Kenya kupitia tume yao ya uchaguzi IEBC wameionyesha dunia kumbe Waafrika tunaweza kuendesha uchaguzi wetu ulio huru wa haki na uwazi (transparent election) bila kuingiliwa na mataifa ya nje.
CCM na tume yetu ya uchaguzi NEC wana mengi ya kujifunza kutoka Kenya, waache kulialia kuwa Odinga ameibiwa kura, kwa vile hadi sasa hakuna aliye na ushahidi wa wizi huo.
Nani asiyejua CCM ni mabigwa wa wizi wa kura wamejaribu kupeleka mbinu hizo Kenya wamegonga mwamba ndipo wanalalamika.
CCM wanatoa wapi upendo kwa mgombea wa upinzani Raila Odinga, mbona 2015 wakati Lowassa akidai kura zimedukuliwa hamkujitokeza kama mnavyojitokeza leo kuitaka NEC itumie fomu kutoka vituoni kujumlisha kura, mbona hamkufanya hivyo kwa Maalimu Seifu aliyedai kashinda na matokeo yake kufutwa. Acheni unafiki.
Odinga kwa mwamvuli wa NASA alipewa kila alichoomba,
Aliomba tume huru akapewa IEBC,
Aliomba mikutano huru hakubughudhiwa na polisi yeyote,
Alimkosoa rais Uhuru kwa kadri alivyopenda hakukamatwa na mtu.
Aliomba wafungwa waruhusiwe kupiga kura akapewa.
Aliomba wakenya waishio nje wapige kura akapewa.
Aliomba kura zihesabiwe upya kwa kutumia fomu 34A 34B IEBC wakarudia.
Sasa CCM mnavyolalamikia matokeo mlitaka rafiki yenu ashinde kwa kura za wizi?
Kenya wameendesha uchaguzi wao kwa uhuru na haki na kwa uwazi wa hali ya juu tofauti na sisi ambapo matokeo huwa siri hadi siku ya mwisho.
Leo vyama vya upinzani vimezuiwa kufanya mikutano ya kisiasa wakati CCM ikiendelea na mikutano kama kawaida, sipati picha itakuwaje wakati wa uchaguzi.
Hongera Uhuru, hongera IEBC na hongera wakenya wote.