ESCROW scandal: Pinda apata watetezi

Hata ile kauli yake ya wapigwe tu, maana wametuchosha!! Hiyo nayo inatosha kuachia ngazi.

hiyo kauli hadi leo mimi naitafakari, ilitosha kabisa kumuwajibisha maana ilikuwa ni ukiukaji wa wazi wazi wa sheria na katiba ila kombe lilifunikwa ili mwanakharamu apite!
 
kama alikosa watetezi kwenye ile kamati basi tena ile report imekaa vibaya. utetezi wake ilikuwa kuzuia uchunguzi usifanyike. Au ccm wamezoea kufukia fukia Mambo?
 
PAC hawakuonyesha kwanini wanasema pesa ni za umma. Waache upande mwingine ujitetee.
PAC wame-rely kwa mkurugenzi wa TAKURURU.
Kiuchunguzi ilibidi aseme ni za serikali, lakini CAG na TRA wameongea kitaalam kuwa kuna element ya kodi, ambayo ni mali ya umma.
PAC wangechukua maelezo ya CAG na TRA

Wote unaowataja wanaishia kwenye mwisho mmoja, kuwa waliotajwa wamehusika kushawishi, matumizi mabaya ya ofisi, kutofuata taratibu au uzembe kazini na yote haya hayawaachi salama!!!
 
Kuna taarifa kwamba Pinder amewapanga wabunge kadhaa (majina kapuni) wamtetee bungeni leo ili asiende na maji. Kwa kufanikisha utetezi wao wanadai kwamba Pinder hajahusika yeye binafsi katika ufisadi huu bali ni watendaji wa chini yake ndio wanapaswa kuchukuliwa hatua.

Kete ya pili wanayotumia 'watetezi' hawa ni kwamba ikiwa Pinder alihusika kwenye ufisadi huu basi asingeagiza uchunguzi ufanyike. So the guy is clean and innocent.

Aidha, kuna timu kubwa imetumwa kumtetea Pinder kwenye social media, hasa JF, kwa lengo la kuupotosha umma na kuwafanya wananchi wasadiki kwamba Pinder anaonewa bure.

Kisingizio kingine kitakachotumiwa kumsafisha ni uwepo wa makundi ya urais, 2015 yanayochafuana.

Anyway, ngoja tusubiri tuone hao vibaraka wake wamejipangaje kumtetea kwa kuwa naona kama wanatumia hoja mfu kumsafisha mtu ambaye amechafuka kiasi cha kutosafishika tena. Mbivu na mbichi tutazipata leo bungeni wakati utetezi wa serikali (utakaotolewa na Pinder mwenyewe) utakaporindima.

Nawasilisha
:israel:
Mwenzie EL aliachia ngazi katika mazingira rafiki kuliko haya ya kwake. Pia ofisi yake kwenda kufungua kesi kuzuia bunge lisifanye kazi yake ni dosari kubwa zaidi.
 
Pinda hafai hata kidogo kuwa raisi kwani Nchi itakuwa ya hovyo hata kuliko ilivyo sasa hivi. Tunahitaji raisi Imara, shupavu, mwenye maono, mzalendo na mkali ili kurekebisha nchi kwani kwa miaka hii 10 imekuwa hovyo kabisa.
 
Wote unaowataja wanaishia kwenye mwisho mmoja, kuwa waliotajwa wamehusika kushawishi, matumizi mabaya ya ofisi, kutofuata taratibu au uzembe kazini na yote haya hayawaachi salama!!!
Hizo ni conclusions za PAC.
 
Hata wewe unakuja na hoja marehemu hapo hakuna kupanga ngoja ukweli uchukue mkondo wake....Mzee Pinda yuko vizuri....ni ukweli usiopingika kuwa Pinda ni kati ya PMs waadilifu na waelewa ukimtoa Mzee wetu late Moringe S....tusubili...
 
PM ukisikiliza na kama ukiisoma ripoti hajashiriki kupiga deal, bali ameshauriwa kuwajibika kisiasa. Naona PCCB na CAG wamefanyakaz yao vema. Na hata PAC wmefanyakaz vema. Na kujiridhisha ni kuwa Gavana wa BoT na Wakuu wa TRA kwenye mapendekezo hawajaguswa, hivyo wako clean, ikiashiria kuwa ueledi ulitumika katika ukusanyaji wa Taarifa iliyopelekea kupata ripoti ile ya PAC!
 
hata lowassa nae alijiuzuru kutokana na uzembe wake kama PM kwenye saga la richmond,na Pinda nae ajiuzuru kutokana na uzembe wake kama PM kuruhusu haya madudu yatokee mbele yake.....cheo ni dhamana sio mali ya baba au mama yake go to he.ll mtoto wa mkulima.
 
PM ukisikiliza na kama ukiisoma ripoti hajashiriki kupiga deal, bali ameshauriwa kuwajibika kisiasa. Naona PCCB na CAG wamefanyakaz yao vema. Na hata PAC wmefanyakaz vema. Na kujiridhisha ni kuwa Gavana wa BoT na Wakuu wa TRA kwenye mapendekezo hawajaguswa, hivyo wako clean, ikiashiria kuwa ueledi ulitumika katika ukusanyaji wa Taarifa iliyopelekea kupata ripoti ile ya PAC!

Pinda ana hukumiwa kwa nafasi yake ya PM kama mtendaji mkuu wa serikali alikua na nafasi ya kuzuia wizi huu mkubwa but alikua wapi? tena kanukuliwa akisema "IPTL deal is clean" na pesa za tgt escrow si za "umma" what does it mean? huu ni uzeme kazini na mistake kama hizi ndizo zilizo mcost EL......pinda aka pumzike tu amekula vya kutosha.
 
Shida nikwamba,sisi mitandaoni na baadh ya vijana ndo hatumtaki huyu bwana.

Lakini,nyuka ya pazia jamaa(#pinda) anawatu Lukuki wanamhîtaji mno. Kuna wakulima,wafugaji,wavuvi & idadi ndogo ya wafanyabiashara.

#MY_TAKE ,
Huyu jamaa hachafuki kirahisi kwakweli. unless tuwaombe kina Lowasa wakate buti hukohuko mjengoni. Vinginevyo,sijui!!!!!!

Kwahiyo unataka kutuambia akina Lowassa ndio wako nyuma ya shutuma hizi?
Pinda naye hakuwa makini! Alizembea sana, alilala usingizi bila kuwa makini na Lowassa!
Hakujua kua Lowassa atatumia karata ya kuteleza kwake kuwa ndiyo njia ya kuelekea Ikulu!
Pole sana mwana wa Mkulima!
 
Huyu jamaa is so weak bdo tu anataka Kuwa Rais?for that matter bora ya Lowassa kuliko PM ingawa wote wezi
 
Pinda ana hukumiwa kwa nafasi yake ya PM kama mtendaji mkuu wa serikali alikua na nafasi ya kuzuia wizi huu mkubwa but alikua wapi? tena kanukuliwa akisema "IPTL deal is clean" na pesa za tgt escrow si za "umma" what does it mean? huu ni uzeme kazini na mistake kama hizi ndizo zilizo mcost EL......pinda aka pumzike tu amekula vya kutosha.

Nawashangaa sana, report ni maandishi. Maandishi yapo kila mahali. Pinda alijifanya hamnazo kwa kusema bungeni na nje ya bunge eti hela za escrow si za umma. Umma au serikali haina interrest katika fedha zile. Hii ilikuwa ndo PR strategy ya Karasinga and Pinda should have known better.

Kama na pinda atapelekwa mahakamani atakuwa mtu rahisi zaidi kutia hatiani kuliko hata hao wengine. He was just too compromised kusema hakuwemo! He was a shame as a PM.
 
Hao lazima watakuwa kina ja pipo, maji marefu, lukuvi, wasira na ------ wengine walioko kule kwa ajili ya upatu.

Pinda hawajibishwi kwa ajli ya kuiba, bali ni kwa ajili ya kushndwa kazi yake katika kuridhia wizi huo na kutetea wzi kwa kutoa taarifa za uwongo huku akijua.

Kuunda tume ya kuchunguza alishinikizwa na external forces. Hakuwa na sababu ya kurdhia wizi huo na kuutetea kwa uwongo, huku akisubiri aje kuunda tume. Upuuzi mtupu.

Jamani tusimamieni maslahi yetu wenyewe, watawala hawa hawaaminiki. Wenye uelewa wameeelwa.

Back
Top Bottom