Eti Mohamed Abood "Alisoma" Shule Ambayo Haikuwepo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Mohamed Abood "Alisoma" Shule Ambayo Haikuwepo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Jul 6, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jul 6, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  WAKATI kinyang’anyiro cha urais wa Zanzibar kikizidi kushika kasi, mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohamed Aboud Mohamed, amepigwa kombora baada ya kudaiwa kuwa ameghushi vyeti vya elimu yake.
  Habari zilizopatikana jana kutoka mjini Unguja, zinasema Waziri Aboud alibanwa kwenye kikao cha Kamati Maalum ya Halmashari Kuu ya CCM-Zanzibar, kueleza namna alivyopata elimu yake.

  “Huwezi amini alibanwa na mmoja wa wajumbe waliokuwa wakihoji mgombea mmoja baada ya mwingine, kuhusu kipengele cha elimu yake, ilionekana kuwa na utata lakini alijitetea na kuahidi kupeleka ushahidi,” kilisema chanzo chetu.

  Chanzo hicho, kilisema suala hilo lilizua mzozo mkali, huku Waziri Aboud akisisitiza kuwa hajawahi kufoji vyeti hata siku moja.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Waziri Aboud alikiri kutokea jambo hilo ndani ya kikao cha Kamati Kuu iliyokuwa ikihojiwa wagombea wote.

  “Ni kweli mmoja wa wajumbe wa kamati yetu aliibua hoja hii kwamba miaka niliyosoma pale Pemba shule hii ya Michakaeni haikuwepo, mie niliwaambia shule hiyo ilikuwepo na vyeti vyangu ni halali kabisa.

  “…kuanzia mwaka 1973, 1974 hadi 1975 nilisoma kidato cha kwanza hadi cha tatu, walimu wangu walionifundisha mpaka sasa wapo, wanafunzi niliosoma nao wapo ambao wanaweza kuwa mashahidi katika hili jamani,” alisema Waziri Aboud.

  Alisema hata mwalimu aliyesaini vyeti vya kuhitimu elimu hiyo, bado yupo hai na ndiye anaweza kutoa ushahidi na kumaliza utata huu.

  “Baada ya hoja hii kuendelea ndani ya kamati, iliamuliwa niandike barua Wizara ya Elimu Zanzibar, kuelezea suala zima ili kupata ukweli… napenda kukwambia kwamba kesho (leo), itatoa majibu ambayo yatamaliza utata huu,” alisema Waziri Aboud.

  “Ninashangaa sana kuhusiana na taarifa hizi, mimi nimesoma kuanzia darasa la kwanza na rekodi zote ziko pale na kuhitimu kidato cha tatu wakati huo, mie sioni tatizo ngoja tusubiri… nikija Dar es Salaam nitakuita uje uvione,” alisema Waziri Aboud.

  Alisema hadi juzi, wagombea wote wanakutana na kamati hiyo, hakupewa taarifa yoyote ya kupeleka vyeti ili vikaguliwe.

  Juzi Aboud alijikuta kwenye wakati mgumu, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Chakechake, Mwanajuma Majid kuhoji uhalali wa elimu yake.

  Alisema shule anayodai kusoma Aboud ya Michakaeni mwaka 1973/74 ndipo ilipoanza na kwamba ilianza kuwa sekondari mwaka 1978
  , jambo ambalo linapingana na maelezo yake.

  WAKATI huohuo, Balozi Ali Karume na mfanyabiashara maarufu Mohammed Raza wamekataa taarifa zilizoandikwa jana kwamba wameondolewa kwenye kinyang’anyiro cha urais wa Zanzibar.

  Wakizungumza katika mdahalo wa wagombea urais ndani ya CCM, ulioandaliwa na Vox Media kwa kushirikiana na Star Tv jana mjini Zanzibar, wana CCM hao walisema Kamati Kuu Maalumu iliyoketi juzi haikumchuja mtu yeyote.

  Walisisitiza kwamba wote 11 wanakwenda Dodoma kwenye vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ambavyo ndivyo vyenye uwezo wa kuchuja wagombea na kubakiza mmoja.

  Akisitiza hoja yake, Balozi Karume alisema chama kilishaweka utaratibu kwamba hakuna kupiga kura wala kutoa alama kwa wagombea, bali kinawajadili na kujaza mapendekezo kwenye fomu zao ambazo zinapelekwa Dodoma kwa ajili ya mjadala na mchujo.

  Kwa mantiki hiyo, alisema hakuna kigezo ambacho kamati hiyo ingekitumia kuchuja wagombea na kubakiza watano kama ilivyotangazwa; na kwamba kama kuna mtu alisambaza taarifa hizo, alikiuka utaratibu, na lazima ashughulikiwe.

  Raza naye alikataa dhana kuwa ni msindikizaji, akidai kwamba ana uwezo wa kuwa rais, na kwamba katika hatua waliyomo sasa, wagombea wote wana haki sawa mbele ya wanachama wenzao, bila kujali vigogo na viongozi wa serikali.

  Katika mdahalo huo wa kwanza kwenye historia ya siasa za Zanzibar, wagombea hao walijadili kwa kina masuala mbalimbali yanayohusu siasa na maslahi ya Zanzibar. Kipindi cha mdahalo huo kitarushwa wakati wowote wiki hii katika televisheni ya Star Tv.


  Source: Tanzania Daima.
   
 2. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli....
   
 3. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 521
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Wasimuonee Mzee wa watu, huyo kapiga kitabu, Vihiyo wapo serikali kuu bara, watu wanashahada na stashahada za kuchonga na wanapata mishahara na mafao kibao tu, mbona hao hamuwaandiki au mnawaogopa? acheni uonevu , mtu anakuwa waziri wakati elimu yake inamashaka, lol shame on u
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mmmh .................wanataka kusema hajafika hata form 3! mmmmh
   
 5. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kama kufoji kweli huyu Kiboko yani hata form three hakufika????bora hawa Mawaziri wetu wa huku bara wamefoji Phd but atleast wana first degree
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hivi ni kweli mtu aseme tu kuwa wewe haukusoma shule fulani bila kuwa na uhakika? Ukitaka kujua kama kweli mtu amesoma hasa digrii ya pili au ya tatu Mlimani tafuta 'thesis' au 'dissertation' yake kwenye library catalogue ya UDSM kwa kutumia jina lake akiwa kama mwandishi (author). Kama hakuna basi ujuwe huyo tapeli!!

  Kwa Aboud watafute records za hiyo shule na wanafunzi wake, matokeo ya mwaka husika. Wasiwatumie hao waalimu wake!
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hahaa, Dr. Karume naye amekuwa na mizengwe sasa??? kwani yeye alipata wapi PHD yake? tuanze sasa kuhoji!!!
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sio PhD tu First degree yake watu waihoji ameipata wapi??? Mie navyojua ana honorary doctorate na sio PhD degree. Hata wewe unaweza kupewa honorary doctorate na sio degree ya falsafa
   
Loading...