Nimesoma gazeti moja linauliza hivi pesa hutokaje serikalini kwenda kwa wananchi? na nikadhani tunaweza kujadili sote
Binafsi kwa uelewa wangu pesa huwa inazunguka na kuzunguka kwa pesa maana yake ni kutoka sehemu moja ikapita kule na kule na kurudi sehemu hiyo hiyo ilipoanzia huo ndio mzunguko kwa lugha ya ki layman.
Sasa mizunguko ya pesa huwa ina njia zake zinazopitisha mizunguko ya pesa. Pesa hizi zikipita kwenye mizunguko inayogusa watu wengi basi kila pesa zinakopita wale ziliowapitia huwaachia neema wale watu wanaokuwa kwenye sehemu ambazo pesa hazipiti basi hawa hulia njaa.
Chukua mfano wa baba mwenye familia akiwa na kipato, akiamua kutumia pesa nyingi kwenye pombe basi baba huyu hujenga jina baa na kuonekana kwa walevi kama mtu anayewapa neema wadau walioko kwenye sekita ya mabaa lakini yawezekana nyumbani watoto wanalia njaa na maendeleo binafsi hakuna lolote.
Yupo baba anayeamua kuweka kipaumbele chake kuwa matumizi ndani ya familia, mshahara wake wote watakula vizuri, watavaa vizuri watajirusha kadiri wawezavyo lakini hafanyi uwekezaji wa kimaendeleo au kutembelea sehemu kama mabaa. Huyu naye familia yake itamuona baba bora kwa raha za mda mfupi huku kimaendeleo akibaki palepale, anastaafu hana nyumba wala biashara fedha yote alikuwa anakula.
Yupo baba ambaye wakati anasoma chuo alikuwa anapewa hela ya kula hali anaweka pesa yote ili aje kufanya kitu cha maendeleo, amemaliza chuo kaajiriwa pesa yote kawekeza kwenye kujenga maghorofa huku watoto wakiugua kwashiakoo na watu wazima wakiwa na vidonda vya tumbo.
Serikali ni mfano wa baba katika familia, pesa yote ni mali ya serikali, mizunguko ya pesa huanzia kwake na kumalizikia kwake.
Swali la msingi ni serikali inayokuwa madarakani ni ya aina gani ndio maisha wanayoishi wananchi wake.
Kama serikali inayokuwa madarakani ni sawa na baba mlevi anayepeleka pesa yote kwenye baa ambapo kama vile vitendo vya ufisadi, mradi unagharimu bei mara mbili ya gharama halisi ni wazi walevi ambao tunaweza kuwaita mafisadi ndio wataiona serikali hiyo ya maana sana huku wananchi wakilia na nchi kutokupiga hatua kimiundombinu.
Kama serikali inayokuwa madarakani inaamua kutumia fedha tu na wanafamilia kula vizuri, kuvaa vizuri basi bila shaka wananchi wake wataiona serikali hiyo ya maana sana kwa maana kila mwananchi anapata mahitaji yake kwa wepesi.
Na kama serikali itaamua kuwa baba anayeshinda njaa na watoto kushinda njaa ilimradi amejenga jina mtaani kuwa ana ghorofa ni wazi kwa nje wataonekana familia yenye uwezo lakini wakiishi maisha ya umasikini.
Swali linabaki kuwa je maendeleo ni nini? au serikali bora ni ipi?
kwa mtizamo wangu maendeleo ni lazima yapimwe kwa kutazama living standard ya watu. Living standard ya watu inapimwa kutokana na purchasing power kwa maana kila kitu kinategemea pesa. Uko na pesa kiasi gani mfukoni ndiyo kipimo cha utaishi maisha gani.
Kama layman ambaye si mchumi kama ningekuwa nimepewa jukumu la kuinua uchumi wa watanzania basi ningeweka vipaumbele vifuatavyo
1. Kipaumbele cha kwanza kingekuwa kuinua kipato cha watanzania.
2. Kipaumbele cha pili kingekuwa kila mtanzania ni lazima alipe kodi
3. Kipaumbele cha tatu kingekuwa ujenzi wa miundombinu
4. Huduma muhimu za kijamii
5. Mambo yote ya kijamii
Kwa kuwa swali la msingi limeuliza kwa kutegemea malalamiko ya wananchi na majibu ya wenyewe basi hatuna budi kujikita huko.
Binafsi ninadhani serikali imeweka kipimo cha maendeleo kuwa
1. Ujenzi wa miradi ya maendeleo na matokeo yake ni fedha zinazokwenda kwenye miradi hii hazigusi jamii ya watanzania walio wengi.
2. Serikali imedhibiti fedha nyingi ambazo zilikuwa zinaingia kwenye jamii kupitia sekita ambazo tunaweza kusema ni za kilevi.
3. Serikali haijapandisha mishahara kwa miaka
4 Mfululizo huku rundo la kodi likiongezeka hivyo hata kipato ambacho kilikuwa kinabaki kwa watu kufanya manunuzi yao kimepungua zaidi.
Principaly binafsi siikubali sana falsafa ya kiuchumi ya awamu ya Tano. ninaiona kama falsafa ya kutengeneza uchumi wa "machinga complex" yaani unajenga uchumi wa miundombinu huku ukiua purchasing power ambayo matokeo yake ni kuwa na miundo mbinu bora kama ya jengo la soko la machinga complex huku miundombinu hiyo ikishindwa kufanya biashara.
Binafsi nakubali falsafa ya wape watu pesa nyingi lakini walipishe kodi ya kutosha na wape majukumu ya kutosha. yaani kupata pesa iwe ni rahisi lakini kuishi pia kunahitaji pesa nyingi hivyo pesa anazopata ntu hazikai na hiyo ni kuongeza kasi ya mzunguko wa pesa ili transactions ziwe nyingi sana kuongeza kodi na ajira na hapa nina uhakika ujenzi wa miundombinu kama kipaumbele cha tatu baada ya kukusanya kodi naona kitafanikiwa.