Habari wandugu, natumaini mko poa.
Mimi nina mpenzi wangu tumekuwa nae kwenye mahusiano huu ni mwezi wa tatu,sio siri huyu binti nampenda sana, nimejitahidi kumhudumia kadri niwezavyo kwa mda mfupi nilikuwa nae, kwa sababu nina nia ya kumuoa, sasa juzi nilikuwa na rafiki yangu tupo maeneo ya Sinza tukapita kwenye bar moja hivi ghafla nikamuona mpenzi wangu nae yupo mle ndani ya bar anakunywa kinywaji wakiwa wamekaa na mwanaume mmi simjui, ndipo nikaamua kumpigia simu mpenzi wangu nakumuuliza yuko wapi.
Akapokea simu nakunijibu yupo nyumbani kwao anapika na wakati minamuona yupo na kijeba wanakunywa vinywaji huku wanacheka, sio siri nilipatwa na hasira ndipo nikaamua kumtuma rafiki yangu akamuite ili niongee, aliponiona alishangaa na aliponisogelea tu sikumsemesha neno lolote nikampiga kofi moja la nguvu rafiki yangu akanishika mikono na watu wakajaa kidogo, nikaamua kuondoka na yule binti akawa amekipingia.
Sasa zimepita siku mbili yule binti nimempigia simu akapokea akaniambia yule alikuwa kaka yake mtoto wa baba yake mdogo na pia ameniambia mimi na yeye basi amesema hawezi kuishi na mtu kama mmi tena, nimejaribu kumuomba msamaha lakini wapi amekataa katakata.
Naombeni msaada wa mawazo jamani nifanyeje? Eti kofi moja tu linikoseshe mke jamani.