Abbasfarudume
JF-Expert Member
- Feb 14, 2017
- 1,625
- 1,326
Wakuu habari za wakati huu nafikili kichwa cha habari hapo juu kinajieleza chenyewe, ni hivi karibuni nilitembelea kijijini njopeka ipo mkoa wa pwani kusini mwa nchi yetu, nilienda kwa matembezi maalum, nilipofika kule kulikuwa na msiba maeneo hayo huo msiba ni mtu nzima wa makamo (mzee) alifariki sasa katika kuwepo kwangu kwenye ule msiba, kwa sababu ipi nilikuwa pale kwenye ule msiba kwanza yule mwenyeji wangu nilioenda kwake na huo msiba ulikuwa upo pale pale kwa Jirani yao sasa yule mwenyeji wangu akawa anaambiwa na rafiki yake jirani yake kwa maelezo zaidi na nukuu "marehemu sijui alikuwa anajua atakufa maanake alijinunulia sanda mwenyewe pamoja na mkeka, akawaonyesha ndugu zake kabla hajafa na wakati huo alikuwa na afya njema tu, nikifa sanda yangu na mkeka ni hivi hapa nimeviweka chumbani sehemu... Fulani kwa hiyo nikifa msipate tabu ya sanda" mwisho wa kunukuu sasa hapo ndio nimekaa na kutafakali na kujiuliza maswali chungu nzima kichwani kwangu Je ni sawa kabla hujafa kujinunulia sanda dukani na mkeka siku ukifa ndugu zako wasiangaike kukununulia Sanda??!