Escrow Saga: Taratibu kwa Kibunge zikoje ikiwa Mh. Rais hatafanyia kazi mapendekezo ya Bunge?

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
12,034
13,417
Wakuu habari za usiku huu,
Nafikiria mambo kadha yanayoendelea nchini na hatimaye nimeibuka na swali ambalo kimsingi nimeshindwa kupata jibu la moja kwa moja.

Hivi taratibu za kibunge zikoje ikiwa Mh. Rais hatafanyia kazi mapendekezo ya Bunge na hasa kwa hili sakata la Tegeta escrow?, yaani bunge litafanya/linaruhusiwa kufanya nini kisheria?

Naomba tu kujuzwa ili niwe na picha halisi ya nini kinaweza tokea ikiwa ukimya huu wa Mkuu wa nchi utaendelea hadi kikao kingine cha bunge kitapokaa tena hapo Januari 27 ambapo pamoja na mambo mengine ni kupitia utekelezaji wa maazimio hayo ya bunge.

Karibuni wadau!

Raisi halazimishwi na taasisi ye yote kufanya maamuzi yake,mapendekezo ya bunge raisi akiyapuuza inakuwa ndio mwisho wa mchezo hakuna hatua inayoweza kuchukuliwa.
Ila kwa kuheshimu mhilimili mwingine wa dola raisi huchukuwa hatua ikizingatiwa kuwa ni bunge lenye uwezo wa kikatiba kumtoa raisi madarakani kwa kutokuwa na imani naye.
 
Ni kweli bunge laweza kupiga kura ya kutokuwa na iman"vote of no confidence" na mkuu. Hivyo naye akaungana na madhambi yake
 
Wapigaji ya kura ya kutokua na imani na rais wenyewe ni wachache it is a lost cause anyway.
 
Hili swali aliliuliza muheshimiwa Simbachamwene siku ya pili kutoka mwisho ya mjadala wa escrow, akazimwa na Spika kiaina hakujibiwa.

Bunge la Tanzania hata kuuliza hili swali inabidi lipigiwe kura na kukubalika kuulizwa na angalau asilimia 20 ya wabunge, siku zisizopungua 30 kabla ya kusikilizwa, kwa maana kumjadili rais katika bunge la Tanzania hakutofautishwi sana na an impeachment motion.

Bunge lilitakiwa kumu impeach rais kutoka mwanzo.

Now, to answer your question.

In theory rais akikalia maazimio ya bunge anaweza kupigiwa kura ya impeachment na bunge, wabunge zaidi ya theluthi mbili wakisema ashitakiwe (ndoto kwa sasa) atashitakiwa kwa mujibu wa ibara ya 46 na 46A za Katiba ya Jamhuri ya Muuungano ya Tanzania.
 
Tatizo wengi hawajui maazimio ya Bunge yaliagiza nani afanye nini.Sehemu kubwa ya maazimio ya bunge yaliagiza vyombo husika vya uchunguzi vichunguze na hatua stahiki za kisheria zichukuliwe kwa wale watakaobainika beyond reasonable doubt kuwa ni wahalifu.Raisi sio usalama taifa,Takukuru,polisi,mwendesha mashtaka wala mahakama ambao ndio sehemu kubwa ya maazimio hayo ya bunge yanawagusa.

Nchi hii inatawaliwa na sheria.Azimio la Bunge halikuagiza raisi kuwa anza fukuza fukuza kienyeji.
Hatua iliyopo ni ya vyombo vya uchunguzi wa hizo tuhuma zilizotolewa na CAG,PAC na bunge.
Vikimaliza kazi zake wa kupelekwa mahakamani watapelekwa wa kutimuliwa na raisi watakaonekana wana hatia watatimuliwa na bunge litapewa taarifa sasa ni bunge lipi litapewa hizo taarifa ni lijalo au mabunge yatakayofuata baada ya uchaguzi hilo sijui sababu itategemea vyombo vilivyokabidhiwa hiyo kazi kama vitakuwa vimemaliza kazi walizopewa kutegemeana na utaalamu wao na uwepo wa nyenzo za kazi sababu kufuatilia hii kesi kutahitaji pesa za watu kusafiri ndani na nje na mambo mengine lukuki.Kwa hiyo hiyo deadline ambayo bunge lilitoa ni laymen deadline sababu bunge lilitoa deadline blindly bila kujua ukubwa wa hiyo kazi sababu wao si wataalamu wa hayo mambo.

Sasa hivi vyombo husika ambavyo bunge liliagiza vinayafanyia kazi.Na vikiwa vinayafanyia kazi huwa havishindi ukumbi wa habari maelezo kujieleza kuwa leo tumeamka asubuhi tuko kwenye daladala kwenda kumhoji mthumiwa wa Escrow.

Tulieni acheni mihemuko
 
wewe unapotosha
1.Mamlaka husika zitengue uteui wa Werema, Muongo na Maswi
2.vyombo vya uchuguzi viendelee na uchunguzi kupata data za wahusika hawa na wengine na kuwafikisha mahakamani
kumbuka watuhumiwa hawawezi kuchunguzwa ikiwa bado wapo madarakani
Mwambie Tezi Dume kuwa amedharau bunge na amedharau ushauli wa idara usalama wa Taifa sasa moto unakuja
 
Back
Top Bottom