Ethiopia hiyoooo

Pamoja na maelezo na picha za kuvutia, inakuwaje basi Wahabeshi wengi wanakamatwa hapa Bongo kama wahamiaji haramu!? Na wengine wanafia kwenye makontena! Hawataki neema hizi?
 
Hawa hamna lolote wananchi wao wanaishi maisha magumu sana na ndio maana wanakimbia nchi yao na kwenda nchi kama south africa ni mara ngapi wamekamatwa kwenye malori hawa wahabeshi kama wahamiaji haramu, mimi wala sioni kama ni nchi ya mfano na pia ki takwimu sisi tunamtandao mpana wa barabara za lami kuliko wao, ADIS ata ikiwa kama JOBERG lakini kama maeneo mengine ni hovyo ni bora DAR isiwe na hizo treni wala fly overs lakini barabara za Tunduru Mangaka Babati Kondoa Ngara Biharamulo Kigoma Urambo Nzega Tabora Iringa Dodoma Tunduma Sumbawanga zijengwe.
 
Magufuli alisema itajengwa tazara sasa sijui kama nafasi itatosha maana haya ma fly over yanachukua nafasi kubwa saana
 
safi..sijui Dar patabadilika..mana mhh foleni is trouble,naona solution ni kuhamia mjini tu
 
Mkuu, Njaa kitu kibaya sana. Mwanaume mzima ananunuliwa kwa buku 7 ili kuja kutetea maslahi ya wanaume wengine!
Mkuu na wengine huwa wanalipwa kushughulikia wanaopinga serikali mbili kama hivi..
 
Unafikiri bila ya kuwapeleka kozi Ulaya watakwambia hawawezi kuendesha hao, chezea mbongo wewe...
Wakitaka kwenda ulaya tunawapeleka tena ndo vizuri maana train zishakua yeboyebo kwa hiyo training itaenda vizuri... Train driving licence mtu haitaji miaka kusomea
 
Yeah, nimeenda Ethiopia mara kadhaa, na kila unapofika unaona mabadiliko ya dhati kwa macho. Highways na miundombinu inajengwa kwa kasi sana. Hawana siasa za kijinga, wanauzalendo wa dhati, huduma kwenye maofisi ya serika ni nzuri sana. Na kwa kweli utofauti mkubwa huonekana kati yao na watendaji wetu ambao 98% hukalia ofisi kwa manufaa ya matumbo yao badala ya manufaa ya nchi na vizazi vijavyo.
 
.......kudadadeki ...wazee watembo wasingekuwepo madarakani leo angalau hata DART ingefanya hata trip mbili.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…