Ethiopia: Msiba wageuka kuwa sherehe

Ethiopia: Msiba wageuka kuwa sherehe

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,048
Reaction score
61,370
Wanakijiji wa kijiji kimoja nchini Ethiopia washeherekea kufufuka kwa mwanaume mmoja ambaye alidhaniwa kuwa amekufa.

Hirpha Negero, ambaye ni baba wa watoto watano alitangazwa kuwa amefariki siku ya jumanne ,majira ya saa nne na nusu.

Kulingana tamaduni zao katika vijiji vya pembezoni mwa miji vilivyopo Sibu Sire na mkoa wa Oromia,bunduki ilipigwa mara mbili na hiyo ni ishara kuwa kuna mtu amefariki hivyo watu wanaitwa kuhudhuria katika msiba.

Ndani ya saa moja, mwanakijiji mmoja kwa jina la Etana Kena alimuweka kwenye jeneza tayari kwa mazishi.

Ingawa wakati wa mazishi katika majira ya saa tisa na nusu, walisikia mtu akigonga kutoka katika jeneza.

''Watu walishangaa na huku wengine wakikimbia na hata sikupata mtu wa kunisaidia," bwana Etana alieleza namna alivyohitaji msaada ili aweze kulifungua jeneza.said.

Mtu aliyefufuka aliiambia BBC jinsi alivyojisikia akiwa ndani ya jeneza: "Nilisikia sauti ya mtu akilia. Nlikuwa sina nguvu kabisa n ahata sikuweza kuongea."

Lakini badaye aliweza kuanza kuita.

Baada ya mshtuko ambao uliwapata wengi katika msiba, mazishi yaligeuka kuwa sherehe.

Hirpha alieleza kuwa alishawahi kuzika maiti zaidi ya 50 lakini hakuwahi kukutana na tukio kama hilo.

"Alionekana kuwa amekufa kabisa".

Dr Birra Leggese aliiambia BBC kwamba labda alikuwa amepooza.

Screenshot_20181125-084507~2.jpeg
 
View attachment 945453
Alifka jehanamu au hakufka?
 
Mada za ubabaishaji bhana,

Hirpha Negero, ambaye ni baba wa watoto watano alitangazwa kuwa amefariki siku ya jumanne ,majira ya saa nne na nusu (Hapa aliyekufa ni Hirpha Negero)

Ndani ya saa moja, mwanakijiji mmoja kwa jina la Etana Kena alimuweka kwenye jeneza tayari kwa mazishi. ( Etana alimueka Hirpha kwenye jeneza)

Watu walishangaa na huku wengine wakikimbia na hata sikupata mtu wa kunisaidia," bwana Etana alieleza namna alivyohitaji msaada ili aweze kulifungua jeneza.said. (Hapa Etana ndio alikuwa ndani ya jenezs)

Kajipange upya.
 
Mbona anaficha kutueleza aloyoyaona huko?

Daah huwezi kuongea ya kule kiapo kwanza memory yote inafutwa fasta au unapata utaahira au ububu maisha yako yote,"ULIOYAONA USISEME KWA WATU MWANANGU"
 
Ana bahati ya kua kwenye kikao na MALAIKA mtoa ROHO. Ila asipo okoka baada ya kisanga hicho, basi hata ashuke Yesu jamaa haokoki tena[emoji53]
 
Daah huwezi kuongea ya kule kiapo kwanza memory yote inafutwa fasta au unapata utaahira au ububu maisha yako yote,"ULIOYAONA USISEME KWA WATU MWANANGU"
Hahahahahaha mkuu akisema aliyoyaona huko tunaweza kuzamia huko kwa kasi ya mwanga
 
Huyo hakufa. Kwa uelewa wangu, mtu akifa hafufuki. Tunasoma Yesu pekee ndie alikufa akafufuka.
 
Back
Top Bottom