Linyakalumbi
JF-Expert Member
- Jul 28, 2011
- 263
- 107
Mkuu kwenye political platform, mvuto wa sura una umuhimu sana kuwavutia watu wakufahamu au wakupende. Umesahau ya JK 2005?
*Esther Bulaya ni mbunge wa kike, kijana kwa tiketi ya CCM viti maalum, watu wengi wamepata kumzungumzia uwezo wake wa kisiasa humu JF mara kadhaa. Ameonekana Bungeni na mara kadhaa kwenye majukwaa ya kisiasa akijenga hoja.
*Esther Wassira alionekana kwa mara ya kwanza kwenye ulingo wa kisiasa siku akichukua kadi ya CHADEMA, watu wengi walitaka kumfahamu uwezo wake wa kisiasa(kujenga hoja na kuamsha ushawishi), na kupitia hotuba aliyoitoa kwenye kongamano la kumbukumbu ya mwalimu Nyerere pale Nkurumah kila mtu sasa anaweza kumzungumzia.
*Sababu za kutaka kuwalinganisha kisiasa.
1/Mfanano wao (Wote ni wanasiasa, vijana, wanawake, wanatoka Bunda, wameshawahi kuwa na mzozo wa kisiasa na Steven Wassira, wote wanaitwa Esther!!)
2/Wanatoka vyama viwili vinavyopinzana.
3/Watu wengi wanataka kuona mmoja wao akirithi kiti cha ubunge wa Steven Wassira kule Bunda 2015.
***Wadau wa JF mnaweza kuchangia kwa kujenga hoja za ulinganifu wao kisiasa.
hatuchagui sura tunachagua mtu mwenye uwezo wa kutunasua kwenye matatizo tuliyo nayo!Esther Wassira kwa kweli sio mzuri wa kujenga hoja tu ila hata sura anayo. Sikuwepo kwenye jukwaa la mwalimu lakini na nilimwona kwenye TV jana akanivutia sana sana learned counsel, nadhani kama vile natamani kumfahamu zaidi
Kila la heri Kamanda
mkuu acha uoga aingie humohumo kwenye jimbo la baba yake.Kwa nilivyo msikia jana tean muda wenyewe aliopewa? Hapa tuwe wawazi, hata kama mtu huwa haipendi CDM utajikuta unaipenda tu, ukweli CDM pale wamelamba Dume, dada ni mzima, anajenga hoja, ana present hoja, hana hofu na anaweza ku-join dots, Bulaya kama ana ndoto za kugombea pamoja na huyu nafikiri atakua anapoteza muda, ataabika, asipeleke timu pale, labda something to caution, kama huyo baba yake naye ataonehs interest za kugombea jimbo moja, nina hofu suala la kifamilia hapo ninaweza kumuathiri huyu binti, atakapo anza kuporomosha madongo ninahakika Steven Wassira atakosa wasikilizaji, kamati ya nyumbani then inaweza kukaa, hebu hapa Esther pamoja na CDM walifikirie hili mapema, ninahakika huyu Binti humu jamvini lazima ni member tu, sio lazima achangie but heb afikiri hili then abadiri hata jimbo, sheria zinaruhusu then pale Bunda CDM wapepeleke mtu mwingine asie na conflict of interest!
Huyu Esther Wassira ndiye yule mwanabongoflava aliyewika miaka ya mwanzoni mwa 2000 au majina tu yamefanana?(Wengine hatukuuona huo mdahalo)
Umenikumbusha kitu mkuu. Nilikuwa najaribu ku-recall hiyo sura na speaking style.
Nadhani atakuwa ndiye yule aliyeshika nafasi ya pili nyuma ya Banana Zahir Ally 'Zorro' kwenye mashindano fulani ya kuimba waimbaji chipukizi (actually Banana alikuwa ameshakuwa mwanamuziki kamili hivyo ushiriki wake ulitiliwa mashaka).
Aliyechaguliwa (Banana) alienda Afrika ya Kusini kwa hatua iliyofuata ambapo alitolewa.
Nakumbuka Ester aliimba wimbo wa 'I miss you' alioimbiwa Aaliyah baada ya kufariki. Aliupatia vibaya!!
Japokuwa huyo wa bongoflavour simkumbuki vizuri bado sioni mfanano wowote kimaumbile wala Kiupeo kati yao.
*Mkuu mpaka sasa Esther Wassira ameshaongea mara tatu katika matukio matatu tofauti ya kisiasa (Akichukua kadi ya Chadema, Akifafanua mzozo wa Wassira, Kongamano la kumbukumbu la Nyerere).Mi naona ni vigum kumlinganinisha Esther Wasirra na Esther Bulaya kwani, watanzania wengi wamemsikia Esther Wasira kwa mara ya kwanza jana.Na hatujui consistency yake itakuwaje,na si rahisi kudraw conclusion yake kwa kumsikia mara moja tu!!Labda tumpe muda,lakin kwa upande mwingine Esther Bulaya tunamfahamu vizuri
*Mkuu mpaka sasa Esther Wassira ameshaongea mara tatu katika matukio matatu tofauti ya kisiasa (Akichukua kadi ya Chadema, Akifafanua mzozo wa Wassira, Kongamano la kumbukumbu la Nyerere)
*Uchache wa kuongea kwenye mambo ya kisiasa angempa Disadvantage na sio advantage.
*Jambo kubwa ni ubora wa unachokiongea(Quality) na
wala sio wingi wa ulichokiongea(Quantity) hivyo bado unaweza kuwapima uwezo wao kisiasa(kujenga hoja na kushawishi)
Mkuu embu fafanua zaidi.Huyo Bulaya naye ni cdm 2015
hayo mashindano yalikuwa yanaitwa coca cola pop idol!