Eti bei ya mafuta ya taa iwe sawa na petrol

Alisema wafanyabishara wamekuwa wakipata faida kubwa katika mafuta wanayoyauza baada ya kuyachakachua kutokana na mafuta ya taa kutozwa kodi ya shilingi 53 kwa lita na dizeli na petroli kutozwa shilingi 490 kwa lita pindi wanapoyaingiza. http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=16637
Hii ni aina ya 'Upumbavu' iliyowagubika viongozi wetu wengi. Yani haya ndiyo yanapelekea uvunjivu wa sheria kila mara na tunatafuta vijisababu vya 'kijinga' na kuzidi kuwatwisha walalahoi wengi mzigo wa ongezeko la gharama za maisha.

Yani mnashindwa kuwadhibiti wachache mnaamua mzigo wote kuubwaga kwa walalahoi walio wengi?

Inakera SANA
 
Ujue kuwa wao hawatumii mafuta hayo ya taa, bali umeme, gesi na nishati zinginezo hivyo suala hilo haliwaumizi sana! Na hatakama wanatumia nishati hii ya mafuta ya taa, wana uwezo wa kutosha wa kumudu!...Kilichofanyika ni namna ya kujionyesha kwamba WAPO na wanatenda kazi, hasa ukizingatia aibu iliyojitokeza kwa mwenye nchi majuzi!Wananchi hawana mtetezi!.


exactly! aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Lakini wanapaswa kujua kuwa wamepewa dhamana (madaraka) kwa ajili ya hawa walalahoi.

Wote mpo sawa, ila kuna alternatives nyingine nyingi tu ambazo walalahoi wanaweza kukimbilia. Crank Box ni bidhaa moja wapo ambayo itawafaa sana walala hoi wa TZ. Angalia tangazo lake kwenye jukwaa la matangazo madogo madogo. Bidhaa hii haina matumizi mengine zaidi ya nguvu zako mwenyewe. Si ndio mtaji wa maskini?

Mafuta ya taa yana gharama zaidi ya kununua tu. Yana wa-cost raia matatizo mengi tu, ikiwa ni pamoja na moto, kiafya n.k. Kwa hiyo mi nashauri wana JF pamoja na jamii ya kitanzania kwa ujumla wasinung'unike sana. Kwani mkombozi wao yupo!!
 
Hapo ndy mtajua jinsi watendaji wenu walivyo WAPUMBAVU na wafinyu wa fikra!!
wanashindwa kukdhibiti wizi kisha kwa kuogopa magari yao yasiharibike basi wanapandisha bei ya mafuta ya
taa bila kujali kuwa watoto wa wapiga kura wao wanategemea mafuta ya taa kujisomea!!

Well said amoeba!!
Crank Box can be used for studying. Wasaidieni ndugu zenu walala hoi wapate walau crank box moja ili watoto wao wapate kusoma bila kuumiza kichwa bei ya mafuta ya taa.
CRANK BOX NDIO MKOMBOZI WETU SASA!!
 
Back
Top Bottom