Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,577
- 113,770
- Thread starter
- #61
Nimenote mjadala mkubwa unaendelea baada ya Ngeleja kurejesha fedha za mgao wa escrow!, kwangu mimi huu ni muendelezo tuu wa hii hii ignorance niliyoizungumzia humu, tangu lini kupokea pesa au zawadi yoyote ikawa ni kosa?, kama wakati ukipokea, hukujua kama fedha hizo ni za wizi?.Wanabodi,
Kwa Nini Watu Wanataja Taja Tuu Majina?, Huu Kama Sio Ujinga ni Nini?!.
Watu wanataja taja tuu majina!, wananyooshea watu vidole!, wanawapigia kelele waliolipwa na JR tuu, waliolipwa na PAP wao wako wapi?, Walioileta IPTL wako wapi?, hii ni nini kama sio ignorance?!, au tumelogwa?!. Tunapaswa kuwatafuta responsible people tangu hili jinamizi la IPTL limekuja nchini, tuwawajibishe!, na sio kutafuta mbuzi wa kafara, au kama kawaida yetu, tufunike kombe mwanaharamu apite!".
Paskali
Ila pia ignorance kubwa ni kushadadia wanaojulikana walipokea, jamani hawa ni wachache na walichopokea ni just a peanut!, wako Watanzania wenzetu, walipokea migao mikubwa ya fedha za wizi, kikiwemo chama fulani kilipokea mgao wa bilioni 40 za Kagoda, watu walipokea mgao wa Rada, Meremeta, Deep Green, Tan Gold, DCP, lakini kwa vile hawajulikani, they are OK!.
Mungu ibariki Tanzania.
Paskali.