Eti katika mapenzi wanaume ni kama Masokwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti katika mapenzi wanaume ni kama Masokwe!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 22, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Katika utafiti uliofanywa na akina Kruger na wenzake kwa wanyama jamii ya Sokwe, ilibainika kwamba kulikuwa na vifo vingi vya Sokwe madume wenye umri wa miaka 13. Hali hii ilitokana na sababu kwamba, kwa kawaida katika umri huoa, Sokwe madume huwa wamefikia umri wa kupanda na kufanya mapenzi na hivyo huanza kushindana wenyewe kwa wenyewe wakigombea majike na hata kwa lengo la kudumisha hadhi yao miongoni mwa Sokwe wengine.

  Katika hatua hii Sokwe hao hufikia mahali pa kupigana na hata kuuana kwa lengo la kujipatia wapenzi na kudumisha hadhi zao. Hali hii haiko kwa sokwe peke yao, bali hata kwa wanyama wengine pamoja na ndege wa aina mbalimbali.

  Hata hivyo, pamoja na ukweli huo binadamu naye hajanusurika hata kidogo na purukushani za aina hiyo.
  Labda kinachomtofautisha binadamu na wanyama hao ni namna wanavyokabiliana na mashindano hayo. Lakini ukweli unabaki palepale kwamba, hata akichagua njia ya aina gani ili kushindana na binadamu wenzake, bado matokeo ya mwisho yatafanana na yale ya wanyama, yaani kifo.

  Imeonekana wazi kwamba binadamu wa kiume ndiye mwenye mwelekeo mkubwa wa kupenda purukushani na kuhatarisha maisha yake. Ingawa binadamu huyu wa kiume au mwanaume hahitaji kupigana mweleka na mwanaume mwenzake ili kumpata mwanamke, lakini harakati zake ni zaidi ya kupigana mweleka.

  Hata hivyo katika mazingira mengine, mieleka hupiganwa sana katika sura ya mieleka halisi au katika sura nyingine za ushindani wa kutafuta ushindi katika kumpata mwanamke. Wengi tunajua kuhusu habari za kuuawa kwa wanaume kutokana na vurugu za kugombea wanawake.

  Tabia hii ya wanaume ya kuhatarisha maisha si ya leo, bali ni ya tangu kale. Huenda huko nyuma baadhi ya wanaume walitumia silaha kwa lengo la kuwadhulumu ama kuwauwa wanaume wenzao ili hatimaye waweze kuwamiliki wanawake wanaowapenda. Kwa kawaida, wanaume hushindana wao kwa wao kwa lengo la kumiliki rasilimali na kuhifadhi au kudumisha hadhi na heshima yao ndani ya jamii wanamoishi.

  Huu ndio ukweli wenyewe ambao hautofautiani hata chembe na ule wa Sokwe. Ukweli ni kwamba mwanaume anapokuwa na uwezo wa kumiliki rasilimali adimu kama vile fedha na anapoweza kusimika kwa uhakika heshima na hadhi yake, ndani ya jamii iliyomzunguka, mambo hayo humpatia thamani kubwa na kumrahisishia kazi ya kumpata mwanamke anayemtaka.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  what????????
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  heee..
   
 4. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Haya bwana
   
 5. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Thanks mkuu for sharing
   
 6. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kwani umesahau sisi ni masokwe tulioendelea?
   
 7. G_crisis

  G_crisis JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 715
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Umenifurahisha kwa kutumia lugha ya taifa
   
 8. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  chagua mji!!!!!!!!!!!!
   
Loading...