KASHOROBAN
JF-Expert Member
- Apr 7, 2017
- 859
- 738
Ethiopia ya kale ndo iko mawazoni mwako, waziri mkuu wao kawa mtamu kwa democracy mpaka kapata Nobel prize, chezea wenye roho nzuri weweWanafanana kwa kiasi kikubwa na wakoloni wao Waethiopia. Ethiopia hairuhusuiwi kwa raia kuwa na akaunti ya $ hata kama mwajiri wake analipa kwa $. Na kwa wageni kama watu wanaofanya kazi balozini wanaruhusiwa kutoa kiasi kidogo tu (nadhani US$300 hivi) tu tena baada ya kuonyesha tiketi ya ndege kuwa una safari ya nje ya nchi. Yaani hao Waeritrea wamechukuwa sheria za Waethiopia waliowatawala kama sisi tulivyochukuwa za Waingereza hata baada ya kupata uhuru wetu. Kama maisha yalivyo magumu Eritrea, ndivyo yalivyo magumu Ethiopia. Kama kulivyo na kampuni moja ya simu Eritrea, hivyo hivyo Ethiopia. Kama Waeritrea wanavyokimbia nchi yao, hivyo hivyo Waethiopia.
mi nachangamsha tu mjadala. hawa ni wanawake wa ki-eritrea.View attachment 1234372View attachment 1234374View attachment 1234375View attachment 1234376View attachment 1234377View attachment 1234378View attachment 1234380View attachment 1234382
Mambo ya 'UKUTA' marufuku !Wewe na wenzako hamjui mnachoongea. Eritrea na Ethiopia walianza hivi hivi kama Jiwe anavyo-jimwambafai. Mara hiki kimezuiwa leo, mara kile kimezuiwa kesho. Mwisho wakafika hapo walipo leo. Kama hamna akili ni vizuri kunyamaza na kula ugali wenu kimya kimya na kuwaacha wenye akili walinde uhuru wenu wa kikatiba.
...mnahangaika !Mbona hata hapa jiwe anatuburuza apendavyo. Ni kama hapa tu, kinachofanyika mpaka kufikia huko vyombo vya dola hutumika na sana ni kwakupewa mishahara minono, na hawasumbiliwi wala kukaguliwa vyeti fake. Vyombo vya dola huweza kufanya lolote na hutekwa na maneno ya viongozi kwa kujifanya wazalendo, ghiliba hiyo huwaingia vyombo vya dola na hasa ukizingatia mishahara na marupurupu manono wanayopewa hugeuka vipofu wa unyama wote. Kisha huundwa kundi la watu wasiojulikana, hili hufanya ukatili wa kutisha huku vyombo vya dola vikifumbia macho mambo hayo, mfano hapa kwetu. Viongozi wa vyombo vya dola huhongwa vyeo na kuwa upande wa kiongozi kwa lolote mfano hapa kwetu. Chaguzi zote huwa kiini macho, na wanaotangazwa washindi ni wale wanaotakiwa na mtawala ili kumpitishia sheria zake za ukandamizaji, mfano huo pia uko hapa kwetu.
Bunge na mahakama nazo hujikuta katika hali hii ya kutii kila kitu kwani kundi la watu wasiojulikana hutumika kumnyamazisha yoyote anayekuwa kikwazo. Gia inayotumika kupandikiza unyama wote huu ni neno uzalendo. Yoyote asiyemtii mtawala huonwa ni msaliti. Wakati hayo yakiendelea zaidi ya nusu ya wananchi hulishwa propaganda na ghafla nchi nzima hujikita ikimsifia mtawala wa aina hiyo. Mifano ya mambo hayo iko wazi hata hapa nchini.
Hao fastjet na precision walikuwa wanahonga watu waiue ATCLMkuu usiseme afadhali ya Tanzania wakati,Magufuli ndo anatamani tufike huko, wakati wa kikwete hali haikuwa Kama ilivyo leo.
Endapo Magufuli atang'ang'ania madarakani na sisi Tanzania tutakuwa kama Eritrea pia, kwanza mpango wake ni kuua sekta zote binafsi ,Tazama alivyoiua fast jet ili ATCL iinuke, amezima uhuru wa Habari hata humu JF yale mazito tunayoandika mods wanayafuta kwa hofu ya kukamatwa.
Tatizo letu Watanzania ni kukosa kumbukumbu. Mtu kasema hadharani kuwa anatamani malaika wangeshuka kuja kuzima mitandao; sijui watu walidhani anamaanisha nini.
Ethiopia ya kale ndo iko mawazoni mwako, waziri mkuu wao kawa mtamu kwa democracy mpaka kapata Nobel prize, chezea wenye roho nzuri wewe
Wengi ni mawakala Wa mashetani.Uwatoa kafala waafrika wenzao kwa ahadi ya kudumu madarakani.Wengi ni uncivilized japo walipita darasaniMimi sijui huwa wanafaidika nini kwa kuwaonea watu wao kiasi hiki.
Ni mindset mbona wwenzetu nao walitawaliwa Leo wako mbali wakikimbizana kiuchumi na waliowatawala.Hali Africa imerudi nyuma baada ya uhuru heri wangewaacha waendelee kutawalaHujiulizi wazungu wachache waliwezaje kutufunga minyororo kwenye ardhi!,...mchawi wa waafrika ni yule anaetufundisha historia ya kwamba tulitawaliwa ...hi ni historia mbaya ambayo hatupaswi kuijua...maana inatufanya tujione waovyo
Mkuu ni warembo kweli ila mila zao za kutoa FGM sijui Kama wameacha
Kama raia wao walizamia Tanzania........basi Eritrea ni sawa na kule kwa lusiferi.........
mi nachangamsha tu mjadala. hawa ni wanawake wa ki-eritrea.View attachment 1234372View attachment 1234374View attachment 1234375View attachment 1234376View attachment 1234377View attachment 1234378View attachment 1234380View attachment 1234382
Unadhan ww usingepata usingenyooka?Natamani iritrea ingekua bongo...yani hawa wakina Kiduku Lilo ndo wangenyooka
kumbe wako wachache hivyo, million 5 tu, hata watu wa dar ni wengi kuliko nchi mzima ya Eritrea!!!!!?Asante kwa nondo mkuu upo vizuri.
Si Afrika tu bali hata Ulaya. Mpaka leo Ulaya na hasa Ujerumani inajiuliza swali hilo hilo. "Hivi mtu mmoja anawezaje kuwaburuza mamilioni ya watu atakavyo?"