Eti hizi ndio sifa 5 zilimfanya Membe apewe ajira TISS

Usishangae pia na sifa nyingine ya nafasi hiyo ilikuwa ni weupe wake. Bongo hakuna kinachoshindikana.
 
Ujasusi wake uliisaidiaje bongo? Kuondoa umaskini, ufisadi, ujinga, ushamba wa viongozi, ulimbukeni wa viongozi na maradhi?

Mi sioni faida yake! Mi naona ni wale wale tu ukoo wa panya! Sorry guys.
Huna haja ya kusema sorry, ni maoni yako, yaheshimiwe.
Kujua ujasusi wake ulisaidiaje bongo, ishu ya ujasusi hapa kwetu waijuao ni wachache huku sie twapata fununu tu.

Ila kwa hizo fununu tupatazo Membe amekua na mchango mkubwa hasa alipokua waziri kwenye serikali ya Jakaya.
Tanzania iliheshimika kimataifa.

RIP kamanda Membe.
 
Dogo Kama wewe na yeye hakuona amejidhalilisha basi hakuwa na akili kabisa za kijasusi. Kuna kushindwa na kudhalilika. Kifupi ni kuwa katika medani ya Siasa hakuwa na mvuto.alikuwa mweupe sana kichwani.
Kua na nidhamu kijana sio kila mtu ni dogo.

Hakujidhalilisha, mpama pale alipofikia alikua ni giant wa siasa nchini.
Ni maamuzi mazito mno kuyachukua kwa wakati ule na mtu kama yeye na kwa heshima aliyokua nayo kwenye chama tawala.
Ni wachache wenye huo uthubutu.
 
Usishangae pia na sifa nyingine ya nafasi hiyo ilikuwa ni weupe wake. Bongo hakuna kinachoshindikana.

Kuna huo uwezekano.

Haikuwa rasmi lakini nashuku hii ilikuwa moja ya sifa za kuingia kwenye baadhi ya vyombo vyetu vya dola.

Hasa majeshi yetu.

With some exceptions of course.
 
Baba yake alikuwa.....muwindaji mkali sana alimfundisha sana matumizi ya silaha za kuwindia ndio alipopata uwezo shabaha ....na ujasiri
 
R.I.P. MEMBE wazuri hawafi
 
Sifa za kuajiriwa TISS ni zipi ili tulinganishe na tuone kama alistahili au alipendelewa
Vinginevyo ungekaa kimya ungeonekana mtu mwenye akili kuliko huku kubwabwaja unakofanya hapa
 

Sidhani ushawishi unaongelewa hapa ni ushawishi wa kisiasa, ni deception kwenye field work. Kazi ya ujasusi ni science ya usaliti. twisting realities upate unachokitaka.
Unaweza kuwa mzuri huko lakini kwenye siasa ukawa 0

Kuna sababu why mamlaka zilimchagua
 
Dogo nikuambie kitu? Membe hajawahi kuwa giant wa kisiasa hapa Tanzania.
 
Mamlaka zetu zinakuchagua sababu wewe ni mwanaccm mzuri na una mtu wa kukuweka pale ulipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…