Eti mpaka leo Mangariba wapo?

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
7,971
13,605
Kuna jamaa yangu kapeleka watoto wake wawili mapacha kuwatahiri kwa hawa mangariba! Nimeshangaa sana.

Zama hizi za utandawazi ukamtahiri mtoto maporini? Kweli jamani? Haspitali zipo kibao, kwa nini umsababishie mtoto maumivu makali wakati angeenda hospitali angetumia gazi?

Hizi tabia za wazazi kupeleka watoto kwa mangaribu ni sehemu ya ukatili kwa watoto. Unaenda kumsababishia mtoto maumivu na uvujaji wa damu mwingi kwa hawa makatili wanaojiita mangaribaa.

Nimeshangaa sana.
 
ukitaka kujua tofauti ya mwanaume alitahiriwa na ngariba na alipelekwa kwenye utandawazi waulize wanawake
Wanajuaje kuwa hii dushe imepitia kwa ngariba au hospitali kwa daktari? Hizo ni story za vijiweni tu.
 
Ngaribas tupo mbona...tena wengi tu! Nikuunge kwenye group letu la Afrika Mashariki uchote maujuzi?
 
Ngaribas tupo mbona...tena wengi tu! Nikuunge kwenye group letu la Afrika Mashariki uchote maujuzi?
Kwa hali ya kawaida kuna vitu vilipaswa kuwa havipo tena. Mangariba mlikuwa mnasaidia kipindi cha nyuma wakati hospitali na vituo vya afya vilikuwa mbali. Ila kwa sasa huduma za afya zimesogezwa karibu, ni wakati wenu kupumzika.

Hii taaluma mmesomea wapi zaidi ya kuwa wajasiri na wakatiili? Nimuda wenu sasa kuachana na huu ukatili.
 
Back
Top Bottom