Eti bei ya mafuta ya taa iwe sawa na petrol

Nemesis

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
5,460
4,359
:A S-confused1:

Inasikitisha, inapotokea mamlaka zinashindwa kuthibiti wezi, wahuni na wahujumu uchumu na kuwaongezea gharama wananchi. EWURA inapendekeza Serikali iongeze kodi ya mafuta ya taa toka sh 53 kwa lita hadi 490 kwa lita ili bei yake ilingane na petrol na dizeli.

Petrol na dizeli zinatumika kuendeshea mitambo, magari na vitu vingine vinavyoingiza fedha nyingi tena vinavyotumiwa na watu wenye pesa (matajiri). Mafuta ya taa yanatumiwa zaidi majumbani tena na watu maskini au kipato cha chini. Watu wengi hawana umeme manyumbani iwe kwa kukosa uwezo au TANESCO hawajafikisha huduma.

Uzalishaji unaofanywa na mtu anapotumia mafuta ya taa nyumbani ni hakuna au mdogo haiwezekani ukalipa gharama ya kulingana na petrol au dizeli. Iweje EWURA wanatoa pendekezo hili? kama wameshindwa kazi si waondoke?

EWURA yaunga mkono bei ya mafuta ya taa kuwa kama dizeli, petrol

na Janet Josiah

MAMLAKA ya Udhibiti wa Matumizi ya Nishati na Maji (EWURA), imeunga mkono, mapendekezo ya baadhi ya wadau kutaka kupandishwa kodi mafuta ya taa kuwa sawa na ya diseli na petroli. Akizungumza na Tanzania Daima, Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Haruna Masebu, alisema endapo kodi hizo zitakuwa sawa na zingine hatua hiyo itakuwa suluhisho kuondoa tatizo la uchachushaji mafuta.

Mapendekezo ya EWURA na wadau wengine, yamekuja siku chache baada ya tukio la magari matano ya Rais Jakaya Kikwete kujazwa mafuta machafu na kugoma kuwaka wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro.

Masebu alisema ingawa bajeti ya mwaka wa fedha ya 2010/2011, haikuzungumzia suala la mafuta ya taa kupandishwa kodi kutokana na nishati hiyo kutumiwa na watu wa hali ya chini, alisema tatizo hilo halitaweza kuisha kwa kuwa ndilo linalowapa faida wafanyabishara wa mafuta.

Alisema wafanyabishara wamekuwa wakipata faida kubwa katika mafuta wanayoyauza baada ya kuyachakachua kutokana na mafuta ya taa kutozwa kodi ya shilingi 53 kwa lita na dizeli na petroli kutozwa shilingi 490 kwa lita pindi wanapoyaingiza.

Masebu alisema baada ya kufanya zoezi la kuyachakachua na kuanza kuyauza hupata faida ya shilingi 450, hali ambayo alisema endapo serikali haitachukua hatua za kuyapandishia kodi, hali hiyo itaendelea kama ilivyo. Alisema wao kama EWURA hawana uwezo wa kupandisha nishati hiyo kodi bali uwezo huo upo katika Wizara ya Fedha na Uchumi.

Masebu alisema kwa kuwa tatizo hilo ni kubwa na kwamba haliwezi kuisha mara moja kama nishati hiyo haitapandishiwa kodi, EWURA imejipanga kutumia njia za aina mbili ili kupunguza tatizo hilo mojawapo ikiwamo ya kuyawekea mafuta ya taa rangi ambayo itayatofautisha na mafuta ya dizeli na petroli hata kama yatachachuliwa yatagungulika mara moja.

Alisema njia nyingine ambayo EWURA itatumia kukabiliana na tatizo hilo, tayari imeagiza magari maalum yenye maabara “Mobile Laboratory” yatayoingia mwezi Agosti, ambayo yatazunguka nchi nzima kukagua na kuwachukulia hatua wafanyabiasha watakaokuwa wamefanya hivyo.

Alipoulizwa endapo nishati hiyo itapanda, haoni kama itawaumiza watu wa hali ya chini, alijibu kwamba kama serikali ikifikia muafaka wa kupadisha kodi, wananchi wa hali ya chini watatafutiwa nishati mbadala ya mafuta ya taa ili kukidhi mahitaji yao kama ilivyo katika nchi nyingine.

Wakati huo huo, Masebu alisema kuwa tayari mamlaka hiyo imeshakamilisha ripoti ya uchunguzi wa kituo cha mafuta cha mjini Moshi ambacho kiliyaweka mafuta machafu kwenye magari matano yaliyokuwa katika msafara wa Rais Kikwete.

Alisema kinachosubiwa sasa ni maelezo ya mmiliki wa kituo hicho ili ripoti hiyo itolewe mbele ya vyombo vya habari kesho kutwa (Ijumaa).

Source EWURA yaunga mkono bei ya mafuta ya taa kuwa kama dizeli, petrol
 
Ufinyu wa fikira wa hawa wanaotakiwa kufikiri, hupelekea kwenye majibu rahisi, "Muumize mtumiaji wa mwisho".

Tatizo linalotokana na kuchanganya mafuta ni kuruhusu kuwa na vituo vingi kama uyoga wakati idadi ya walaji ni constant. Nina maana kuwa kuna idadi inayoeleweka ya magari katika kila eneo, hamna sababu ya kuwa na kituo zaidi ya kimoja ndani ya kilometa 5.

Kama wangeweza kutekeleza hilo, ingekuwa ni rahisi kudhibiti wanaochanganya mafuta kuliko hili swala wanaloliita biashara huria ambayo ni kero na kero na kero kila kukicha.
 
Ujue kuwa wao hawatumii mafuta hayo ya taa, bali umeme, gesi na nishati zinginezo hivyo suala hilo haliwaumizi sana! Na hatakama wanatumia nishati hii ya mafuta ya taa, wana uwezo wa kutosha wa kumudu!...Kilichofanyika ni namna ya kujionyesha kwamba WAPO na wanatenda kazi, hasa ukizingatia aibu iliyojitokeza kwa mwenye nchi majuzi!Wananchi hawana mtetezi!
 
exactly! aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Lakini wanapaswa kujua kuwa wamepewa dhamana (madaraka) kwa ajili ya hawa walalahoi.
 
Naona EWURA waheshindwa kazi, haya mafuta ya taa ndio mkombozi wa wale akina yahe wa kule Kidodi, Kisanga, Deko nk ambako hata Oryx hawajafikisha gesi wala moto poa, kama watu wa kule Mkadage wanashindwa hata kupata milo miwili kwa siku, iweje leo hii unafikiria kuwapandshia bei ya nishati ambayo ndio mkombozi wao?

Jamani kwa hili tusiwape nafasi, Ewura na watu wa Vipimo tunawalipa kwa kodi zetu, hebu fanyeni kazi kuzuia uchakachuaji na sio kupandisha bei ya mafuta ya taa, mtawauwa hawa wa kule Ibinzamata kwa kukosa Mwanga, mwataka watu wajifungue kwa mwanga wa kijinga cha moto??????????

Mimi sikubaliani nalo hata kidogo!!!!!!
 
Hapo anayetafutwa ni mlalahoi, wanajua kabisa over 95% ya wakazi wa dar wanatumia mkaa na mafuta kama nishati ya kupikia. Ni lazima mlalahoi anyongwe ili serikali ipate mapato?
 
Nashangaa mabosi wa EWURA hawajajiwajibisha wala kuwajibishwa kwa kushindwa kabisa kuthibiti hili la uchanganyaji mafuta. Wanatafuta majibu rahisi yanayowakandamiza mamilioni ya walala hoi - ali mradi hao wenye magari wapone!
 
Bei ya mafuta ya taa kuwa sawa na petroli, pengine sio tatizo sana kama bei hizo zipo chini (affordable). Tatizo hapa wanataka bei ziwe sawa kwa kupandisha bei ya mafuta ya taa badala ya kupunguza bei ya petroli. Kama issue ni differential price pekee basi washushe bei ya petroli (wapunguze kodi kama ilivyo kwa mafuta ya taa) ili ilingane na bei ya mafuta ya taa!
 
mie kaniwacha hoi kwa kusema ikiwa kodi itaongezwa kwa mafuta ya taa basi watu wa chini watatafutiwa nishati mbadala! puuuuh-liii-ze.......y tell and outright lie!
 
Hawa watu wa jabu sana....sasa watu wa kawaida wata afford vipi?

Kwani wakati wa TPDC ilikuwaje?....tatizo wanalijua vizuri lakini kwa kuwa perpetrators ni watu wao wanagwaya.....badala ya kuangalia amhitaji halisi ya nchi ni yapi kwa mafuta ya taa na kuweka kiwango(quota) cha uingizaji(import) ili kubana hiyo chakachua...say nchi inahitaji tani 100,000 kwa mwaka...basi weka hiyo ceiling bila ku affect bei....wao siku zote walikuwa wanaangalia eti importer analeta tani 50,000 diesel,60,000petroli na 90,000 mafuta ya taa na mtu hashangai mafuta ya tyaa hayo yote yanaenda wapi....

Kuna wakati nilipewa kazi ya kukagua mahesabu ya kituo...muendeshaji kanunua lita 5,000 diesel na lita 4,000 mafuta ya taa,nikamuuliza mbona umeuza lita 8,560 za diesel wakati opening stock ya diesel ilikuwa lita 860? Akakosa jibu lakini ukweli ni kuwa ukijumlisha opening stock na purchases unapata lita 5,860 sasa hizo lita extra (8,560-5860)=lita 2,700 ni mafuta ya taa...ajabu ni kuwa alikuwa na salio lita kama 1250 za mafuta ya taa kwenye stock lakini mauzo hakuna,nikamuuliza umenunua lita 4,000 za mafuta ya taa umeyapeleka wapi...hakuwa na jibu akataka tuongee...nikaondoka
 
Hapo anayetafutwa ni mlalahoi, wanajua kabisa over 95% ya wakazi wa dar wanatumia mkaa na mafuta kama nishati ya kupikia. Ni lazima mlalahoi anyongwe ili serikali ipate mapato?

Eee Mwenyenzi Mungu, mwingi wa rehema tujaalie waja wako tuwe na viongozi wenye punje ya busara na huruma....
 
eee mwenyenzi mungu, mwingi wa rehema tujaalie waja wako tuwe na viongozi wenye punje ya busara na huruma....

mimi nawaunga mkono ewura maana hawa mnaowatetea kama walala hoi ndio ambao muda wote hawataki mabadiliko , acha wajionee ili akili zao zipate amka naamini mungu amewatumia hao ewura kwa upendo wake kwetu ili kuwaamsha watanzania ktk usingizi huu mzito.
 
kwa lugha nyingine unamaanisha uzembe wa ewura kuthibiti hili tatizo ubebwe na mlalahoi ili wao ewura kazi yao iwe ni kukaa tu ofisini na kupandisha bei. hivi umewafikiria watu wanao ishi vijijini kuwa mafuta ya taa ni nishati muhimu kwao, naamini huyo Mungu unaye mzungumzia sio huyu MUNGU wa upendo tunae mjua
 
Nadhani hujamwelewa SHA.

Anasema sarcastically kwamba hio mbiu ya EWURA itawaamsha walalahoi kujua kwamba serikali haiwajali kama inavodai na kujinadi, hivo itawaamsha kuchukua hatua..at least hivo ndio nilivomuelewa.
 
Nimekusoma mkuu , imekaa vizuri hiyo.
 
Tanzania ni nchi ambayo ina sheria nzuri sana tatizo ni kwamba hazifuatwi.
  • Sheria ya trafiki - njia moja hugeuzwa tatu na hakuna noma, viwango vya mwendo kasi vipo lakini havifuatwi na hakuna noma, waendeshaji wasio na leseni wanaendesha na hakuna noma.
  • Uvutaji sigara sehemu za uma
  • Miziki ya sauti za juu sehemu za makazi
  • Kwenda umelewa kazini
n.k, n.k
 
Hawa watu wa jabu sana....sasa watu wa kawaida wata afford vipi?

Kwani wakati wa TPDC ilikuwaje?....tatizo wanalijua vizuri lakini kwa kuwa perpetrators ni watu wao wanagwaya.....badala ya kuangalia amhitaji halisi ya nchi ni yapi kwa mafuta ya taa na kuweka kiwango(quota) cha uingizaji(import) ili kubana hiyo chakachua...say nchi inahitaji tani 100,000 kwa mwaka...basi weka hiyo ceiling bila ku affect bei....wao siku zote walikuwa wanaangalia eti importer analeta tani 50,000 diesel,60,000petroli na 90,000 mafuta ya taa na mtu hashangai mafuta ya tyaa hayo yote yanaenda wapi....

Kuna wakati nilipewa kazi ya kukagua mahesabu ya kituo...muendeshaji kanunua lita 5,000 diesel na lita 4,000 mafuta ya taa,nikamuuliza mbona umeuza lita 8,560 za diesel wakati opening stock ya diesel ilikuwa lita 860? Akakosa jibu lakini ukweli ni kuwa ukijumlisha opening stock na purchases unapata lita 5,860 sasa hizo lita extra (8,560-5860)=lita 2,700 ni mafuta ya taa...ajabu ni kuwa alikuwa na salio lita kama 1250 za mafuta ya taa kwenye stock lakini mauzo hakuna,nikamuuliza umenunua lita 4,000 za mafuta ya taa umeyapeleka wapi...hakuwa na jibu akataka tuongee...nikaondoka

je hatua gani alichukuliwa baada ya hapo? au mliongea kesho yake
 
Back
Top Bottom