitisha mizigo hiyo na ripoti mbali mbali kimataifa kupata shutma ya biashara haramu na Utalii ndio ukastawisha mauzo ya madawa.

  Mara kadhaa, kuna ripoti za kukamatwa wahusika kesi ikienda polisi na ushahidi, mkemia mkuu akidhibitisha,mahakamani husemwa lilikuwa ni jivu la mkaa wa mkarafuu au muembe na habari kama hizo na kutolewa kauli, hakuna kesi ya kujibu na kesi dismiss ,vijana wanateremka habari ndio hii.....

  Vyombo vya ulinzi vimefikia kusaidia ubaya huu ,kwa vile wao kibinafsi wanakwenda mbio za bure .

  Hawa wanavijua vituo vyote ambayo wewe msemaji huvijui lakini ,mipango ikipanga siku ya ambush- wahusika wapelekewa habari in advance ,leo ni leo ikipita pekua pekua - matokeo hamna kitu.

  SURA ya mchezo mchafu hauondoki na ndio kipimo cha kuona watawala wapo wale na watawaliwa wache wafe mradi mambo yao yanawaendea vizuri ,Burda wa sharaba!

  Kwa ufupi, tusitafute mchawi ni sisi wenyewe.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mchawi ni lazima atafutwe kwa sababu si 'sisi' sote ni wachawi. Ni baadhi miongoni mwa 'sisi' ndio wachacwi, kama ulivyoonyesha mwenyewe makundi yanayojihusisha na biashara-vyombo vya usalama, wafanyabiashara na viongozi (wa kisiasa?). Hivyo ni lazima tutafute miongoni mwetu ni nani anahusika. Tukiachia kusema mchawi ni 'sisi' tutakuwa hatujitendei haki kwa sababu si 'sisi' wote tunahusika na biashara hiyo
   
 3. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Kwani ili tatizo liko Zanzibar tu? Mbona bara ndio zaidi na mwuungwana alikabidhiwa majina ya vigogo wanaojihusisha na hayo madawa lakini amekaa kimya mpaka leo? Sijui aliambiwa asiwachukulie hatua kwa kuwa walifund kampeni za uchaguzi zilizomwingiza ikulu?

  Vita dhidi ya drug trafikkers haiwezi kufanikiwa kama vyombo vya usalama na watawala hawatakuwa tayari kutoa ushirikiano unaostahili.

  Tiba
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Jul 12, 2013
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  duh!
  tatizo la madawa ya kulevya ni kubwa kuliko watu wanavyofikiri aisee, loh!
  si ajabu uongozi wa juu unagombewa kwa gharama yeyote makanisani na misikitini.
   
 5. mtu kitu

  mtu kitu JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2013
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  we raia ukitaka kuwataja basi wanakuuwa....wanajulikana ila hao waondoaji wa uovu huu nao wanapewa donge nono ili biashara iendelee....hili janga sio la zanzibar pekee .....ni tz yote
  tuwe makini......
   
Loading...