Eti anataka tusahau yaliyopita..........

Mfalme Daud

Senior Member
Feb 3, 2012
166
109
Wanajanvi wenzangu, Asalam aleykum? Ninalo tena jaribu linaloitesa roho yangu. Mapenzi yanataka kunifanya, sijui? Sahibu langu ni kama ifuatavyo; miaka mitano iliyopita nilikuwa na mpenzi. Alikuwa mwanafunzi wa sekondari minikiwa mtumishi wa serikali. Nilimpenda na kumtimizia chochote alichohitaji. Kwasababu nilikuwa na mpango wa kumuoa na yeye akiwa mwanafunzi sikupenda kabisa ku"do" naye na tulikubaliana hivyo. Matokeo ya kidato cha nne yakatoka, kwake hayakuwa mazuri kwani alifeli kabisa. Ok misikujali suala la elimu kwangu hakikuwa kigezo. UKAFIKA MUDA WA KUOANA. Tulipanga miezi minne kabla sijaenda kuongeza elimu tufunge ndoa na awe wa kwangu kwelikweli. Tulipendana sana. Muda huo ulipofika nikaanza kumfuatilia ili tuanze maisha, hapo ndio utata ukaanza. Alikuwa haoneshi RESPONSE yoyote. Nilimbembeleza utadhani ndo tunaanza mapenzi, kwa kweli hakunielewa. Minikaenda Shule, baada ya miezi kadhaa nikasikia ni mjamzito. Roho iliniuma kweli lakini sikuwa na jinsi. Akawa ameolewa na jamaa alompa mimba, akaanza kumtesa. Baadaye binti akaachana na jamaa na kujifungulia nyumbani salama. Yule jamaa alishaoa mke mwingine. Huyu binti anajutia makosa aliyotenda NA ANATAKA TUSAHAU YALIYOPITA. WANAJF naombeni ushauri JICHUKULIE KAMA ni wewe. NIFANYEJE
 
MMh, unaonekana umeshafanya maamuzi
Hapa unataka justifications tu.

Kama una kifua beba.
Lakini una vi-element vya Bushoke:A S embarassed:
 
We bado unampenda? Moyo wako unakuambia nini? Nafsini mwako kama mwanaume unalionaje hilo? Jibu haya maswali yangu halafu naweza kukusahuri
 
Achana nae!

Kwani mwanamke ni yeye peke ake?

sasa unataka kumlazimisha aachane naye kisa wanawake ni wengi?unajua nafsin mwake kuna nini? Au huujui msemo wa kila shetani na mbuyu wake,kipendacho roho hula nyama mbichi.
 
Yaani wewe NECTA imetema, afu unataka ukang'ang'ane na used iliyokukimbia??
 
Siku hizi nyama mbichi ina mafua ya wanyama

Afu mibuyu imeisha sasa hivi mashetani yanaenda hata kwenye miembe
sasa unataka kumlazimisha aachane naye kisa wanawake ni wengi?unajua nafsin mwake kuna nini? Au huujui msemo wa kila shetani na mbuyu wake,kipendacho roho hula nyama mbichi.
 
Wanajanvi wenzangu, Asalam aleykum? Ninalo tena jaribu linaloitesa roho yangu. Mapenzi yanataka kunifanya, sijui? Sahibu langu ni kama ifuatavyo; miaka mitano iliyopita nilikuwa na mpenzi. Alikuwa mwanafunzi wa sekondari minikiwa mtumishi wa serikali. Nilimpenda na kumtimizia chochote alichohitaji. Kwasababu nilikuwa na mpango wa kumuoa na yeye akiwa mwanafunzi sikupenda kabisa ku"do" naye na tulikubaliana hivyo. Matokeo ya kidato cha nne yakatoka, kwake hayakuwa mazuri kwani alifeli kabisa. Ok misikujali suala la elimu kwangu hakikuwa kigezo. UKAFIKA MUDA WA KUOANA. Tulipanga miezi minne kabla sijaenda kuongeza elimu tufunge ndoa na awe wa kwangu kwelikweli. Tulipendana sana. Muda huo ulipofika nikaanza kumfuatilia ili tuanze maisha, hapo ndio utata ukaanza. Alikuwa haoneshi RESPONSE yoyote. Nilimbembeleza utadhani ndo tunaanza mapenzi, kwa kweli hakunielewa. Minikaenda Shule, baada ya miezi kadhaa nikasikia ni mjamzito. Roho iliniuma kweli lakini sikuwa na jinsi. Akawa ameolewa na jamaa alompa mimba, akaanza kumtesa. Baadaye binti akaachana na jamaa na kujifungulia nyumbani salama. Yule jamaa alishaoa mke mwingine. Huyu binti anajutia makosa aliyotenda NA ANATAKA TUSAHAU YALIYOPITA. WANAJF naombeni ushauri JICHUKULIE KAMA ni wewe. NIFANYEJE

kwenye blue hapo wengi wameangamia kwa kosa hilo.
 
Gonga mzigo halafu tambaa.Naona umesikia uchungu sana huku mgonga ndo kinachokuangaisha hapa fanya huo mpango fasta
 
sasa unataka kumlazimisha aachane naye kisa wanawake ni wengi?unajua nafsin mwake kuna nini? Au huujui msemo wa kila shetani na mbuyu wake,kipendacho roho hula nyama mbichi.
Namuhurumia asije akatendwa tena akaja na uzi mpya, manake alimthamini bidada ili asome kwanza kumbe mwenzie anamchora tu kwa pembeni!..

Hata hivyo akili za kuambiwa achanganye na zake, sitegemei majibu yetu humu yatampa mwongozo bila kuchanganya na yakwake!...

Hujambo?..za kupotea?
 
Kwa kuwa ameachwa ndio wewe umekuwa kimbilio
Je kama asingeachwa wewe ungekuwa wapi au angekuona wa maana
So siku yule aliyempa mimba akijijua amekosea na akaja kumuomba msamaha itakuwaje
Mkuu akili kichwani mwako na wewe jitambue uko wapi
Usifanywe makapi kwa kuwa ana shida ndo anakuona wa maana sasa
Wakati anaolewa hakukujua wewe na msaada uliompa
 
hakuna penzi hapo hakupendi ila shida ndo zinasababisha piga chini
 
Kwa kuwa ameachwa ndio wewe umekuwa kimbilio
Je kama asingeachwa wewe ungekuwa wapi au angekuona wa maana
So siku yule aliyempa mimba akijijua amekosea na akaja kumuomba msamaha itakuwaje
Mkuu akili kichwani mwako na wewe jitambue uko wapi
Usifanywe makapi kwa kuwa ana shida ndo anakuona wa maana sasa
Wakati anaolewa hakukujua wewe na msaada uliompa
Umesema vema Mr. Rocky, huyu sidhani kama amejiuliza hayo maswali manake kama angejiuliza asingekuja na huu uzi... Mwenzie katemwa ndio mana anamwona wa maana kwa sasa.
 
Namuhurumia asije akatendwa tena akaja na uzi mpya, manake alimthamini bidada ili asome kwanza kumbe mwenzie anamchora tu kwa pembeni!..

Hata hivyo akili za kuambiwa achanganye na zake, sitegemei majibu yetu humu yatampa mwongozo bila kuchanganya na yakwake!...

Hujambo?..za kupotea?

mi nipo sijapotea,ni kuna wakati tu napoteza hamu na hili jukwaa, hivyo napita zaidi jukwaa la matangazo,mchanganyiko na siasa.sometimes nakuwa bored na mmu kwani kuna post nyingine zinaweza kukusababisha hata ukatenda dhambi kwa kuandika mambo ambayo siyo, hata kwa kuchangia tu.maana post nyingine kuzisoma tu ni najisi ukizichangia ndio kabisaa unajitia unajisi.
 
Maamuzi unayo mwenyewe. Lakini tafakari kuwa alikusaliti hapo awali..... Je hatafanya hivyo tena? Huwezi kuoa mwanamke ajili ati unamwonea huruma. Kwani wewe ni BABA HURUMA. Kaa ukitafakari na umpe ulicho shuriwa iwe kama inatoka kichwani mwako. Maamuzi unayo mwenyewe.
 
Back
Top Bottom