ESTIM Construction ni kampuni ya nchi gani?

ESTIM Construction ni kampuni ya nchi gani?

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,262
Reaction score
18,706
Katika uchunguzi wangu wa miradi ya barabara nimegundua kampuni inayojulikana kama ESTIM inajenga barabara zenye ubora wa hali ya juu sana. Cha ajabu zaidi hawa ESTIM wapo vizuri sana kwenye madaraja na majengo hasa yale makubwa.

Kuna picha nimeona wanavyo jenga barabara ya Kimara kibaha kule Dar es salaam. Kilicho nivutia ni jinsi wanavyo jali mazingira kuhakikisha kwamba sehemu ambazo wameharibu uoto wakati wanajenga wanajitahidi kurudiashia uoto huo kwa kupanda nyasi na miti hata kabla barabara haijaisha kitu ambacho sijakiona kwa kampuni nyingi za kichina.

Jambo kama hilo limeonekana hasa kwa wale jamaa wanaojenga SGR pekee.

Pamoja na hayo yote hawa jamaa wanaonekana kuleta namna mpya ya ujenzi wa barabara zenye quality.

Baadhi ya barabara niliwahi kuipita ni ile ya Goba jijini Dar es salaam sijui kwa sasa kama bado nzima lakini kwa ujenzi ule naamini hadi sasa itakua bado imara.

Kuna wachina walipewa kujenga barabara ya Bagamoyo Msata, nasikia waliopoona lile bonde walikimbia, nasikia kazi iliyo fanywa na ESTIM ya kujenga Madaraja katika bonde lile ni ya kutukuka.

Sijajua kampuni hii inatoka nchi gani lakini serikali inahitaji kuitambua kwa mchango wake.

Mapendekezo

Kwenye issue za madaraja waachiwe hawa jamaa.

Barabara za magari makubwa waachiwe hawa jamaa.

Majengo ya taasisi kama vyuo etc waachiwe hawa jamaa.

Nasema kutoka moyoni, sijawahi kusikia kashfa ya kazi mbovu toka hii kampuni.

Kama ipo ni ya bahati mbaya.
FB_IMG_1559735159631.jpeg
 
Ni kampuni inayomilikiwa na mtanzania mwenye asili ya Uhindini (Uraia wa kusajiliwa)

Hivyo kuiwezesha kusajiliwa kama kampuni ya kizawa

Ni kampuni daraja la kwanza (1) kwenye majengo na uhandisi wa miundombinu jamii.
 
Una akili mbovu sana, sema umeingilia fani isio yako. Hata Estim hujui ni ya wapi, na umekuja na unaa kama sio sifa za kuipigia debe. Kuanzia lini wewe ukasema Estim ndio inatakiwa iachiwe Kazi za madaraja, Kazi za majengo na barabara kampuni zingine zitafanya nini? Umekuja na hoja mufilisi kabisa eti wachina walikimbia ujenzi wa Bagamoyo- Msata, wakafanya Estim, umezidi kujichanganya kwamba umetumwa.

Sasa kwa taarifa yako ni ujenzi wa Kawaida sana kutokana na aina ya ujenzi wa barabara uwe na Kiwango gani. Barabara zina madaraja matano, earth road, gravel road, single surface dressing na double, la mwisho ndio premix ndio hizo wanajenga hao wanaume wako. Zitatofautia layer tu za ujenzi basi kwa ajili ya kuhimili uzito tofauti tofauti.
Kwa taarifa yako ni kampuni ya hapa Tanzania, ikiwa kampuni tanzu ya Caspian.

Ili kukuweka wazi kuna kampuni kubwa zenye level moja na hiyo na zinafanya Kazi iliyotukuka sana.
Mtu wa muhimu kuhakikisha ujenzi unakuwa wa Kiwango ni specification za kwenye mkataba, na usimamizi na ukaguzi wa client na consultant.

Wafanye stage zote za ukaguzi, kabla, wakati na mwisho.
Pole na hongera kwa kuongea hisia zako hadharani. Tabutupu,
 
Kama na akili mbovu niambie mradi wowote ambao walau umelalamikiwa kwamba umejengwa chini ya kiwango.


Hata kampuni yako ingefanya vizuri ningefanya the same.

Kuna makapuni kibao yanachoma kodi za wananchi. Gullam,
 
Naweza sadiki
Ni kampuni inayomilikiwa na mtanzania mwenye asili ya Uhindini (Uraia wa kusajiliwa)

Hivyo kuiwezesha kusajiliwa kama kampuni ya kizawa

Ni kampuni daraja la kwanza (1) kwenye majengo na uhandisi wa miundombinu jamii.
 
Back
Top Bottom