Eti kinadada mmezidi kuchambua

charger

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
2,320
1,369
Kuna suala lilizua mjadala mahali kwamba,woaji sikuhizi hawapatikani wengine wakasema no!waoaji wapo ila waolewaji wamekua na vigezo vingi mno kumchambua huyo muoaji ndio maana suala la relationship na relationship zinazoishia kwenye ndoa linaonekana kama gumu siku hizi au hata hizo ndoa hazidumu sijui mnaonaje hili??
 
Hili jambo halina kanuni kwa ninavyoona mimi, mtu atulie, amuombe Mungu wake, Wakati utaamua mambo!!!
 
Kuna suala lilizua mjadala mahali kwamba,woaji sikuhizi hawapatikani wengine wakasema no!waoaji wapo ila waolewaji wamekua na vigezo vingi mno kumchambua huyo muoaji ndio maana suala la relationship na relationship zinazoishia kwenye ndoa linaonekana kama gumu siku hizi au hata hizo ndoa hazidumu sijui mnaonaje hili??

Ni kweli, binadamu wa sasa wamekuwa too selective hasa pale anapopata multiple choices. Si mwanamke wala mwanaume.
Kuna kipindi fulani EATV muda kidogo uliopita, mtaalam mmoja (mwanamke) wa saikolojia na mahusiano alielezea upande wa wanawake wengi wa mijini kutaka kuolewa na mwanaume ambaye tayari ana maisha mazuri au ana future nzuri ya maisha hasa kiuchumi. Na wanaume wa aina hiyo wanahesabika kuliko wanaume wengine.
Mi nadhani ni mabadiliko ya kiuchumi duniani pia yanachangia ambapo wanawake wengi, mbali na suala la mapenzi ya dhati, pia wangependa kupata mwanaume ambaye atasaidia familia kiuchumi kwa kiasi kikubwa kuliko mwanaume ambaye anategemea pato la mwanamke zaidi.
 
Kumchambua huyo muoaji unamaanisha nini?

Mbona wanawake wengi sana siku hizi ni "niangusage"?
 
Umeonaaa eehhh
 
Achana na muonekano wa nje tu yapo pia mambo ya umri,ya kiuchumi kama vile kumiliki au kutomiliki gari,nyumba miradi mikubwa,elimu etc nafikiri umenisoma
Kumchambua huyo muoaji unamaanisha nini?

Mbona wanawake wengi sana siku hizi ni "niangusage"?
 
Ndoa ni jambo linaloweza kubadili uelekeo wa maisha yako kabisa,hivyo uchambuzi ni muhimu ili kupata mwenzi mwenye dira na uelekeo wako ili kuepusha janga la migongano huko mbeleni ambayo huishia separation na kukwaza familia wakati muda nao ushapotea hata kuanza upya haiwezekani tena.
 
ni kweli kabisa hapo umenena mimi mwenyewe nilikua natamani sana kuoa ila baada ya kuoa natamani niwe bachelor
Ndoa ni jambo linaloweza kubadili uelekeo wa maisha yako kabisa,hivyo uchambuzi ni muhimu ili kupata mwenzi mwenye dira na uelekeo wako ili kuepusha janga la migongano huko mbeleni ambayo huishia separation na kukwaza familia wakati muda nao ushapotea hata kuanza upya haiwezekani tena.
 
Kwahiyo unataka kubebana tu ili mradi??Bora kuchambuana kwa muda mrefu mkaingia kwenye isiyo na vikwazo vingi kuliko kubebana juu juu mkaishia kujuta na kuachana baada ya muda mfupi!
 
Tunaogopa magalasa mwenzangu lazima tuchambue ila ikija kuchambuliwa sisi tunajutaje?
 
Mbona umeelemea upande mmoja tu?
Kwani nyie wanaume hamchagui?
Katika kosa ambalo utajutia maisha yako yote ni kufunga ndoa na mtu ambae hakuwa chaguo lako.
Usiwe na pupa katika hilo.
 
Shida inakujaje? Mwanamke anakuwa na vigezo vyake kabla mchumba hajajitokeza, ugumu unakuja pale mwanamme anapokuja na mwanamke anapojaribu kufix vigezo vyake kwa mwenzi. Ni lazima kutakuwa na gap, mf utakuta jamaa yupo vizuri kimaisha lakinis iyo handsome au mfupi demu alikuwa anahitaji mtu mrefu, mrefu lakini hana mwili kidogo yaani shida tupu!
Kwa wanaume ndiyo shida atataka mtu aliyeenda shule halafu awe pini (mzuri ) ambapo tasfiri ya uzuri mpaka leo bado siyo uniform. Mwisho wanaume wengi huishia kuoa kazi badala ya wanawake ambao ni machaguo yao kwa asilimia fulani!
 
Anatafuta Mr right wake jameni ila mi naona kama wanaume ndio wanachambua sana!
 
wanawake hatuna choice sana kny hilo..since sie ndio tunaofuatwa na sio tunaotongoza mnh nahisi ni wanaume ndio wako selective na wana choice kushinda sisi.:A S 13::A S 13:
 
Inawezekana wadada ni wachambuaji maana hata mimi
lazima nichague na naamini hiyo ipo kwa wote.
Lakini wanaume hatuwaelewi wanataka nini, anaweza
kuwa na mpenzi miaka halafu ghafla anamuacha na ndani
ya muda mfupi anatangaza ndoa na mwingine!
Sasa kwa hili sijui nani mwenye choice zaidi.
 
Nilishashuhudia hilo maana lilimtokea jamaa yangu mmoja aisee utata mtupu yaani!
 
Back
Top Bottom