Eti Bunge limeahirishwa kwa sababu ya Ukata? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Bunge limeahirishwa kwa sababu ya Ukata?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zwangedaba, Feb 13, 2009.

 1. Zwangedaba

  Zwangedaba Member

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 1, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Wana JF kuna tetesi nimezipata mtaani kwetu, Eti bunge limeahirishwa kwa kutokana na ukata unaolikabili hakuna fedha za marupurupukwa wabunge....
  Kuna aliyesikia hilo pia au news yoyote kuhusu hilo?
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,186
  Trophy Points: 280
  Kwani wana jipya gani?
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Yawezekana kabisa kwenye nchi itegemeayo marupurupu ili kujitungia sheria kupitia moja ya mihimili yake na katika kutekeleza sheria hizo kupitia moja ya mihimili yake mitatu.

  Hope hili halijatokea.... !!!
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama ni kweli sioni ajabu maana CCM imeshakwangua hazina yote au ni mkakati wa kuwabana wabunge mpaka wasikie njaa ili kuweza kuwapiga bakora kiulaini.

  Unajua serikali imeshaona kitita wanacholipwa wabunge ni kikubwa na namna uchumi wa dunia unavyokwenda kuna hatari kukafilisika kabisa ,sasa kupunguza kitita hicho ni mbinde na aidha serikali inaogopa au inaona si adabu nzuri kuwapunguzia posho na mishahara wabunge hivyo ni bora waahirishe ,pengine mpaka itakapotolewa tangazo rasmi.

  Kwa upande wangu naona serikali wangekaa na bunge ili kujadiliana juu ya ukata huo aiddha bila ya kuogopana waelezane ukweli na katika kuelezana ukweli moja ni kubana matumizi ya bunge (Bajeti ya bunge fedha yake imeenda wapi).

  Na katika kushauriana huko moja ya njia ambazo zitamuathiri kila mmoja wao ni kupunguza mishahara kwa asilimia 25 halikadhalika na posho ipunguzwe kwa asilimia 50.
  vile vile Serikali ipunguze mawaziri wa serikali yake ni wengi mno ,maana idadi ya mawaziri inashinda idadi ya mikoa tuliyonayo.

  Hivi sasa taasisi mbalimbali duniani zinapunguza wafanyakazi wake international ,hivyo hata na sisi tuaweza kujiunga nao na kupunguza idadi ya wafanyakazi katika balozi zetu aidha kuziungasha Balozi iwe balozi anahudumia nchi nyingi ,kwa mfano zile nchi ambazo raia anaweza kwenda na kutembelea nchi jirani bila ya kuulizwa pasi naona nchi hizi zingekuwa na balozi mmoja au wawili tu ingetosha kabisa.
  Kwa ufupi kunahitajika punguzo katika serikali ikichangia iwe ya kupunguza wafanyakazi na pia kupunguza mishahara yao.
   
 5. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ......mh, kama ni kweli basi sisahihi kuahirisha bunge kwani hata wanafunzi huwa wanakopwa na serikari na baada ya muda fulani wanalipwa pesa zao japo sometime mpaka wagome. Waalimu wamekuwa wakikopwa na serikali mpaka kipindi cha mwaka mzima sasa wao wameshindwa kuvumilia hata week moja. Itadhihilish kuwa lengo mahusisi ni pesa na sio wananchi.

  Hata hivyo serikari haitakiwi kusita kupunguza marupurupu ya wabunge kama hali imesha kuwa mbaya. Naungana na mdau hapo juu, serikari za wenzetu zimeanza kupunguza mishahara ya vigogo ili kuweka mambo sawa. Hata hivyo natoa angalizo mishahara ya walalahoi haitakiwi kupunguzwa bali kuendelea kupanda. Wasije wakataka usawa katika swala la kupunguzwa mishahara, kwani wao wapo mbali sana kimapato.
   
 6. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Halafu kuna mpango wa kuongeza majimbo ya uchanguzi kama 100 hivi 2010. Sasa sijui itakuwaje..
   
 7. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ulitaka wakae mwaka mzima ndio ujue kuna fedha. Kila kikao kikikaa huwa kuna mwisho kinaahirishwa, nadhani kwa hili ni tetesi kama ulivyoandika. Tangu mwanzo ilitangazwa lini Bunge litaanza na siku gani litaahirishwa, kama lingeahirishwa nyuma ya tarehe iliyopangwa hapo ndio tungesema kuna mgogoro. Kikao cha bajeti ndio huwa kirefu.
   
 8. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Iwapo tunataka kujiweka katika hali ya kutotambulika duniani basi na tutekeleze huo ushauri wako. Kwa taarifa yako hivi sasa idadi ya Balozi zetu ni chache sana kulinganishja na haja hasa ya kuitambulisha Tanzania.
  Kupunguza Balozi haitosaidia kitu kwani Taifa linahitaji huduma za Kibalozi hivi sasa kuliko wakati wa nyuma. Tuna vivutio vingi kwa Utalii na biashara lakini tunashindwa na mbinu za kuvitangaza huko nje kutokana na ukwasi tulionao. Tuna hisia kuwa fedha nyingi zinatumika kwenye mabalozi yetu lakini ukweli ni kwamba kwa taarifa zitokazo balozini kwetu hali ya kifedha ni ngumu huko na wanshindwa kutekeleza kazi zao. Hadi sasa mgawanyiko wa balozi zetu hautoshelezi mahitaji halisi ya huduma zinzokusudiwa kuwepo kwa balozi.
  Fikira kwamba tunaweza kurundika kazi za kundi la nchi kwenye nchi moja haiwezi kusaidia kwani kuna nchi kuihudumia kibalozi ni kazi ya kutosha , sasa kuunganisha kundi la nchi zaidi ya kumi kwa balozi moja haifikiriki. Kwa mfano tuunganishe nchi za Kiarabu 10 wakati kila nchi ina uhusiano tofauti na nyengine na kila nchi ina umuhimu tofauti kimahusiano, balozi zetu zitafanya nini?
  Nafikiri matokeo kama haya ya kuahirishwa kwa Bunge ni sehemu ya kujitowa muhanga katika hali inayotukabili na Balozi zetu kule nje zinafanya sehemu yao ya kujitowa muhanga. Upo wakati mambo hayakuwa mabaya hivi na tutegemee kuwa mambo yatabadilika baada ya muda.
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  sio kweli - uzushi mtupu
   
 10. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  ... amesikia mtaani, kwa hiyo tuishia hapo tu:confused:au wabunge walitaka siku ziongezeke ili wapate zaidi?
   
 11. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Zwangedaba,

  Mbona ungetumia muda kidogo tu ku search kwenye google ungepata ukweli mzima? Vikao vya bunge vinatangazwa mapema sana; wanapotangaza kunakuwa na siku ya kuanza na kumaliza. Kikao kilichofungwa kimeanza na kuisha kwa wakati uliokuwa umepangwa.
   
 12. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Sio uzushi ni kweli, Spika Sitta amethibitisha hilo.
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Aliitisha press conference siku moja baada ya kikao na kueleza kwua wamelazimika kukatisha mkutano kwa sababu ya ukata uliopo serikalini kutokana na global financial crisis
   
 14. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Hawa wamekwepa kujadiliwa kwa hoja moto moto zilizokuwa zimejitokeza ikiwamo ya masha, richmond etc... hakuna ukata hapa. Ni upuuzi mtupu wana buy time.
   
 15. M

  Mwanagenzi JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2009
  Joined: Sep 11, 2006
  Messages: 690
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Waliogopa hoja muhimu kujadiliwa...na hata siku ile serikali nzima ilipoingia mitini wakidai wana kikao cha baraza la mawaziri, kiasi cha kufanya bunge kuahirishwa, si bahati mbaya, waliamua kupunguza muda wa kubanwa bungeni...wizi mtupu!
   
Loading...