Eti, chuki nichukie moyo wangu niachie...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti, chuki nichukie moyo wangu niachie...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 13, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Kila mtu ni mbaya kwako, kila mtu anakuchukia, wewe tu, kila mtu hakutendei haki, kila mtu ana kasoro?

  Je wewe ndivyo unavyoishi hivi?
  Kama jibu ni ndiyo au kama una mtu wako wa karibu ambaye anaishi katika mtindo huu wa maisha, unapaswa kujua kwamba, una mtu ambaye ana matatizo makubwa. Mtu yeyota ambaye anapenda kusema kwamba, kila mtu anamchukia au kila mtu hamwelewi, basi jua kwamba huyo ni mtu ambaye kimsingi ana matatizo makubwa sana.

  Kwa nini?

  Haiwezekani kila mtu akawa kama mwingine, yaani akikuchukia huyu na yule ni lazima atakuchukia, ni lazima hatakutendea haki na mengine ya aina hiyo. Kwa nini sasa wote wawe na tabia za aina moja, yaani wafikie kukuchukia?


  Kwa kuwa watu hawafanani kitabia, kimwenendo na kimtazamo, ni wazi ukiona wote wanakuchukia wewe, tatizo haliko kwao, kwa sababu hawawezi wote kuwa na mkabala wa aina moja. Ina maana kwamba wewe ndiye ambaye hujipendi na kutojipenda kwako kunaonekana kwa watu hao. Tunaposhindwa kujipenda, hasira dhidi yetu huwa tunazitolea kwa watu waliotuzunguka. Kwa hiyo kama unahisi kwamba watu wanakuchukia, jitahidi kujiuliza kuhusu jambo hilo. Ni wazi haliwezi kuwa jambo la kweli hata kidogo. Kama ni kuchukiwa, hivi inawezekana ukachukiwa na kila mtu kweli?

  Ukichunguza ni wazi utagundua kwamba wenye tatizo sio hao watu. Mwenye tatizo ni wewe na watu hao ni kioo chako kwa tabia yako. Kama kila unakopita, iwe ni kazini au popote unajikuta ukiondoka umeacha watu wengi wakiwa wanakuchukia badala ya kukupenda, ujue kwamba wewe ndie mwenye tatizo, wewe ndio mwenye kasoro. Haiwezekani watu wakae kikao cha kukuchukia, bali watu wanaweza kukerwa na kutojiamini kwako au vitendo vyako hadi ikaonekana kama wamekula njama kukuchukia.

  Kwa tabia zako, wanajikuta wakikujadili na kuambiana ‘humjui, ndivyo alivyo huyo' Basi wanakuwa wameunda aina ya timu ya kukuchukia. Kumbuka tu kwamba kila binadamu anapenda kuona anapendwa na kuheshimiwa, ingawa ni vitu visivyo na maana sana kwake. Na kama unashindwa kumfanyia hivyo, anaingia mahali ambapo anaona huenda kuwa karibu na wewe ni hatari au haipendezi. Kama hii ndio tabia yako, utamfanya kila mmoja ahisi kukereka kuwa karibu na wewe.

  Hapo ndipo kuchukiwa kunapoanza. Naomba nikwambie ukweli kwamba usije ukasema unachukiwa na watu fulani au kwamba watu fulani hawakupendi. Ukisema hivyo, watu wanaojua tabia za binadamu, watajua kwamba wewe ni mkorofi sana. Ukiona mtu anasema jirani zake, watumishi wenzake, wanafunzi wenzake, ndugu zake, wanaye, wazazi wake au kundi fulani la watu wanamchukia, basi kwa kiwango kikubwa mtu huyo ni mkorofi. Tafadhali kama imetokea ukahisi kwamba watu fulani wanakuchukia, au hawakupendi inabidi uanze kujiuliza bila kujipendelea kama wewe sio chanzo cha chuki hizo.
   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Nadhani kwa wale wanaojua nguvu ya mawazo wanaweza kujua ni namna gani mawazo yanaweza yakaathiri mazingira yako ya nje mpaka kuwavuta wale unaofanana nao kifikra!
   
 3. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii thread inafundisha mengi cha kwanza binadamu unatakiwa ujiamini kama hujiamini utaona kila kitu kipo opposite na wewe....Hao wanao sema wanachukiwa wangekuwa wanajipenda wao kwanza wasingesema wanachukiwa.

  Out of thread; Mtambuzi huyu babe naweza kumpata wapi mana ana vutia vutia, I wish I have her now, b-side me.
  [​IMG]
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi, Kwanini kila nikifanikiwa ninakuwa nachukiwa zaidi......
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa mkuu,nakubaliana na wewe. Ila naomba nikuulize Mtambuzi leo hii wewe ukiachana na Mama Ngina(siombei hivyo,usije ning'oa meno bureee...lol), halafu ukapata kimwana mwingine baada ya muda ukaachana nae mara tena ukavuta zigo la haja nae tena mkatemana muda si mwingi ukamleta mwingine hamjakaa sawa ukagundua umelamba galasha,ukampiga kibuti.....ukabeba tena mwingine mnaishi nae lakini kila kukicha matatizo hayaishi!!!! Hebu kiukweli kabisa utawezaje kuwa convince ndugu/jamaa na marafiki kuwa wewe ni msafi kabisaaa tatizo huwa unalambaga magalasha???!!!!

  Je, yawezekana kweli wewe ni msafi ila huwa na bahati mbaya??!!??:rolleyez::rolleyez::rolleyez::rolleyez::rolleyez::rolleyez::rolleyez::rolleyez::rolleyez::rolleyez::rolleyez:

  My point of view; huwezi kuchukiwa na kila unaekutana nae kama wewe huna mapungufu yasiovumilika(kila binadamu ana mapungufu yake) tatizo litakua kwako wewe,jitazame/jichunguze na kujitathmini na sio kunyooshea vidole watu kila kukicha oooh hawa hawanipendi, mara wale wananionea wivu blah blah blah kibao bila kujiangalia/kujiuliza kama mwenye tatizo ni wewe.
   
 6. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Haswaa ,hii mada imekuja wakati muafaka halafu Mtambuzi ingekuwa picha ya mwanaume ingependeza
   
 7. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Unachukiwa na nani MadameX???baadhi ya watu au jamii nzima iliyokuzunguka???!!!??
  Kuna watu wana WIVU(huu ni ugonjwa mbaya sana looh) kupita maelezo hata kama yeye amekuzidi yaani ana maendeleo zaidi yako lakini hata akikuona umenunua kijiko roho inamuuma, na watu wa namna hii hatuwezi kuwabadilisha. Mimi nna hili tatizo mara nyingi nilikua nikijiuliza hivi mtu ananionea wivu kwaajili ya nini maana nikimuangalia huyo mtu anakua amenizidi kwa maendeleo sasa ni kitu gani kinamfanya anionee wivu.......nikagundua kuwa mimi muda wote niko happy,sasa nafikiri huwa wanajiuliza kwanini mimi ni mwenye furaha na amani muda wote wakati nna matatizo lukuki na wao wana kila kitu lakini they are not happy!!! Nilipogundua hilo nikadharau na kuzidi kusonga mbele,na hii ndio dawa ya wenye wivu yaani wewe endelea na maisha yako kama vile hawa exist!! Na kikubwa usishindane, ishi maisha yako....hii ni bakora tosha.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...