Eti anaoteshwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti anaoteshwa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by JICHO LA TATU, Oct 2, 2012.

 1. JICHO LA TATU

  JICHO LA TATU JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 307
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jamani mi mwenzenu kuna kaka mmoja huwa ninamfanyia kazi zake, kwa kifupi ni mteja wa ofisi yetu sana hatimaye ametuzoea wote pale ofisini.
  Eti kama mwezi hivi anakuja kwangu nakuniambia anaoteshwa kila siku akilala na Bwana kwamba mimi niwe mke wake
  Kiukweli nimejitahidi kumkatalia kwa juhudi zangu zote kwamba haiwezekani inshort sijaridhika naye.
  Sasa naona ishakuwa kero kwangu c'z kila akija lazima aongelee hilo suala na anasisitiza ni bora nimkubalie ili aweze kulala na kuishi kwa amani.
  Wanajamvi wenzangu nimelileta kwenu naomba mnisaidie nimpe jibu gani ili apate kunielewa.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kama wewe ni mama huruma chukua hatua mapema kama unajitambua muoneshe bwana ako nadhani ataona noma na chengine isije ikawa ulimpa kisela halafu kakuganda kama ruba ndio uje umtoe nishai humu jamvini..maana hizo ndio zenu mashostito..
   
 3. m

  mhondo JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mwambie asubiri na wewe uoteshwe.
   
 4. JICHO LA TATU

  JICHO LA TATU JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 307
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0


  Ningekuwa nimempa basi kusingekuwa na haja ya kuposti na kuomba msaada
   
 5. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Huyo ni tapeli wa kawaida na muogope kama ukoma. Muulize huyo Bwana kwanini anamuotesha yeye peke yake. Isitoshe nani ataamini upuuuzi unaoitwa ndoto kwenye karne hii? Kama kweli anakupenda na kukufaa kwanini asiwe mkweli badala ya visingizio vya kitoto? Kesho atakuoa na akikuchoka anakwambia ima Bwana amemuotesha aoe mke wa pili au akuache kama si kukutoa kafara. Yesu aliwahi kuonya kuhusu kuwaogopa waota ndoto. Maana hawa ni manabii wa uongo ambao kwa sasa wamejaa. Kama anaoteshwa basi mwambie akamuoa Getrude Rwakatare maana hana mume.
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ila unampango gani nae kama hujaridhika nae chukua uamuzi wakumuonesha mshkadau mwenyewe ndio huwa tunafanya hivyo hasa unapo sumbuliwa na mdada ambaye humpendi so unaweza tumia idea hiyo kwako sawa mama..
   
 7. JICHO LA TATU

  JICHO LA TATU JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 307
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Thank you,na hii nayo inamantiki
   
 8. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Kama humtaki mwambie point blank kuwa HUMTAKI, mambo ya ndoa siyo ya kubahatisha. Kwanza mwongo, uongo huo huwa wanautumia walokole akitaka kumpata mtu. Acha biashara hiyo kabisa, ni ushetani afadhali angelisema nakupenda, lakini ya kuoteshwa anataka akuonje akutupilie kwa mbali!
   
 9. moto2012

  moto2012 JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 2,168
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Heshimu hisia zako, na kama hakidhi vigezo vyako achana nae!!!
   
 10. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Tabu ya nini! WE MUOMBE 1M ULIPIE KODI YA NYUMBA!!!! Hatokaa akusogeleee, atakuwa anapita mbali. Ukiendelea kumkataa kistarabu mwenzio anaona UNAZUGA TU ILI USIMKUBALI HARAKA HARAKA!!!! Bugdha hazitoisha, dawa ni hiyo hapo INATIBU AINA ZOTE ZA PENZI LISILOTAKIWA!!!! LOLEST!
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Una vituko sana!


   
 12. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Itakuwa vipi kama huyo Jamaa akimkatia hiyo Im?
   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Huyo ni mjanja wa town tu !
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  yaani akili zako za mchuzi lakini saa zingine zinafanya kazi eeh?
  Au amuambie na yeye kaoteshwa kuwa mume wake mtarajiwa atamjengea nyumba ndani ya mwaka mmoja kwa jina la bibie. Waone huo mwaka utakavyoisha na ndoto kuyayuka.
   
 15. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Thubuuutu yake!!! Akimkatia sio ishu ANAAGIZA 2M YA SOFA, IKITOKA INAFATIA 4M YA KIWANJA!!!! LOLEST! There is always more than 1 way to kill a person!!! Hata kumtosa mtu pia! LOL! Watu wengine maneno hawaelewi, hadi PICHA!
   
 16. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Angekuwa kweli kaoteshwa na wewe pia ungekuwa umeoteshwa dhidi yake maana hayo mambo huwa yanagusa pande zote mbili. Hiyo ni janja yake tu ya kutongoza, kwa ushauri kama humpendi achana naye. Si vyema kujilazimisha kuingia kwenye mahusiano ambayo moyo wako haujaridhika nayo. Take Care.
   
 17. Root

  Root JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,189
  Likes Received: 12,906
  Trophy Points: 280
  Mawazo ya binti fulani ni sawa na icecream juani

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 18. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Heshima kwako mdada, hapo sina swali
   
 19. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  hivi maono bado yapo??? kazi ipo!
   
 20. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #20
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  lara 1 sijui maneno huwa unayapata wapi? Khaaaa!
  Kwa 1m hata mimi kama sina nia ningeingia mitini!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...