Escrow yarudi bungeni kwa kishindo

Escrow yarudi bungeni kwa kishindo

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,331
Escrow yarudi bungeni kwa kishindo

KASHFA ya uchotwaji fedha za Umma katika Akaunti ya Tegeta Escrow Sh. 306 bilioni, iliyofunguliwa kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT) bado haijazimika, licha ya Serikali kujaribu kuwasafisha baadhi ya watuhumiwa ikidai hawahusiki. Anaandika Edson Kamukara … (endelea).
Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM) ndiye ameifufua bungeni akisema, kitendo hatua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kuwasafisha baadhi ya watuhumiwa wa kashfa hiyo ni ubaguzi na usanii usiokubalika.

Wiki iliyopita, Ikulu ilitangaza kuwasafisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi na waziri wake, Prof. Sospeter Muhongo kwamba tume iliyoundwa kuchunguza tuhuma dhidi yao, haikuwakuta na hatia katika suala la miamala ya fedha za Escrow.

Pia, Ikulu kupitia kwa Balozi Sefue, iliwasafisha mawaziri watatu waliojiuzulu kwa shinikizo la Bunge katika kashfa ya oparesheni tokomeza, ikisema licha ya wananchi kupoteza maisha, kuteswa na mifugo kuuawa na askari waliotekeleza oparesheni hiyo, lakini viongozi hao hawakuhusika moja kwa moja.

Mawaziri hao ni Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii) na Dk. Mathayo David (Mifugo na Uvuvi).
Ikumbukwe kuwa sakata la escrow liliibuliwa bungeni na mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na baada ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Fedha za Serikali (CAG) kufanyika, ilithibitika kwamba miamala hiyo ilifanyika kinyume cha sheria huku baadhi ya viongozi wakiwa wamenufaika na mgawo wa fedha hizo.

Akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2015/16, katika eneo la utawala bora, Serukamba amesema "hii staili inayojaribu kutumika ni ya kizamani ya kusafisha watu kiani, imepitwa na wakati".

Huku akisikilizwa na kushangiliwa na wabunge wengi, Serukamba amesema "kama Balozi Sefue anasema Maswi na mawaziri hao ni safi, basi atwambie Andrew Chenge (Bariadi Magharibi), Prof. Anna Tibaijuka (Muleba Kusini), William Ngeleja (Geita), uchafu wao ni upi wakati walipata mgawo halali?"

Chenge, Ngeleja na Victor Mwambalaswa (Lupa), walivuliwa uenyekiti wa kamati za Bunge baada ya kuthibitika kuwa walipokea mgawo wa fedha hizo kutoka kwa mmoja wa wamiliki wa IPTL, James Rugemalira bila kutangaza maslahi kama sheria ya maadili ya viongozi wa umma inavyotaka.

Katika mtiririko huo, mawaziri Tibaijuka, Muhongo na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Jaji Fredrick Werema walijiuzulu kutokana na kashfa hiyo huku baadhi ya watendaji katika mamlaka mbalimbali za serikali wakifikishwa mahakamani na kwenye Baraza la Sekretarieti ya Viongozi wa Umma.

Akizungumza kwa masikitiko kuhusu uamuzi huo wa Ikulu, Serukamba alishauri kuwa, "Chenge, Ngeleja, Werema, Mwambalaswa na mawaziri wengine waliowahi kujiuzulu kama sehemu ya uwajibikaji nao wasafishwe na kurudishwa katika nafasi zao."

"Bunge hapa tuliomba ripoti ya oparesheni tokomeza lakini haijawahi kuletwa ila anajitokeza katibu mkuu kiongozi kusafisha baadhi ya watu. Huu ni usanii wa kuwasaidia watu wachache na kuumiza wengine kwa malengo binafsi. Hatuwezi kuwa na serikali yenye "double standards".

"Lazima wakina Chenge, Tibaijuka na wengine wote mawaziri waliojiuzulu huko nyuma kwa kashfa ya Richmond nao waundiwe tume wasafishwe kama wakina Maswi, vinginevyo mna ajenda binafsi ya kujisafisha," amesema.

Serukamba ameongeza kuwa, wako watumishi wa Ikulu (akina Gurumo na wenzie) wenye tuhuma za escrow lakini bado wanaendelea kubaki kazini huku watumishi wengine wa umma katika taasisi zingine wakifikishwa mahakamani kwa jambo hilohilo na hivyo kuhoji hii ni serikali gani yenye ubaguzi wa aina hiyo?

"Kama ni kuunda Judicial Inquiry (Tume ya kimahakama), basi ifanyike kwa watuhumiwa wote. Hiki si Chama Cha Mapinduzi tunachokijua. Sasa kinachofuata hata hao mliowapeleka mahakamani kwa suala hilo watawashinda kutokana na uamuzi huu wa kusafisha baadhi ya watu.

"Katibu Mkuu Kiongozi anasema hiyo ripoti ya tokomeza hawezi kuileta bungeni badala yake anaisoma nusu nusu na kuwasafisha baadhi ya watu. Huu ni ubaguzi na labda tuambiwe kuna watu mnaowalenga lakini haitawezekana," alisisitiza Serukamba na kushangiliwa.

CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, lyinga, NATA, Chakaza, Elly B, Ablessed, Michelle, KikulachoChako, Emma, EMT, Daudi Mchambuzi, Arushaone, MziziMkavu, Ablessed, afrodenzi, Heaven on Earth, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka, adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, Honolulu, August, dyuteromaikota, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Shark, mirisho pm, Camp 05, Ngoami, Kamakabuzi, jerrytz

 
Mkuu i am telling you it will be old same story, hakuna kitakachofanyika.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hilo linajulikana Mkuu, Rais kayakimbia majukumu yake sasa kamuachia Katibu wake ndiye awe anatangaza maamuzi ya Rais.

Mkuu i am telling you it will be old same story, hakuna kitakachofanyika.
 
Hii ni move ya kuwasafishia njia kugombea na kuiba kura za ubunge ifikapo oktoba, kama uchaguzi utafanyika bila kujali uandikishaji wa wapiga kura umekamilika.
 
...hiki chama kimeshakuwa genge la wah..uni tu wasaka tonge na madaraka kwa udi na uvumba....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Watawala wetu wametufanya wapuuzi na wajinga...hawana tena muda na sisi waliokuwa wakizunguka na magari wakiomba ridhaa zetu za kutuongoza...badala ya kuwa viongozi wamegeuka kuwa watawala na kwenda kinyume na matarajio yetu....wanayapa vipaumbele matumbo yao na ya familia zao kuliko sera zao walizotuaminisha kuwa ni nzuri kwenye kampeni zao....wengi wamegeuka mabilionea kama sio mamilionea baada ya kuwapigia kura za kutuwakilisha....hawana tena huruma nasi bali wanachojali ni matumbo yao na mifuko yao.......utashindwaje kuwa milionea ikiwa tu kukaa tu bungeni kwa masaa kadhaa na kusinzia unalipwa posho ambayo ni sawa na mishahara ya watumishi wengine??....

.utashindwaje kuwa milionea ikiwa mtu unapokea mamilioni ya pesa kama mshahara kwa kukaa tu bungeni na kusinzia???.....wengine mpaka wamevimbiwa na mali mpaka wanaita bilioni moja ni vijisenti......wengine wanaitwa mamilioni ya kodi za wavuja jasho kuwa ni hela ya mboga....katika hali halisi ni mambo yenye kushangaza kama sio kustaajabisha.....uongozi wa umma sio tena kwa ajili ya kuwatumikia wananchi bali ni nafasi adimu ya kujilimbikizia mali...katika mazingira kama haya haishangazi kuona kuwa kila mtu anataka kuwa mwanasiasa..........Kitu pekee wanachokisahau watawala wetu ni kwamba hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho....haijalishi mwisho huo uwe mbaya au mzuri....uwe wa kukaraisha au wa kufurahisha....lakini ukweli unabaki kuwa kila lenye mwanzo basi halikosi mwisho....itafika wakati WATANZANIA

watachoka kuona mahospitalini hakuna dawa wakati wanalipa kodi kila kukicha lakini kila siku wanawashuhudia watawala wao wakipishana angani kwenda kutibiwa nje ya nchi tena kwa kodi zao huku wao wakifia kwenye korido za mahospitali kwa kukosa tiba....itafika kipindi WATANZANIA watachoka kuona watawala wao wakijichotea mali za umma bila kujali zao huku mamlaka husika zikiwatazama bila ya kuwachukuli hatua.....itafika kipindi kina mama wa vijijini watachoka kutembea kilometa zaidi kumi kutafuta maji ambayo hata hivyo sio safi na salama huku kila siku wakishuhudia watawala wao wakimwagilia maua na kulisha mifugo maji safi na salama yaliyotokana na kodi zao......itafika kipindi vijana wa taifa hili watachoka kuona wanabaguliwa kwenye ajiria kutokana na nafasi zao kuchukuliwa na watoto wa watawala huku wao wakizeekea vijiweni wasijue kesho yao itakuwaje..

..........itafika kipindi waalimu watachoka kuona serikali ikigoma kuwalipa madai yao yaliyoota sugu kwa kisingizio cha ukata wa nchi huku wakishuhudia viongozi wao wakijilipa posho zisizo na kichwa wala miguu.....itafika wakati wanafunzi nao watachoka kukaa chini huko madarasani na kugombea kitabu kimoja huku wakiwashudia wanafunzi wenzao wakipelekwa kusoma nje ya nchi na wengine wakipelekwa shuleni na mabasi ya shule....huku wao wakitembea umbali mrefu kuifuata shule........itafika nyakati hata maaskari watagoma kupokea amri kutoka kwa mabosi wao wanaoshinda maofisini wakila kuku kwa mishahara minono wanayopeana kwenda kuwavunja viuno walala hoi wenzao wanaoandamana kudai haki zao...

.....itafika wakati wananchi watachoka na manyanyaso na mateso wanayofanyiwa na watu wanaojiita wawekezaji ndani ya ardhi yao huku wakingiwa vifua na watawala.....itafika kipindi hata wahisani watagoma kuchangia bajeti yetu kutoka kuzidi kuongezeka kwa pengo la walionacho na wasionacho baada misaada yote kuishia kwenye matumbo ya watawala wetu...na huo ndio utakuwa mwisho wa utawala dhalimu, utawala usiojali wananchi wake, utawala kiburi, utawala jeuri na hapo ndipo itakapokuwa mwanzo wa

HISTORIA MPYA.........PENYE DHURMA HAKUNA AMANI............THE DAY WILL COME............TIME WILL TELL
 
Inasikitisha kuona wagonjwa mahospitalini hawapati dawa wala chakula. Huu ni unyama. Tuamke.
 
Mkuu "kikulachochako"umemaliza kila kitu mwenye akili ametambua umeandika nini
 
Daaa Nikiona Escrow nakumbuka Fedha zangu zote za Service Charges Tanesco.
 
Hilo linajulikana Mkuu, Rais kayakimbia majukumu yake sasa kamuachia Katibu wake ndiye awe anatangaza maamuzi ya Rais.
Kinacho nisikitisha ni jinsi wabunge wengine wa
ccm wanavyo shindwa kupata tafsiri ya kauli ya serikali kupitia Katibu mkuu kiongozi. Ujumbe anaotoa Sefue ni kwamba Ikulu imedharau azimio la bunge na zile taarifa za CAG na PCCB.
Nasikitika kwa vile wangekuwa wameijua tafsiri hiyo hata wao wangeungana na Serukamba na wabunge wa upinzani kuikona serikali katika jambo Hilo, lakini ukiona jinsi mishipa ya shingo inavyo wasimama kuitetea serikali unatambua kuwa hawa ni mbumbumbu hawajui kinachoendelea au watu walio uza utu wao na wa waliowachagua kwa kulambishwa sukari
 
Hii ni sarakasi ya kujaribu kumsafisha mmoja kati ya potential candidates wa URAIS ili aingie kwa mtindo wa Mzee RUKSA!! Sasa team Lowassa wamelibaini hilo, ndio maana wanalipinga kwa nguvu zao zote!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Historia ya IPTL inajieleza vema sana ... wote tulitegemea haya kutokea!!!
 
Kinachonishangaza na uamuzi huu ni kwamba siku hizi hakuna uwajibikaji. Watu waliuawa na kuteswa katika operesheni tokokeza, hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika na kujiuzulu kwa mawaziri wa wizara zilizohusika ilikuwa sahihi. Sasa leo Ombeni Sefue anakuja kutuambia kuwa mawaziri hawakuhusika? Mwinyi alijiuzulu mwaka 1975 baada ya wafungwa kufariki gerezani Shinyanga. Mwinyi hakuwaua wafungwa hao, lakini kama waziri mwenye dhamana alijiuzulu. Hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa wakati wote.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hii serikali imezidisha double standards kwakweli mpaka wanatia kichefu chefu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huu ujinga unafanyika tanzania tuu badala ya watuhumiwa kupelekwa mahakamani kujibu shtuma hizo wanasafishwa na wahusika wao hili dili la pesa za ESCROW uliwanufaisha vigogo wakubwa sana ndo maana wameshaanza kuwasafisha kuna ile kauli mwaga ugali na mimi nimwage mboga .lakini ni vema serikali ya ccm ikatambua wananchi wa sasa siyo wale wa zamani .UKAWA hii nafasi nzuri kujipanga kuchukua dola tusiposhinda uchaguzi huu basi tusitegemee tena kuja kushinda .
DSC011181.jpg
Hizi BAKORA 6 zinatosha kabisa kuindoa madarakani serikali ya ccm.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom