Pinder ndio nani tena?
Sina hakika kama uko sahihi kwenye red bold. Kama Pinda ndiye alitoa maagizo ya uchunguzi kufanyika, kwa nini matokeo ya uchunguzi yapelekwe bungeni?? Kwa kumbukumbu zangu, bunge liliamuru uchunguzi huo ufanyike, na ndiyo maana hata kale ka-memo kutoka mahakamani kaligonga ukuta pale Idodomya.
Hata wewe unakuja na hoja marehemu hapo hakuna kupanga ngoja ukweli uchukue mkondo wake....Mzee Pinda yuko vizuri....ni ukweli usiopingika kuwa Pinda ni kati ya PMs waadilifu na waelewa ukimtoa Mzee wetu late Moringe S....tusubili...
Kuna taarifa kwamba Pinder amewapanga wabunge kadhaa (majina kapuni) wamtetee bungeni leo ili asiende na maji. Kwa kufanikisha utetezi wao wanadai kwamba Pinder hajahusika yeye binafsi katika ufisadi huu bali ni watendaji wa chini yake ndio wanapaswa kuchukuliwa hatua.
Kete ya pili wanayotumia 'watetezi' hawa ni kwamba ikiwa Pinder alihusika kwenye ufisadi huu basi asingeagiza uchunguzi ufanyike. So the guy is clean and innocent.
Aidha, kuna timu kubwa imetumwa kumtetea Pinder kwenye social media, hasa JF, kwa lengo la kuupotosha umma na kuwafanya wananchi wasadiki kwamba Pinder anaonewa bure.
Kisingizio kingine kitakachotumiwa kumsafisha ni uwepo wa makundi ya urais, 2015 yanayochafuana.
Anyway, ngoja tusubiri tuone hao vibaraka wake wamejipangaje kumtetea kwa kuwa naona kama wanatumia hoja mfu kumsafisha mtu ambaye amechafuka kiasi cha kutosafishika tena. Mbivu na mbichi tutazipata leo bungeni wakati utetezi wa serikali (utakaotolewa na Pinder mwenyewe) utakaporindima.
Nawasilisha
:israel: